NIDA Mnakwama Wapi?

Mimi nimetuma 100 kwenye ile namba *152*00# kwa ajili ya kupata namba toka juzi hawajaituma hiyo namba na mia yangu wamekula
 
Miezi saba unalalamika mkuu!!! Mimi nilijaza fomu ya kitambulisho cha uraia tangia mwaka jana mwezi 2 hadi leo sijaona kitu!

Baadaye wakaleta namba za kutupiga pesa bure bure!
 
Asante mkuu kwa Maelezo murua!
 
Kwa hiyo huu ubabaishaji viongozi wa serikali ni wahusika?Kama ni hivyo kwanini walianzisha hilo zoezi wakati wanajijua hawana nia thabiti ya kulifanikisha si wangeacha tu ?Kwani kuna raia aliyedai hivyo vitambulisho kuwa navyo?
Kwani mfumo wa vyama vingi wanautaka! Wanajilazimisha tu ndiyo maana mtu anatangazwa mshindi eti kwa sababu watu walivua mashati ukumbuni wakati wa kuhesabu kura!
 
Nimejaribu kufuatilia nakala mtandaoni bila mafanikio ni kama system Yao ime-collapse hivi sasa sjui kama ni kwangu tu au na wengine ni hivyo hivyo??

Aliyefanikisha kupata nakala kwa njia ya mtandao kama yupo atusaidie...
 

Kuhusu NIDA wanakwama au wamekwama wapi sasa nadhani Jibu sahihi atakuwa nalo DG wa Idara Muhimu Tanzania nzima iliyopo Oysterbay mkabala na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro.
 
Kuhusu NIDA wanakwama au wamekwama wapi sasa nadhani Jibu sahihi atakuwa nalo DG wa Idara Muhimu Tanzania nzima iliyopo Oysterbay mkabala na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro.
Mbona hapo ni km jumba jeupe ,wazee wa Kaunda suti.Wanahusikaje na NIDA?
 
Mbona hapo ni km jumba jeupe ,wazee wa Kaunda suti.Wanahusikaje na NIDA?

Ina maana hujui kwamba Bosi wao ndiyo alikuwa anaijua NIDA kuliko hata aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana DM ambaye hivi sasa Kesi zinamuandama tu hadi anatia Huruma wakati kama ni Kula ( Kufisadi ) NIDA walikuwa wengi ila Msala wote umemuangukia Yeye na Wenzake wachache.
 
Hivi hii huduma ya kupakuwa online bado ipo ukiwa na no.?
 
Nimejaribu kufuatilia nakala mtandaoni bila mafanikio ni kama system Yao ime-collapse hivi sasa sjui kama ni kwangu tu au na wengine ni hivyo hivyo??

Aliyefanikisha kupata nakala kwa njia ya mtandao kama yupo atusaidie...
Mkuu unakwama wapi!? Mbona kwenye tovuti ni rahisi sana!?? Ukifungua tovuti unapata maelezo gani!??
 
hii mambo ya kuzima cm si wangetanguliza. tungepumzika na mambo ya social media. tumechoka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…