NIDA Mnakwama Wapi?

Jackal

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
10,258
Reaction score
14,106
Jana nilienda kurekebisha kitambulisho changu cha kupiga kura ,mkoani Arusha.Zoezi lilichukua takribani dakika 20.Toka kujaza fomu,kupigwa picha hadi kupewa kitambulisho.

Nimejaza fomu za NIDA toka mwezi January mwaka huu.Kitu cha ajabu hadi Leo,miezi saba imepita sijapata kitambulisho.Kwanini NIDA wasijifunze kwa wenzao wa tume ya uchaguzi?Wakishahakiki taarifa zako,ukapigwa picha basi na wao wangetoa kitambulisho hapohapo badala ya kuzungushana.

NIDA na tume ya uchaguzi zote ni idara za serikali.Sasa nataka kujua NIDA mnakwama wapi?
 
serikali ya CCM inahitaji wapiga kura wengi kuliko inavyohitaji wamiliki wa vitambulisho vya taifa.
 
Kitambulisho cha kupigia kura hakina faida kwako kinafaida kwao uwachague wapate uraisi,ubunge na uwaziri ndio maana ukikitaka hausumbuliwi

Na hichi cha NIDA wao hawana faida nacho ila wewe ndio unafaida nacho maana usipokuwa nacho mambo yako mengi yana kwama kwa hiyo hata ukichelewa kukipata wao hawajali

Lakini siku itakapo amuliwa kuwa wenye NIDA I'd ndio watakao piga kula utaona siku hiyo hiyo ukienda utakipata ili mambo yao yasikwame
 
miezi saba unalalamika!!
sisi wenzako mwaka wa tatu huu sasa hakuna kitu,,,,,,,,,,,
Ndio maana nauliza sijui hawa jamaa wanakwama wapi?
 
Ujue kuna siasa(kitambulisho cha kura) na utaifa(kitambulisho cha uraia)
 
Ni kweli sijui wana kwama wapi Nilivyo ziangalia zile process za NIDA hazina tofauti na process za kutoa kitambulisho cha NEC
NEC kupiga picha hadi kuprintiwa haizidi dakika 30 lakini wao NIDA siku 60 na unaweza ukaenda ukambiwa bado
Naamini hata Kenya na Uganda upuzi kama huu hawana
Na tunajijua ugoigoi wetu ndio maana tunaogopa kuingia jumla jumuia ya afrika mashariki

Maana zingetokea furusa zinahitaji kitambulisho cha taifa Kenya na Uganda wao wangepata kwa siku moja sisi Tanzania siku 60 sasa hadi ukipata hiyo fursa itakuwepo
 
Heri yako wewe ambae hata mwaka mmoja hujamaliza wengine tumejiandikisha tangu 2016 mpaka leo hola tu.
 
Jiongeze mkuu, we kaa tu hapo ungoje uletewe.
 
Kwa hiyo huu ubabaishaji viongozi wa serikali ni wahusika?Kama ni hivyo kwanini walianzisha hilo zoezi wakati wanajijua hawana nia thabiti ya kulifanikisha si wangeacha tu ?Kwani kuna raia aliyedai hivyo vitambulisho kuwa navyo?
 
Heri yako wewe ambae hata mwaka mmoja hujamaliza wengine tumejiandikisha tangu 2016 mpaka leo hola tu.
Nafikiri huu uzembe tuupige vita kwa nguvu zote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…