NIDA Imevunja Katiba ya Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NIDA Imevunja Katiba ya Nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sophist, Jul 15, 2012.

 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,730
  Trophy Points: 280
  NIDA Imevunja Katiba ya Nchi

  Mamlaka ya Vitambulisho Nchini Tanzania (NIDA) yamekiuka Katiba ya Nchi. NIDAimeundaa mfumo wa kukusanya taarifa za wakaazi nje ya mfumo rasmi wa serikaliuliowekwa na kutambuliwa kikatiba.

  Mfumo uliondaliwa na NIDA unamtambua Mjumbe wa Nyumba Kumi wa CCM kamaMamlaka rasmi ya kuthibitisha uhalali wa ukaazi wa mwananchi anayejiandikishakupata kitambulisho cha taifa.

  Kwa mujibu wa Katiba na sheria Mjumbe wa Nyumba 10 si sehemu ya mfumo wauongozi wa dola. Mamlaka rasmi wa uongozi wa dola unaanzia kwa Mwanyekiti waMtaa (mijini) au Mwenyekiti wa Kitongoji (vijijini).

  Uchunguzi nilioufanya Jijini Dar es Salaam umebaini kuwa mwananchianalazimishwa kumtambua/kutambuliwa na Mjumbe wa Nyumba 10 ili akubaliwekuorodhesha majina ya watu katika kaya yake. Aidha, upande wa kulia katika vitabu(template)vya NIDA unaonesha na kumtaka karani wa NIDA kuandika jina la Mjumbewa Nyumba 10 kama mdhamini kuthibitisha ukweli wa taarifa za mkaazi.

  Vilevile, maudhui ya mafunzo kwa makarani wa NIDA yanaonesha (makaraniwamefundishwa hivyo) kuwa Mjumbe wa Nyumba 10 wa CCM ni mamlaka rasmi na kamilikuthibitisha uhalali wa ukaazi wa wanakaya.

  Kana kwamba hiyo haitoshi, NIDA inawalipa pesa wajumbe wa nyumba 10 wa CCM kwakazi ya 'kuandaa' wakaazi katika himaya yake ya nyumba 10. Yaani kazi wa uwelediya kuhamasisha watu kujiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifawamepewa Wajumbe wa Nyumba 10 wa CCM bila hata kufuata sheria ya manunuzi yaumma ya 2004.

  Ni vigumu kuamini kuwa uamuzi huu wa NIDA umetoke kwa bahati mbaya. Hapana.Ni mkakati rasmi wa kisiasa wa Serikali na CCM kutumia fursa, hata kwa kukiukaKatiba na sheria, kujiandalia na kujihakikishia wapiga kura wa 2015. Ni mkakatisawia na ule ulioasisiwa na Komandoo Salmin Amour Zanziba enzi hizo kuzuiaWazanzibari, wengi wao wakiwa Wapemba, wasipate fursa ya kupiga kura katikachaguzi zilizofuata baada ya ule wa mwaka 1995. Tusishangae iwapo masibu ya Zanzibarya vitambulisho wa ukaazi kuamua nani aruusiwe kujiandikisha kupiga kura au layataamia Tanzania Bara come 2015.

  Wadau wafuatao wanapashwa kuchukua hatua stahiki, ikiwezekana hata kupelekapublic litigation Mahakama Kuu dhidi ya NIDA kukiuka Katiba na Sheria;


  1. Vyama vya Siasa,
  2. Asasi za Kiraia,
  3. Chama cha wanasheria Tanganyika,
  4. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
  5. Vyombo vya habari,

  Pale ambapo makosa yamekwishafanyika, mchakato urudiwe upya. Lakini paleamabapo mchakato bado haujaanza panatakiwa marakebisho kurudiwa haraka.

  Wahenga walisema, Ada yaMja Kunena; tusipoziba ufa tutakuja kujenga ukuta.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wenyeviti mnaanza kulalamika sasa mmekoseshwa mlo.
   
 3. a

  admiral elect Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli kaka usemayo! majuzi alikuja kwangu huyo kada wa ccm, mimi sikuwepo akamkuta dogo na kumuumba amwandikie orodha ya watu wanaoishi kwangu! dogo akumuuliza we ni nani,lete kitambulisho chako kwanza!baada ya kushindwa kutoa kitambulisho cha nida au nido sijui sido vyovyote vile zaidi ya kudai kuwa yeye ni mjumbe wa nyumba kumi(ccm) dogo akamtoa baruti. jamaa akaanza kutoa vitisho kuwa nyumba hiyo haitapewa vitambulisho! dogo akamwambia kwanza hatuvihitaji,mjumbe akapigwa butwaa na kuondoka kwa aibu. chezea dogo ya admiral wewe?dogo ya ya admimiral captain!
   
 4. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe ni mtanzania kweli, au haujaelewa kilichoandikwa hapa?
   
Loading...