Nick Minaj alamba dili la Pepsi

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
pepsi.png


BAADA ya kufanya vizuri kwenye muziki, festledi wa lebo ya Young Money, Nick Minaj sasa ameanza kupanua wigo wa kibiashara baada ya kulamba dili ya kutangaza kinywaji cha Pepsi.

Inasemekana dili hiyo ni ya mamilioni ya pesa na huenda ikamlipa mara dufu kuliko anapotoa albamu moja ya muziki.

Tayari Minaj ameshatengeneza tangazo ambalo limefanyika katika nchi moja ya Amerika ya Kusini na litaanza kuruka baada ya miezi miwili kuanzia sasa.

Minaj anaingia kwenye rekodi ya mastaa wakubwa waliowahi kufanya matangazo ya Pepsi akifuata nyayo za mwanamuziki Michael Jackson.
 
Back
Top Bottom