Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....
Kijana kwanza
angalia nini plan yako kwanza ikimaanisha unataka kozi gani baadae ili
usije kujiroga mwenyewe. Kisha angalia masomo gani unayamudu ili baadae
usije kujutia kwanini uliacha somo fulani. Kisha utaamua mwenyewe nini
ufanye baada ya kuangalia vigezo hivi.
Ajira zenyewe za serikalini
unazodhani utapata ni za *******. Soma kozi unayoipenda na kuiweza. As
long as unaiweza na utafaulu vizuri, ajira au kujiajiri kutakuja baadae.
Mi binafsi ni engineer. Nlichagua njia hii tangu form one. Advance
nilichaguliwa kusoma PCB, nikakomaa kubadilisha kwenda PCM ingawa watu
walinipa porojo kama hizo unazoambiwa kuhusu ajira. Nimeajiriwa na
natengeneza millions (za kitanzania), na nina mpango wa kuachana na
ajira na kuanza kufanya mambo yangu binafsi.
Kijana kwanza angalia nini plan yako kwanza ikimaanisha unataka kozi gani baadae ili usije kujiroga mwenyewe. Kisha angalia masomo gani unayamudu ili baadae usije kujutia kwanini uliacha somo fulani. Kisha utaamua mwenyewe nini ufanye baada ya kuangalia vigezo hivi.
Narudia tena pcb & pcm hizo kombi ukienda shule zaidi ya mzumbe,kibaha,taboraboys &ilboru lazma ufeli
Narudia tena pcb & pcm hizo kombi ukienda shule zaidi ya mzumbe,kibaha,taboraboys &ilboru lazma ufeli
Mentor...Ndiyo maana tuna wasomi lakini hakuna output yoyote kwenye taaluma zao.
What's your dream young man??
Soma hata HKL kama ndiyo itakufikisha kwenye ndoto zako..otherwise utakuwa doctor lakini not self motivated koz ulisoma tu upate ajira kirahisi upate pesa not what u really wanted to do!
Think again why you want to study either of those!!!!
PCB hutajutia,kwanza ukisoma udaktari una uhakika wa gov sponsorship,pili ajira miaka 3 serikalini, PCM utasugua sana mtaani
Apo kweliAre you good in Mathematics or Biology ?
Jibu lipo hapo hayo mengine ni ya ziada