SaveTheOthers
Member
- Jan 29, 2017
- 99
- 230
Heshima kwenu Waungwana.
Mara nyingine binadamu hupitia katika kipindi kigumu haswa. Kipindi ambacho nakifananisha na mtu mwenye mtumbwi asiyejua kuogelea huku hali ya bahari ikiwa yenye kujaa taharuki na mawimbi makali.
Mtu huyu, ama aokolewe na wasamaria au apokelewe na Rabana. Mtu huyu hushukuru sana pasipo kuchoka, endapo utakuwa msamaria mwema utakayeyaokoa maisha yake yasiangamie ndani ya Bahari. Hakika kumbukumbu ya wema wako hautafutika ndani ya Moyo wake.
Naam, naomba uwe Samaria mwema kwangu. Samaria ambaye atayaokoa malengo ya maisha yangu. Yaokoe maisha yangu kwa kunichangia japo kidogo niweze kuendelea na masomo yangu ya Chuo.
Nisikuchoshe sana. Mimi ni mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA), tawi la Dar es Salaam. Nasoma Shahada ya Uhasibu (BAC) Mwaka wa Pili. Hali yangu i tete sana katika kipindi hiki. Ni kipindi ambacho wenzangu wanafurahia kufanya mitihani yao ya Semista ya 1 kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Kwa bahati mbaya sana hali i tofauti kwangu, mimi sijafanikiwa kuanza mitihani hiyo. Sijafanikiwa baada ya kutotimiza taratibu za Chuo.
Taratibu za Chuo zinaelekeza kuwa, "Mwanafunzi atasajiliwa na kuruhusiwa kufanya mtihani wa Semista ya Kwanza endapo atakamilisha asilimia 70 ya malipo ya ada ya mwaka mzima". Yaani semista ya kwanza utalipa 70% alafu semista ya pili 30%. Kwa Mwaka huu, ada ya Mwaka mzima kwa Wanafunzi wa Shahada ya Uhasibu, mwaka wa pili ni Tsh 1,204,000. Kwa maana hiyo itatakiwa ulipe Sh 842,800 kwa semista ya Kwanza na kiasi kitakachobakia kwa Semista ya Pili.
Kutokana na hali duni, sijafanikiwa kutimiza kiasi hicho mpaka sasa. Nimejikusanya na kupata Sh 220,000. Ambapo, nabakiwa na Pungufu ya Sh. 622,800.
Basi nakuomba unichangie japo kidogo niweze kutimiza kiasi hicho ili niruhusiwe kufanya mitihani iliyobakia kwani mpaka sasa ishafanyika mitihani miwili. Na endapo nitashindwa kufanya mitihani iliyobakia basi itanibidi nihairishe mwaka.
Kidogo utakachonichangia hata Sh 1,000 itanisukuma hatua moja kubwa sana mbele. Nauomba unisaidie sana Mkuu.
Ili kuepusha udanganyifu na utapeli, mimi naomba nisikabidhiwe chochote. Badala yake fedha zote zilipwe benki ya NMB. Kwenye akaunti yenye jina TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY, nambari yake ikiwa 2061100017. Au kama itakavyoshauriwa, Uongozi wa JF uhusishwe katika hili, watoe namba na wenye chochote watakachoguswa nacho watume kwenye namba hiyo, kisha wailipie benki na mimi nitakuwa tayari kwenda kuchukua Slip.
Nitakua tayari kupokea pay in slip na kuiwasiisha chuoni ili deni langu liwe cleared na niweze kujisajii na baadae kuruhusiwa kufanya mitihani.
Utakuwa umeyaokoa sana maisha yangu. Siyo kwamba naangamia, la Hasha! Bali umeniokoa sana kutoka kupoteza rasilimali ya muda wa mwaka mmoja mzima bila kufanya chochote na kuniepushia na mambo mengi ambayo huenda yangetokea kwa sababu ya mimi kuwa mtaani bila kazi yeyote. Siku moja nitasimama na kufurahi huku nikijua wewe mwanaJF ni sehemu ya mafanikio yangu.
Najua si mimi pekee niliye na shida na matatizo, ila naomba hili nililete kwako mwanaJF na uweze kuliangalia kadri ambavyo Mungu atakujalia.
Najua yatazuka maswali, nipo tayari kuyatolea ufafanuzi. Ila nakuomba usinivunje moyo na kunifedhehesha kwa sababu ya hitajio langu.
Nimeshahangaika sana kutafuta suluhisho la hitajio langu, lakini sikufanikiwa.
Mungu akubariki.