Nichague chama au mgombea?

Mimi nafikiri unatakiwa "uchague mtu (strong man/women), kwasababu hapa kwetu strong man anaweza kufanya kitu hata kwenye chama kibovu, unlike mtu wa hovyo hata kama chama kizuri kwasababu mtu wa hovyohovyo hawezi ku-argue his/ her case mbele ya chama...though we need both strong man and strong institution tofauti na obama alivyosema africa inahitaji strong institution than strong man, nafikiri tunahitaji both.
 
NImeipoteza haki yangu ya kupiga kura kwenye chaguzi za Rais mbili sasa hivi. Nafuatilia sana siasa lakini si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Tusaidiane katika hili;
Nimchague mgombea ambaye anafaa au nichague chama bila kuzingatia mgombea wa chama hicho anauwezo kiasi gani na amepatikanaje?

KWELI UNAHITAJI ELIMU YA URAIA WEWE. nDIO KWANZA UMEINGIA MIAKA 18 HIVYO IAKUWA MARA YAKO YA KWANZA KU VOTE?
 
Ndugu,
1.Kama umepoteza haki-si uone kwamba haki yako inarejeshwa kabla ya kupiga kura haramu?
2.Upo nchi gani?

Yote hayo nafikiri yanamuangukia mchaguzi, mpiga kura, bila kujali chama au mgombea.

Kwa vile tunaenda na wakati, ni vizuri ukapitia unayotegemea kwenye chama na mgombea.

Kwa sababu zako, haitakuwa rahisi kwangu kukupa usaidizi wewote. Ila kwa sababu ninazozijua mimi; Uwezo wa Chama na Mgombea ni muhimu.
 
Soma vizuri hapo juu, nimeipoteza haki yangu vipindi viwili. Ndio miaka 18 hiyo? Otherwise nisingeipoteza
 
Ndugu,
1.Kama umepoteza haki-si uone kwamba haki yako inarejeshwa kabla ya kupiga kura haramu?
2.Upo nchi gani?

Yote hayo nafikiri yanamuangukia mchaguzi, mpiga kura, bila kujali chama au mgombea.

Kwa vile tunaenda na wakati, ni vizuri ukapitia unayotegemea kwenye chama na mgombea.

Kwa sababu zako, haitakuwa rahisi kwangu kukupa usaidizi wewote. Ila kwa sababu ninazozijua mimi; Uwezo wa Chama na Mgombea ni muhimu.
Nipo Ughaibuni lakini nitakuja kuvote. Kwamujibu wako hapo hatuwezi kutenganisha chama na mgombea?
 
Kwa mujibu wa wa wanaasisi waliopita...ni sheria na miongozo iliyowekwa kwa ajili ya mazoezi hayo ya kupiga kura, ndio ya kufuatwa-vile vile ina ambatana na siasa mbadala na sehemu\nchi husika.

Ni vigumu ketanganisha matakwa ya chama na ya mwanachama! Vivyo hivyo ya chama na mgombea.

Nafikiri kama unazungumzia siasa za kwetu(sheria za uchaguzi na kadhalika...) bado kuna mengi ya kuridhia.
 
Kwahiyo ni kama kufumba macho na pale kalamu itakapodondokea ndiyo nitie tick kwa mgombea huyo. Asante nimeelimika
 
Kamwe sitakushauri vibaya na siku zote inabidi tuwe wawazi, tatizo letu kubwa la watanzania ni unafiki,wengi huwa tunatenda tusiyo yaamini na tunaamini tusiyoweza kuyatenda.
Uchaguzi wowote ule inabidi uangalie mgombea ana uwezo gani na pili unaangalia chama, maana akichaguliwa itabidi aongoze kwa kufuata ilani ya Chama chake na siyo vinginevyo,lakini kama tungekuwa na flexible constitution ambayo mbunge au diwania anaweza kuacha chama chake na bado akaendelea kuwa mbunge, definetely 90% tungetakiwa kuangalia mtu na wala siyo chama, lakini kwa sasa huo ndo ukweli (Chama+Mgombea).
 
Basi jibu ni chama, maana kama utekelezaji ni ilani basi ni lazima nianze kujipinda kupitia ilani moja baadaye ya nyingine then hapo ndiyo nitakuwa salama kwenye kugawa kura yangu
 
Mbona unajikanyaga umetaka ushauri ,tumekushauri kila mmoja na rai yake ,umedai kwenye chaguzi za Rais ,mara wabunge mara Pemba,sasa nakushauri bora uanze na udiwani.

Mheshimiwa nbhai tayari analo jibu bali amekuja hapa either kuona watu wanasemaje au na yeye aonekane tu angalau ameanzisha thread.
 
Mwanzoni kabisa nimesema wazi sijawahi kushiriki uchaguzi wowote. Nilidhani jamvi lingenipa uzoefu. Nilikuwa nina maswali ambayo hayakuwa na majibu? Waliowahi kuwachagua wagombea na kuacha vyama( wapinzania) wamenufaika nini? Na waliochagua chama bila kuzingatia wagombea wamenufaika nini? Preferences zetu zinajengwa na chama au wagombea, wagombea na chama, au ilani za chama.
Tunataka nini hasa katika uchaguzi ujao? Mtu au Chama?
Katika nchi yetu kuna maeneo ya maendeleo kuzidi mengine, hao walichagua chama au wagombea? Uzoefu pls
 
Mheshimiwa nbhai tayari analo jibu bali amekuja hapa either kuona watu wanasemaje au na yeye aonekane tu angalau ameanzisha thread.

Mkuu,
Hizo hisia zako weka pembeni. Maelezo ya bnhai yako wazi kabisa na yanajieleza vizuri. Mpe nafasi ya yeye kujifunza kile anachoamini anahitaji kukifahamu.
Uchaguzi wa Biharamulo umeonesha wazi kuwa kuna haja ya kutoa elimu ya kutosha kwa wapiga kura kwani imekadiriwa kuwa about 60% ya waliojiandikisha hawakupiga kura, kwa maana nyingine kama hao 60% wangekuwa wanapigia TLP ni wazi kuwa si CCM wala Chadema wangeona ndani.
Tusipandikize mawazo yetu kuwa ndiyo mawazo ya mleta mada...tujadili kwa upeo mkubwa ili sote tufaidike.
 
Back
Top Bottom