Nichague chama au mgombea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nichague chama au mgombea?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bnhai, Jul 12, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  NImeipoteza haki yangu ya kupiga kura kwenye chaguzi za Rais mbili sasa hivi. Nafuatilia sana siasa lakini si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Tusaidiane katika hili;
  Nimchague mgombea ambaye anafaa au nichague chama bila kuzingatia mgombea wa chama hicho anauwezo kiasi gani na amepatikanaje?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama bado hujajenga,unatafuta shamba ,kiwanja au leseni ,au una mipango yako ambayo inakubidi upitie kwenye mawizara ya serikali na taasisi zake na unahitajia fedhaa nyingi sana basi ichague CCM unaweza kufanikisha yote hayo japo kwa robo ya gharama au ukafanyiwa mambu yako hata bila ya wewe kuinua mguu na kuletewa hapo hapo nyumbani na aliekufanyia ukampa takirima na akaridhika kabisa tena ukishafanikisha kura yako usiipeleke tena kwa CCM.
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwenye ubunge na udiwani ---- absolutely angalia mgombea.

  Kwenye uraisi angalia mgombea+chama.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 4. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haijalishi utachagua nini - tume ya uchaguzi ndiyo ina mamlaka ya kuamua mshindi kwenye chaguzi za Tanzania.
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Zipo kona ambazo hata tume ya Uchaguzi haipenyi. Kama Karatu na Pemba huko hakuna ujanja. Ukweli naamini zaidi katika mgombea kuliko chama. Mf kina mama Kilango na wengine kutoka watawala na wapo wapinzani wamesinzia pia. Naomba hoja zenu wana JF ili hii mizania hapo mwakani twende sawa
   
 6. b

  bnhai JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo tuamini kwamba Watanzania wote tunaweza kujenga kwa kuchagua CCM? Mbona wengi hawana makazi basi? Naomba nieleweke kura yangu anapewa yule mwenye nia ya kuikomboa nchi na si maslahi yangu binafsi. Naamini nikiinufasha nafsi yangu siepuki matatizo yanayonizinguka mf miundombinu nk
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mbona unajikanyaga umetaka ushauri ,tumekushauri kila mmoja na rai yake ,umedai kwenye chaguzi za Rais ,mara wabunge mara Pemba,sasa nakushauri bora uanze na udiwani.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Bila ya shaka yeyote inategemea mbinu zako tu,Tanzania imeshakombolewa zamani sasa tunakula matunda ya uhuru :D
   
 9. b

  bnhai JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Inawezekana sikujieleza vya kutosha. Kwenye chaguzi naongelea ngazi zote. Mwanzoni nilisema chaguzi za rais ili kuonyesha time frame lakini si specific kwenye kura za rais. Nashukuru kwa rai yako, lakini lengo hasa si kujenga na kupita wizarani lakini kumpa yule au chama( kutegemea na maoni ya hoja) chenye(mwenye) malengo ya kuwanasua watanzania katika lindi la umasikini
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Basi itabaki palepale CCM maana malengo yao ni mazuri sana ..Maisha bora kwa kila Mtanzania...hiyo haijakutosha tu kuichagua.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Swali zuri sana. Maana ukimchagua mgombea mzuri na chama chake ni kibovu basi ni tatizo. Na ukichagua chama bora lakini mgombea akawa hovyo basi napo ni tatizo. Mkuu swali lako lita tegemea na wewe mwenyewe mpiga kura unataka nini.
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Honestly ningependa kuona jamii inajikwamua katika umasikini na uwajibikaji wa viongozi, yote haya yakithibitishwa na uhalisia si takwimu au reviews za literatures. Labda hili swali linaweza kujibiwa na wale waliotoka mikoa ambayo kitakwimu anaonekana bora kuliko mingine, walichagua chama au mgombea? Labda we can generalise that to the national level.
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa ishu si maneno "slogans" nzuri, ishu ni uhalisia.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba you can not separate one from the other. Mgombea ana hitaji chama na chama kina mhitaki mgombea. This means that mgombea ni lazima afanye kazi kutokana na ilani na kanuni za chama. Kwa hiyo ukichagua chama automatically umemchagua mgombea na ukimchagua mgombea automatically umekichagua chama. Ni tofauti na mfumo wa Marekani ambapo chama huo hakina kazi maalumu baada ya uchaguzi. Chama inakua kazi yake ni kuingiza wagombea wake madarakani tu lakini vyama vyetu go beyond that.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..kwa Zanzibar chagua CCM.

  ..kwa Raisi wa Tanganyika/Muungano usichague CCM.

  ..kwa wabunge wa Tanganyika angalia sifa mgombea usiangalie chama.
   
 16. b

  bnhai JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani unawafaham wagombea wa uchaguzi ujao au hiyo ni fixed variables throughout all elections. Kwamba bara isiwe CCM na ZNZ iwe CCM?
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  bnhai,

  ..CCM inajulikana kwamba watamsimamisha JK. sasa huyu namjua kwamba he is not serious.

  ..Zenj, nadhani CCM ni afadhali kuliko CUF.

  NB:

  ..baraza la wawakilishi Zenj inafaa liwe na majority CCM.
   
 18. b

  bnhai JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Ok kwa bara JK umemlinganisha na nani JokaKuu? Maana siwafaham wagombea wengine? Na Znz kama unaweza nidokeze though ninavote bara.
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Bnhai,
  Mara nyingi kura watu hupigia chama au mtu kutokana na utashi binafsi wa mpiga kura. Lakini kwa vile umetaka ushauri basi nitakupatia kwa kadri nitakavyoona inafaa.
  Tunapopiga kura kawaida sisi wananchi tunatoa ridhaa kwa wanaoomba uongozi washike hatamu za kuongoza nchi kwa maana ya bunge na serikali. Hii ridhaa ambayo tunayowapa inabidi pia kuangalia uwezo HALISI wa kuendesha vyombo hivo hasa serikali au uwezo wa kuwakilisha wananchi hasa inapofikia kwa wabunge na madiwani.
  Mimi bila ya kujali mambo mengi kwa maana ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, ninajali uwezo wa CHAMA kwa kuangalia rekodi yake ya utendaji, rekodi ya uwajibikaji hasa katika kutatua matatizo kwa viongozi wake, oganaizesheni ya chama chenyewe na mwisho katika upande wa chama ninaangalia mtandao wa chama husika. Vitu nilivyovitaja ndiyo vitu ambavyo hujenga uimara wa chama cha siasa.
  Baada ya kuchagua chama ambacho nadhani kinafaa kupewa ridhaa na wananchi ya kuongoza kura yangu ya rais inakwenda hapo then ninaangalia case by case, je mgombea katika nafasi ya ubunge anafaa? je mgombea katika nafasi ya udiwani anafaa?
  Huo ndiyo mtazamo na ushauri wangu.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  bnhai,
  Maoni yangu chagua MTU. nadhani tukianza hapo tunaweza fika kwenye demokrasia ya kweli haraka zaidi ya kuchagua CHAMA..
  Sababu kubwa inayonisukuma kukupa oni hili ni kwa sababu Vyama vyetu havina tofauti zaidi ya watu wanaotawala..Binafsi simani kabisa msemo wa kwamba chama kinaweza kuwa imara wakati viongozi wake ni duni..Ila yawezekana kabisa viongozi wazuri kuwa ktk chama kibovu..kwani ubovu wa chama kwa mtazamo wa watu mara nyingi hutokana na chama kutoweza kushinda uchaguzi..

  Kama unakumbuka Nyota ya Morogoro ilikuwa team mbovu sana, lakini siku wachezaji wa Yanga walipojiunga na team hiyo tuliyaona matunda ya team ile mbovu..Tofauti na Siasa viongozi wazuri wote hukosa nafasi ya kushiriki kwa mpango wa vyama kuwaengua wagombea kabla hawafika hatua ya kuchaguliwa na wananchi. Na ubovu unazidi pale viongozi hawa wazuri wanaposhindwa kuondoka ktk chama ambacho kimewafunga kamba wasipate kuonyesha uwezo wao badala yake wamebakia ktk chama wakilalama pembeni kuchelea macho na maneno ya NDIVYO TULIVYO, kwamba ukiondoka chama chochote kile ni Unafiki na mchovu kisiasa.

  La msingi nalotakla kuwaomba vijana wenye moyo na uwezo mkubwa wa kuongoza waingie vyama ambavyo vitawapa nafasi ya kushindana ili sisi wananchi tupate nafasi ya kupiga kura zetu lakini huwezi kusimama chama kimoja ambacho unaelewa fika utaenguliwa ktk teuzi za chama..
   
Loading...