Nianzaje kumkumbushia deni langu huyu dada!

kuna vitu usipoweza kujisimamia ndo unaenda mpaka ktk maisha yako! Kwanza ulipaswa uwe umeshamdai kujua kulikoni kimya kosa la kwanza. . Mana mi mwenyewe sidai ovyo lakini muda mrefu ukipita lazima nijiulize na kuuliza! Pili kosa lingine ni ilo la kujiuliza kumpa i mean how? Why? Jamani sipendi kabisa mtu ambae hana uaminifu na kusimamia ahadi! Yani ya mwanzo haina maelezo then unaomba nyingine? Sikupi ili ujifunze nidhamu nyie mnaosema ampe kiasi tabia zingine zinaongeza uharibifu kwa tabia za watu uyo anahitaji a lesson. . Kama alikosa alipaswa awe anatoa updates then hapo ningeweza kumsaidia kwa uangalifu sasa!
 
Imetokea ya aina yake huko kanda ya ziwa. Dada mmoja kaomba lifti kwa mkaka mmoja mtanashati mwenye prado kwamba anaomba lift kwenda mjini. Huyo mkaka alipofika mahali anapokwenda dukani kwake, akamwambia yule mdada anaishia hapo hivyo ashuke. Yule mdada akang'aka kwamba kwani hapo ndiyo kwenye ATM? Akamwambie mbon sikuelewi? bo kwani kazi yote niliyofanya usiku kucha tukakubaliana laki na nusu unajifanya kusahau ati. Ukawa mzozo. Mjini hakuna dogo watu wakazonga kutakujua kuna nini? Ndipo wenye busara wakambie aampe hata kidogo ili asepe vinginevyo atazidi kujiabisha tu. Jamaa akatoa laki kwa shingo upande demu akasepa.
 
Pole mkuu. Mimi pia nina story kama hii ya kwako, japo ya kwako ni cha mtoto ukilinganisha na ya kwangu. Kuna dada mmoja tunayefahamiana japo si karibu sana alikuwa na shida akaniomba nimkopeshe pesa. Nikamkopesha na nikaahidiwa ningerudishiwa mwezi unaofuata. Mwezi ukaisha nikaanza kupewa series ya matatizo aliyonayo (nahisi ilikuwa ni namna ya kuniambia nisimdai tena), mara ana harusi ya ndugu yake mara ana mgonjwa mara hiki mara kile na sikumwambia chochote. Ikapita kama miezi 2 hivi akaja na shida nyingine ya dharura akaomba nimkopeshe tena na nikaahidiwa ningerushiwa baada ya miezi miwili mpaka sasa sijarudishiwa. Kwa jumla namdai zaidi ya Tshs. 2.6 mil. Dada mwenyewe ana kazi nzuri sana yenye mshahara usipoungua Tshs. 1.9 mil. kwa mwezi. Nimemkumbushia mara kadhaa jibu ninalopewa nivumilie kidogo. Lol! Sasa najiuliza huyu dada yangu anafikiri mimi sijihitaji hizo pesa jamani? Na mimi niliahirisha mipango yangu baada ya kuhakikishiwa ningezipata tu bila shida. Kwa kweli amenipa somo, na nahisi ana ajenda ya siri sasa.

pole sana mazingira.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom