Niambie kituko kimoja ushawahi kutana nacho kwenye filamu za bongo, mimi nilikutana na hiki...

Ila movie ya Chausiku walijitahidi jamani, story ilikua tamu na waigizaji walivaa uhusika wa maana,

pia movie ya Kigodoro ilikua poa sana story ilieleweka sema mwishoni kuna sehemu waliharibu ila si mbaya,

Movie ya Mdundiko(ilipata tuzo kubwa tu ya kimataifa ajabu haikutangazwa kiviile sijui kwa kua hakua Ray wala JB) pia ana nyingine yaitwa Kisate.

Movie zingine zenye story nzuri ni za huyu Nice a.k.a Mr. Mtunis, kwa kweli jamaa anajitahidi sana hata makosa ni madogo madogo, movies zake ni kama BARMAID, MREMBO KIKOJOZI, MY DREAM (Riyama alifunika sana humu), TOMBOY(Wolper nae alitisha sana alijua kuvaa uhusika).
Ukiona wamevaa uhusika, mfano tomboy, ni tabia zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom