Ni yapi matumizi bora ya maji majumbani?

Itabidi upunguze matumizi ya maji...kufua iwe ni baadhi ya siku na sio kila siku...kufua fua kuna maliza maji sana.
 
Kwanza inabidi tueleweshana hapa

Unapoambiwa umetumia unit moja maana yake nini? Hii ni sawa na ujazo wa lita 1,000.

Kisha tufahamishane hapa unit moja ya maji tunachajiwa kiasi gani?

Jee hizi bei zipo uniform nchi nzima.. kama vile jamaa zetu wa Tanesco?

Bil inapokuja tofauti,hii mara nyingi mteja huwa anaonewa maana mechanism za kuikataa huwa na changamoto.

Hapa tunahitaji assesors wawepo katika ku resolve hizi changamoto.

Kuitembelea nyumba na kuona namna ya maisha yao,lazima itakupa mwanga. Haiwezekani mwezi huu 25,000 gafla mwezi unaofata 63,000 tena inarudi 22,000.

Hizi taasisi za maji zinawajibu pia kuona maji yanatumika kwa usahihi,sio tu kukusanya mapato. Wawe wanawashauri pia wateja namna bora ya kuhifadhi na kutumia maji. Pale panapotekea utofauti wa matumizi kwenda mara 2 zaidi wawatembelee wateja wao na kupata maelezo.

Maji ni uhai. Tulinde vyanzo vya maji.

Sent using iphone pro max
 
Juzi wananitumia meseji nimetumia unit 13 (yaani kutoka 205 mpaka 218) . Kwenda kuhakiki kwenye mita ni 214. Yaani wamenipiga zaidi ya unit 4. Hawa wasoma mita ni vilaza wasiokuwa na weledi au ni strategy ya kampuni kuwapiga wateja kukuza mapato ya shirika.
 
Unadhani kunafuliwa kila siku basi Mkuu Labda kama wafuaji wakifua nisipokuwepo ndio wana matumizi mabaya ya maji yanayofanya bili inakuwa kubwa.
 
Cheki bomba kutoka kwenye mita mpk kwako labda limepasuka linaongeza bili
Sijaelewa hapa Mkuu kwamba linakuwa linachuruzisha maji huku mengine yanaingia ndani?

Mana kuna siku maji hayakufika ndani kwa siku kadhaa kuja kuangalia kuna sehemu maji yanamwagika na mpira umepasuka au ikiwa hivi pia bili nayo inasoma?
 
Kwanza inabidi tueleweshana hapa

Unapoambiwa umetumia unit moja maana yake nini? Hii ni sawa na ujazo wa lita 1,000.

Kisha tufahamishane hapa unit moja ya maji tunachajiwa kiasi gani?

Jee hizi bei zipo uniform nchi nzima.. kama vile jamaa zetu wa Tanesco?

Bil inapokuja tofauti,hii mara nyingi mteja huwa anaonewa maana mechanism za kuikataa huwa na changamoto.

Hapa tunahitaji assesors wawepo katika ku resolve hizi changamoto.

Kuitembelea nyumba na kuona namna ya maisha yao,lazima itakupa mwanga. Haiwezekani mwezi huu 25,000 gafla mwezi unaofata 63,000 tena inarudi 22,000.

Hizi taasisi za maji zinawajibu pia kuona maji yanatumika kwa usahihi,sio tu kukusanya mapato. Wawe wanawashauri pia wateja namna bora ya kuhifadhi na kutumia maji. Pale panapotekea utofauti wa matumizi kwenda mara 2 zaidi wawatembelee wateja wao na kupata maelezo.

Maji ni uhai. Tulinde vyanzo vya maji.

Sent using iphone pro max
Huku kwetu kuna baadhi wanachaji 2000 na wengine 2500 kwa unit moja.

Nilishawahi jiuliza pia hii bei wanakuwa wanaitowa wapi je ni elekezi kutoka Serikalini au ni ile mtu akijisikia tu anaamua aweke kiasi fulani?

Sababu maji ya Dawasco huwa nasikia haizidi 1000 kwa unit moja.
 
Juzi wananitumia meseji nimetumia unit 13 (yaani kutoka 205 mpaka 218) . Kwenda kuhakiki kwenye mita ni 214. Yaani wamenipiga zaidi ya unit 4. Hawa wasoma mita ni vilaza wasiokuwa na weledi au ni strategy ya kampuni kuwapiga wateja kukuza mapato ya shirika.
Ukachukua hatua gani Mkuu au ndio ikabidi kuwafuata Ofisini?
 
Je ukifunga bomba huwa kuna matone yanamwagika?, ni heri ufungulie maji yamwagike kuliko yale matone...kule wanahesabu.
Labda hivi mana unaeza amka asubuhi ukakuta bomba la nje chini pamelowa maji ambayo si yale yakufunguliwa yakamwagika na ukienda kuangalia unakuta bomba linamwaga matone matone ambayo yamedondoka kwa usiku mzima.
 
Tafuta fundi alikaze, bill itapungua.
 
Kwanza inabidi tueleweshana hapa

Unapoambiwa umetumia unit moja maana yake nini? Hii ni sawa na ujazo wa lita 1,000.

Kisha tufahamishane hapa unit moja ya maji tunachajiwa kiasi gani?

Jee hizi bei zipo uniform nchi nzima.. kama vile jamaa zetu wa Tanesco?

Bil inapokuja tofauti,hii mara nyingi mteja huwa anaonewa maana mechanism za kuikataa huwa na changamoto.

Hapa tunahitaji assesors wawepo katika ku resolve hizi changamoto.

Kuitembelea nyumba na kuona namna ya maisha yao,lazima itakupa mwanga. Haiwezekani mwezi huu 25,000 gafla mwezi unaofata 63,000 tena inarudi 22,000.

Hizi taasisi za maji zinawajibu pia kuona maji yanatumika kwa usahihi,sio tu kukusanya mapato. Wawe wanawashauri pia wateja namna bora ya kuhifadhi na kutumia maji. Pale panapotekea utofauti wa matumizi kwenda mara 2 zaidi wawatembelee wateja wao na kupata maelezo.

Maji ni uhai. Tulinde vyanzo vya maji.

Sent using iphone pro max

Tanesco Bil zao sio uniform Nachi nzima, kuna baadhi ya mikoa shilingi elfu moja unapata unit 8, lakini Kwa kiasi hichohicho kuna baadhi ya mikoa unapata unit 2.8
 
Habarini wakuu. Natumai tunaendelea vyema katika mapambano ya kujikinga na hili janga la Corona.

Ni yapi matumizi bora ya maji ya nyumbani kwa upande wako na je bili unayoitarajia kwa mwezi ndo inayokuja?

Ikitokea labda kwa mwezi gharama zimekuja juu mfano umejiwekea labda kwa ukubwa wa familia uliyonayo kwa mwezi ni units 10, 15 au zaidi halafu ikaja bili nje ya ile uliyojiwekea ni kipi unafanya kudhibiti hayo matumizi kwa mwezi ujao ili yabaki yale ambayo ndio umejiwekea?

Kwa uzoefu wangu ni kwamba ( kama bomba halivuji) matumizi ya maji yanakuwa makubwa kama kuna ufumauji wa mara kwa mara usiozingatia matumizi sahihi, kwa mfano mtu anafua nguo moja "size ya vest" anasuuza na maji lita 10 au zaidi.
Pia matumizi ya maji moja kwa moja kutoka kwenye bomba au tank kuingia ndani ( bafuni, chooni na jikoni), usipokuwa na watumiaji wazuri bili lazima itakuwa kubwa kwa mfano mtoto kanywa uji kikombe kitaoshwa kwenye bomba la ndani labda zaidi ya sekunde 30 likiwa limeachwa wazi bila kufungwa wakati wa kusugua na sabuni, na mengine kama hayo maji yajiwa ndani yanatia mshawasha wa kuyafungua hata kama yalihitajika kutumika kidogo sana.
Wachotamaji hasa hawa dada zetu wa kazi anaweza kukinga ndoo bombani akaenda kufanya shughuli nyingine, huku maji yatajaa ma kutiririka zaidi ya dakika zaidi na hii inaweza kuwa mara kwa mara.

Jaribu kutafuta uhalisia wa matumizi halisi ya familia yako,kama extreme zinatokea sana, jaribu haya hapa;
1. Kuwa na tank/ ma-tank la kuhifadhia maji ambayo ukijaza mara moja unaweza tumia kwa wiki mbili au zaidi kulingana na familia au matumizi yako bila kufungua tena kwenye bomba ndani ya hizo siku.
2. Weka utaratibu mzuri wa kufua nguo sio kila siku watu wanafua mara leo nguo 3, kesho 4, keshokuwa 6 nk.
3. Waelimishe nyumbani watumiaji umuhimu wa kutumia maji kwa usahihi na madhara yanayoweza kujitokeza wanapotumia maji vibaya (kusababisha bili kubwa).
4. Wasiposikia funga bomba na kufuli mpaka hapo muda ulioweka wa kujaza tena maji kwenye tank utakapofika ndo ufungue tena.

Tena kama unaenda kazini ni muhimu kuzingatia hayo.

Wengine wataongezea.
 
Tanesco Bil zao sio uniform Nachi nzima, kuna baadhi ya mikoa shilingi elfu moja unapata unit 8, lakini Kwa kiasi hichohicho kuna baadhi ya mikoa unapata unit 2.8
Aisee..

Hii ni tofauti na ngazi ya utumiaji uliyopo?

Kumbe kuna mikoa inapewa unit bei nafuu kuliko mingine.

Tanesco ama mliopo huko tupeni hii ikiwezekana tujue hiyo mikoa na vigezo vinavyotumika.

Inaweza kutusaidia sisi wawekezaji wa viwanda.

Sent using iphone pro max
 
Back
Top Bottom