Ni watu wachache sana wanabahatika kuoa 'Soul Mates'

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Kuna watu nature yao wanapenda usafi, akiamka asubuhi atasafisha alipo lala, bafuni atakuweka sawa baada ya kutumia, jikoni ataweka kila kitu sawa baada ya kutengeneza kifungua kunywa. A tafuta vumbi TV kabla ya kukaa na kuangalia taarifa ya habari.

Mtu wa pili atakua na budget nzuri ya pesa. Ukimpa laki tano ya matumizi inaweza kumaliza miezi mitatu hajaomba hela na ukirudi kutoka kazini chakula utakikuta. Utagundua pesa imekwisha pale utakaporudi na kukuta dinner ya wali mchicha na ukimuuliza sana atakuambia ni mchele tunaomalizia na mchicha nimechuma hapo nyuma.

Hawa watu hata wakiwa na mabishano ya kawaida ya kibinadamu hawezi mmoja kulalamika kuwa mimi huwa ninasafisha bafu kila siku wewe hisafishi kwakua kusafisha bafu hajitumi. Au huyu wa pili hawezi kusema nimekuvumila tunakula wali na mchicha, kuweka hela ni jadi yake

Kuna wanaooa uzuri, msichana mrembo au mwanaume mwenye sura ya kuvutia siku ya kwanza tu ulimuona mapigo ya moyo yalikwenda mbio. Huyu hata akikuudhi ukishaona sura yake unatabasamu. Unawahi kufika nyumbani ili tu umuone.

Hii ni mifano tu, lakini usiombe uolewe au uoe asiyeelewa jitihada zako, kila unachofanya haridhiki. Huyo si soul mate.
 
I can feel you...... tabia nyingi hujificha kabla ya kuishi na a mtu, Kwa hiyo kujua ni ngumu sana!

Mfano mie kuwekewa chakula, maji ya kuoga, na huduma za ki mme mme hata mke asipofanya sina shida,

Ila asipofanya usafi wa Nyumba, I mean I need a neaty House, nateseka mno, naweza hata Piga deki na kuosha vyombo mwenyewe!
 
I can feel you...... tabia nyingi hujificha kabla ya kuishi na a mtu, Kwa hiyo kujua ni ngumu sana!

Mfano mie kuwekewa chakula, maji ya kuoga, na huduma za ki mme mme hata mke asipofanya sina shida, ila asipofanya usafi wa Nyumba, I mean I need a neaty House, nateseka mno, naweza hata Piga deki na kuosha vyombo mwenyewe!
Mfahamishe hayo aelewe, kuna vitu vidogo vinafanya watu wasirudi nyumbani waishie baa kumbe mnaweza kuviweka vizuri.
 
Na kweli kabisaa kuna Watu kutwa kucha ni kuona ubaya wako tu hakuna jema hata moja tofauti ya mwaka juzi inakumbushiwa kila uchwao mkibishana. Yaan mpaka unajiuliza hivi huyu Mtu ni Timamu kweli?
Hapo basi kuna ambae hajaridhika na hali ya mwenzake. Lakini ajabu ni kuwa ukisafiri anauona umuhimu wako na kukuomba urudi haraka.
 
Mfahamishe hayo aelewe, kuna vitu vidogo vinafanya watu wasirudi nyumbani waishie baa kumbe mnaweza kuviweka vizuri.

Ndugu yangu tabia kubadilika ni ngumu, she cant aisee, nimefanya mpaka kwa vitendo, But still Hakuna, utakuta tu vitu havipo sawa!

Sasa akatokea Dada wakazi is wired like me! Msafi mno, sasa huyo ndo kwa kweli ananifanya Nina raha!

Yani yeye hata nikimwambia fua hizi nasafiri, hemu fanya faster rekebisha hiki anafanya! Mwishowe keshanijulia na wala simwelekezi tena!

Now, the issue is akiondoka Sasa sijui, maana naona wifi yako kaanza figisu figisu, ila najitahidi kumkingia kifua!

Yani kwa kifupi huyu Dada wa kazi ni shockabsobder ya udhaifu wa huyu Mama, anasawazisha!
 
Mkiwa kwenye pillow talk mwambie wifi ajiongeze ongeze. Jana nilimtembelea rafiki yangu ambae nilimsaidia uzazi alipojifungia binti yake ambae sasa ana miaka saba. Nilipofika binti alinionyesha chumba anacholala yule binti ni msafi. Mama yake aliniambia alianza kumfundisha tangu akiwa na miaka mitatu. Viatu vinakaa kwenye shelf ya viatu, kalamu kwenye pen holder nk.

tufundishe watoto usafi mapema.
 
Ndugu yangu tabia kubadilika ni ngumu, she cant aisee, nimefanya mpaka kwa vitendo, But still Hakuna, utakuta tu vitu havipo sawa!

Sasa akatokea Dada wakazi is wired like me! Msafi mno, sasa huyo ndo kwa kweli ananifanya Nina raha!

Yani yeye hata nikimwambia fua hizi nasafiri, hemu fanya faster rekebisha hiki anafanya! Mwishowe keshanijulia na wala simwelekezi tena!

Now, the issue is akiondoka Sasa sijui, maana naona wifi yako kaanza figisu figisu, ila najitahidi kumkingia kifua!

Yani kwa kifupi huyu Dada wa kazi ni shockabsobder ya udhaifu wa huyu Mama, anasawazisha!
Fanya uwezavyo dada asiondoke, ili aendelee kuwa sapota mzee
 
Mkiwa kwenye pillow talk mwambie wifi ajiongeze ongeze. Jana nilimtembelea rafiki yangu ambae nilimsaidia uzazi alipojifungia binti yake ambae sasa ana miaka saba. Nilipofika binti alinionyesha chumba anacholala yule binti wa miaka saba ni msafi. Mama yake aliniambia alianza kumfundisha tangu akiwa na miaka mitatu. Viatu vinakaa kwenye shelf ya viatu, kalamu kwenye pen holder nk.

tufundishe watoto usafi mapema.

Huu ni msingi mzuri sana kwa Mtoto wa Kike!
 
Kuna wanaooa uzuri, msichana mrembo au mwanaume mwenye sura ya kuvutia siku ya kwanza tu ulimuona mapigo ya moyo yalikwenda mbio. Huyu hata akikuudhi ukishaona sura yake unatabasamu. Unawahi kufika nyumbani ili tu umuone.
Hapa nakubaliana na wewe 100% tokea nimemuona mwenza wangu mpaka hii leo nimewacha kila kitu nafocus na kutafuta hela tu na kila tukionana kumbatio mwanzo mwisho na kisses za hapa na pale. Yaani kumpata soulmate raha kama Zuchu na wimbo wake wa raha.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom