Ni wapi wataalamu wa kitanzania tulipofikia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni wapi wataalamu wa kitanzania tulipofikia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nyalotsi, Sep 18, 2012.

 1. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Wakati serikali zingine zikiwakusanya na kuwasikiliza wasomi walio kwenye field,serikali yetu inafanya juhudi zote kuhakikisha wanagawanyika na kutokuwa na msimamo wa pamoja kwa ajili ya yale yahusuyo utaalamu wao. Ukianza na wanasheria, wamekuwa wakiteuliwa majaji wasio na vigezo ili wenye vigezo wawaseme waanze kuchukiana. Siwezi kurudia ripoti ya lisu. Sasa hivi hawawezi kusimama na kutetea utaalamu wao kwa msimamo mmoja. Wanahabari nao wamegawanywa kwa mfumo wa wanaowatumikia mabwana na walio huru. Kuna wengine maisha yao hayawezi kwenda bila rushwa ya viongozi wa serikali. Nafikiri kila mtu anajua kinachoendelea kwa hawa ndugu zetu. Sasa hivi mpasuko mkubwa uko kwa madaktari. Ulianza pale specialists waliposhindwa kusimama na kuwatetea interns waliofukuzwa. Ulikuwa ni usaliti mkubwa sana ambao umesababisha na yanayotokea wakati huu. Lakini kosa la mwanzo lisiwe sababu ya grave mistake iliyotekea wakati huu. This is an insult to the profession. Kuomba msamaha sio kosa, kosa ni yale waliyoelekezwa wakaongee kwenye vyombo vya habari. Hivi ndo wamejua leo kwamba wameua watu wakati wa mgomo? Wanataka kutuambia walidanganya kwamba wagonjwa wanalala chini? Hospitali vifaa hakuna? Dawa hakuna? Ina maana wao hawana akili mpaka watuambie mat iliwalazimisha? Si kuna waliogoma kugoma, kwa nini nao wasingekataa? Wanataka kutuambia wao wameijua sana MAT mpaka kuwashauri watu wajipime wanavyojiunga nayo? Ok, wametukana mat na viongozi wao, wametubu na kukiri kwamba waliua wakati wa mgomo, tukiwashtaki kwa kusababisha vifo watasema tumewaonea? Ushaidi si upo! This is now Specialist vs juniors, waliogoma vs waliogoma kugoma, walioomba msamaha vs wasioomba msamaha. Walioitukana mat vs wanaoipenda. Hii ndo furaha ya wanasiasa, kuhakikisha nyie mnawatumikia wao na sio wao kuwatumikia wananchi. Visasi vitakavyotokea kwenye hii fani ni wagonjwa watakaoumia. Mungu tuepushe na hizi laana
   
Loading...