Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni jambo la kumshukuru Mungu kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendelea vema na majukumu yake tena kwa kasi ambayo wapinzani hawakuitarajia. Wakati Wao walikuwa wananadi mabadiliko ya kuzungusha mikono, Magufuli alikuwa ananadi mabadiliko ya kweli ambayo kwa sasa tunayashuhudia.
Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa Rais Magufuli analeta mabadiliko ya kweli wakati waliokuwa wananadi mabadiliko ya kuzungusha mikono wanashuhudia. Huu ni wakati muafaka kwao kujitathmini kama walikuwa na dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo Watanzania ama ulikuwa ni ulaghai wa kisiasa.
Siku za mwanzo za utawala wa Rais Magufuli, Lowasa na genge lake walitoa kauli kadhaa za kejeli. Kwanza walidai kuwa jitihada za kulipa kodi anazofanya Rais Magufuli zinalenga kuwaonea na kuwakandamiza wafanyabiashara waliounga mkono upinzani. Baadaye wakajiona wajinga kumbe waliyotamka hayana uhalisia wowote. Then wakatoa kauli kuwa Rais Magufuli anafukuza hovyo watendaji wa serikali kwa sababu hakuwateua yeye. Aibu. Kwa kadri majipu yanavyotumbuliwa, wamejikuta wakiwa mabubu wasijue nini cha kusema.
Hata yule Kikongwe aliyesema kuwa CCM imeishiwa pumzi kwa sasa hasikiki kabisa. Naona yeye kwa sasa pumzi zimekata ama amebaini kuwa Magufuli ndiye aliyekuwa mgombea sahihi wa Watanzania. Kule kwa Lowasa alifuata ulaji tu.
Wasomi na watu kadhaa wametoa maoni yao juu ya siku 100 za Rais Magufuli Madarakani. Wengi wamepongeza na wameunga mkono jitihada anazochukua Rais za kurekebisha Serikali. Wale wa mabadiliko ya kuzungusha mikono hakuna hata mmoja aliyediriki kupanua mdomo wake ama kunyoosha vidole vyake kucmment. Wengi wamegeuka kuwa bubu wasijue nini cha kusema. Maana wakiunga mkono roho zinawauma na wakikosoa hawaoni wapi pa kukosoa. Mambo yanaenda kwenye mstari. Watakuja kushtuka 2020 hiyo imewadia.
Jumamosi njema. Kwa wale mlioko Dar na mikoa ya jirani, tafadhali jitokezeni kwa wingi kushuhudia mpambano wa karne baina ya Yanga na Simba. Ubashiri wangu ni kuwa mechi itakuwa sare. Sisi tuliopo mbali tutautazama mtanange huo kupitia Azam TV