MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Yaani nimepita maeneo mengi nchi hasa vyuoni, Wanafunzi wa vyuo vikuu waliodahiliwa kwa vigezo vya stashahada mwaka jana wote hawana mikopo! Vijana hawa wanalia, ni taabu tupu! Serikali haitaki kabisa kuwasikia wala kuwasaidia.
Hakuna mnyonge anayefaidika na Serikali hii, wanyonge wanalia vilio vya huruma kama vile ni wakimbizi,hawana amani kabisa ndani ya taifa lao.
100% ya viongozi wote wa Serikali walioko madarakani walisoma kwa gharama za Serikali tena bure, Viongozi wote wakuu wa nchi yetu wamesomea degree zao za kwanza wakitokea stashahada kama walimu na wamesoma kwa msaada wa pesa za serikali! Kwanini vijana hawa wateseke kiasi hichi? Wana tofauti gani na waliosoma enzi hizo? Huu ni ubaguzi mbaya sana kutokea nchini.
Kama mimi nina vijana wangu naweza kujikaza nikawasomesha kwa kubangaiza, lakinije yule mkulima wa kijijini aliyejikasa walao kijana wake akapata stashahada ya ualimu atamsogezaje kupata walau kupata shahada kuongeza kaujuzi chake?
Tunawaonea sana wanyonge, tupite vyuoni tune vijana wanavyotaabika ndani ya taifa lao.