Kama shida siyo pesa. Weka ndani kama kumbukumbu. Itakusaidia sana maana hiyo Laptop mbovu wakikupa pesa basi haifiki 70,000. Hii pesa utaifanyia nini?
Kioo, Ram na hard disk unaweza kutumia kwa matumizi yako binafsi. Chukua Hard disk, nunulia kasha na cable yake, tumia kuhifadhia doc zako. Hard disk ya 320Gb ni kama 30k inategemea na maeneo. 500GB ni 60k inategemea maeneo.