Ni wakati wa Benki Kuu (BoT) kutoa Digital currency na kuiita e-TZS

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Ni muda muafaka kama Taifa tuwe na pesa yetu ya kidijitali yaani electronic currency yenye tabia na mifumo ya blockchain technology ambayo Itakuwa chini ya usimamizi wa Benk kuu ya Tanzania ( BOT).

Tangu Rais aongelee suala la pesa za mtandaoni alipozindua jengo jipya la Bank kuu ya Tanzania tawi la Mwanza hakuna taarifa yeyote imetolewa toka BOT.

Wakati ndio sasa wa BOT kuamua kutoa pesa yake ya kidijitali yaani e-TZS kama ninavyopendekeza, currency iwe yenye tabia na mifumo ya blockchain technology.

e-Tzs Itakuwa salama zaidi kwani BOT watakuwa na uwezo wa kuifuatilia(Regulate) tofauti na pesa zingine za kidigital ambazo zipo nje ya uwezo wa BOT kuzifuatilia( out of government Control).

Hofu kubwa ambayo BOT na Serikali walikuwa nayo sasa itaenda kuisha kwani pesa hii ya ( e-TZS) Itakuwa inafanya kazi kama pesa ya kawaida (Physical cash) chini ya sheria ya BOT.

Ni muda muafaka wa Benki kuu ya Tanzania kutengeneza Application ya ( e-Tzs) ambayo itawekwa kwenye iOS store na Google store kwa watumiaji kuanza kutumia pesa hii ya kidijitali yenye muundo na mifumo ya blockchain technology.

e-TZS itarahisisha mifumo ya manunuzi yaani( On line purchases) na itaondoa mfumo wa kuwa na Fedha halisi hivyo kuwezesha malipo bila pesa halisi yaani( Cashless transaction).

Muda wa maamuzi ndio sasa, Kwa kuwa Taifa limewapa BOT nguvu ya kusimamia mifumo yetu ya fedha hivyo ushauri huu ni muhimu kwa kuwa na Taifa imara lenye nguvu ya kitekinolojia.

e-TZS wallet kama ninavyopendekeza iunganishwe moja kwa moja na mifumo ya Mabenki pamoja na mifumo ya simu, e-TZS wallet Itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara, Wakulima na wafanyakazi wa Taifa hili la Tanzania.
 
Itapigwa sana serikali。e-gov yenyewe tu imewaelemea. Hakuna wataalam huko katika hii hii nyanja na hawana watu wakufanya transformation. Ukienda na CV yako kazi wanaziweka pembeni na kuendeleza princelings

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ni muda muafaka kama Taifa tuwe na pesa yetu ya kidijitali yaani electronic currency yenye tabia na mifumo ya blockchain technology ambayo Itakuwa chini ya usimamizi wa Benk kuu ya Tanzania ( BOT)

Safi sana lakini nini faida za blockchain technology kwenye hii e-TZS unayoongelea?
 
Una idea na digital currency lakini kitu ambacho hujui ni kuwa dhana kubwa ya digital currency au tuseme cryptocurrency ni kuondoa ukiritimba (regulation) ya central banks ndio maana inaitwa "peer to peer" , hatakiwi mtu wa kati (third part) hapo!
Digital currency bado ni eneo ambalo Serikali isilikurupukie bila utafiti wa kutosha ! That is bubble economy na muda wowote inaweza ku- burst against!
 
El Salvador wali anza kutumia hizo crypto currency na wameisha Lizwa!! Tuwe cautious tusiende kichwa kichwa sidhani hata hao viongozi wanaoshabikia kama wana uelewa wa hii technology!!
 
Ukisoma comment za watu kwenye huu uzi utagundua tuna safari kiasi kiasi gani kuyafikia maendeleo! Kazi ipo!
 
Kuilinda kuibiwa ni ngumu kwetu msana hatuna wataalamu wa kudhibiti mtandaoni. Wataalam wapo ila hawajiriwi kwa kuwa hawana marefa. Wanaoajiriwa sekta hiyo niwale waliosoma kushika mouth tu si waliosomea I T kwani ndugu zao ndo wana madaraka na mamlaka
 
Back
Top Bottom