Point sana chama kiwe kinapitisha Wabunge wakazi
Ipo haja kupunguza idadi wabunge.Walau 2 kila mkoa kwa njinsia.
Yeah! Ndio maana naona haja ya kuifanyia reform TAMISEMI.Kweli kabisa kuna haja ya kuwa na wabunge wanaoendana na mahitaji yetu.
kwa kuongezea katika hili mimi nilitamani mbunge awe ni mwakilishi wa wilaya, Badala ya kuhangaika na Kusema sijui wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi au wakuu wa wilaya basi kama fedha za serikali kuu zinatolewa ki wilaya au halmashauri na makusanyo cha chini yanafanyika katika ngazi hiyo basi wananchi wawe na mwakailishi ngazi hiyo.
Hata mimi nalikubali hiloPoint sana chama kiwe kinapitisha Wabunge wakazi
Hata akikaa jimboni kama ni mpiga makofi kwa kila kinachozungumzwa na kusema ndio kimepita ni kazi bure.
Una mawazo mazuri sana sana. Hili hata mimi nilishaliwaza siku nyingi. Wabunge wengi siyo wakazi wa maeneo wanayowakilisha. Infact kwenye nafasi ya ubunge kuna mapungufu mengi sana ambayo yanatakiwa kurekebishwa na hili la ukazi ni moja. Iwekwe sheria mbunge awe ni mwenyeji wa eneo husika na awe anaishi pale muda wote. Akisafiri basi anaenda tu kwenye vikao vya bunge. Halafu hawa wabunge wa viti (soma vitu) maalum wooote wanatakiwa kuondolewa. Hawa wamekuwa wanachaguliwa wale wanawake wajanja wajanja (wengi vimada wa viongozi) wanaishi mjini na wakiona wakati wa uchaguzi umekaribia ndiyo wanakimbilia maeneo husika. Kama ni suala la kutaka uwakilishi wa makindi fulani basi tuweke utaratibu wananchi kuwapigia kura huko majimboni. Idadi ya wabunge nayo ipunguzwe. Tuna waaunge wengi sana pasipo sababu yoyote. Kuna mengi ya kuangalia lakini ni vigumu wanasiasa kukubali kubadilisha kwani ndiko kwenye ulaji wao.Nchi inaongozwa kutokea Dar! Kwa sasa wanapanga mikakati ya ubunge.
Anyway! Wanaweza kuwa wazawa, na wakichuma wakimbia.
Tumesikia vigogo wamechuma Bongo na kukimbilia South, ....kusimika mahekalu, huku asilia wanaishi kimachalemachale. Kikisanuka, waamshe na familia zao. Ndivyo ilivyo kwa watawala wengi wa Afrika.
Kwa maoni yangu, kuna namna TAMISEMI inaweza kuboreshwa ili transparency, check and balance vizae matunda.
Tatizo lipo kwa wananchi wenyewe.
Kwa nini wamchague mtu ambaye siyo mwenzao kuwawakilisha au kuwasemea?
Anatakiwa muwakilishi wanayeshiriki naye katika mazingira wanayoishi.
Umasikini unaanzia hapo kwenye fikra za kuchagua mgeni.
Viongozi hutokana na wananchi, hivyo wananchi wa hovyo huchagua viongozi wa hovyo.ukiwalaumu wananchi basi hakuna haja ya kuwa na viongozi, kila mtu angeona njia sahihi na akafuata akafanikiwa, lakini kiuhalisia maisha hayako hivyo. jamii zetu nyingi mbumbu ambao wakipewa vitu wanachagua, wakichezewa ngoma wanachagua bado ni wengi. tatizo kubwa ni elimu au uelewa kwa maana wengi wetu hatuwezi kuunganisha maisha yetu na hawa tunaowachagua.
waliibuka wahuni wakabadili taswili za nafasi hizi, wapo waliozipa taswila za ngo za kutoa misaada hivyo wanatafuta misaada na kwenda kugombea. imekuwa kama kazi za mbunge ni kutoa mabati ya shule, kuchangia mifuko ya simenti n.k.
unahitajika mwongozo unaowaelekeza wananchi na kazi ya wananchi iwe ni kumalizia tu
wabunge wakazi mana yake nini mzawa ama? mbona mimi sijaelewaPoint sana chama kiwe kinapitisha Wabunge wakazi