Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Serikali yeyote makini katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake kipaumbele kikubwa ni kutoa huduma ya kama ya afya na elimu, lakini hapa Tanzania nakubaliana na nia ya serikali ya awamu ya tano katika kuifufua shirika la ndege la ATC, serikali iliponunua ndege 2 za Bombadier ilikuwa ni mwanzo mzuri ila haraka za kuongeza ndege zingine wakati sekta ya elimu na afya inazidi kuzorota hilo si sahihi. Mashirika makubwa ya ndege mfano Kenya Airways pamoja na kuwa na ndege nyingi na za kisasa zitaendelea kupata hasara mwaka wa hesabu 2015/16 shirika hilo lilipata hasara ya dola milioni 252 na mzigo wa deni hilo serikali ya Kenya imeibeba, mashirika mengi makubwa kama Air France,Air India,Lufthansa etc huduma zao nazo zimesusua kutokana na ushindani mkubwa kutoka mashirika ya ndege ya mashariki ya kati kama Emirate, Altihadi na Flydubai ambazo zinafadhiliwa sehemu kubwa na petrodollars kutoka kwenye serikali za nchi hizo.
Wizara ya Ujenzi kutenga bilioni 500 kwa ajili wa ununuzi wa ndege zingine bila kufanya feasibility study makini itakuwa ni upotovu wa pesa, serikali itambue wapiga kura wengi sio wanaotumia usafiri wa anga ni Watanzania walio wa kipato cha chini ambao wangefurahia sana kuona huduma hizo muhimu zikitolewa bure na nzuri.