NI vipi Thamani ya Fedha inapanda

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,743
Nauliza hivi ni vipi thamani ya pesa inapanda,Je Tanzania tunaweza kuipandisha thamani ya shilingi na kukaribiana au kuipita dola ,kwa njia zipi ?
 
Ndugu Mwiba,

Thamani ya fedha inaongezeka kufuatana na Principles za demand na supply.
Inawezekana kabisa fedha yetu ikaongezeka thamani iwapo mambo yafuatayo yatapewa naasi;
a. Kuongeza thamani ya mauzo ya nje (Exports) na kupunguza manunuzi ya nje (imports)

b.Manunuzi yote ya ndaniya nchi yafanywe kwa edha ya ndani na siyo kama tufanyavyo huku kwetu kwani biashara zinafanywa kwa dola kiasi cha kufanya pesa yetu kukosa thamani sokoni.

c. Kuuza vitu vilivyoongezwa thamani (not raw materials)

d. Kujenga uchumi imara unaojitegemea kwa kiwango kikubwa n.k
 
Hapa kuna thamani real na relative.Kuna kulinganisha na vipimo kama uwezo wa manunuzi au vipimo kama dola.

Thamani ya fedha inaweza kupanda katika vipimo halisi na vipimo vya uwiano.Kwa mfano hata kama thamani ya shilingi haijapanda kwa misingi ya uzalishaji na biashara iliyotajwa hapo juu, inaweza kupanda ikilinganishwa na dola kama dola itashuka (i.e shilingi ikisimama na dola ikashuka basi shilingi itapanda ikilinganishwa na dola) au hata kama uchumi ukishuka na kusababisha nguvu ya shilingi kushuka kwa asilimia chache, lakini nguvu ya ununuzi ya dola kupungua kwa silimia nyingi zaidi, basi kwa ujumla thamani ya shilingi itapanda ikilinganishwa na dola ingawaje kiuchumi uwezo wa kununua unaweza kushuka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom