gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,311
- 3,341
Kwanza nianze kwakusema mpaka hapa silaumu kitengo cha polisi kwani huenda hakijafanya hili kwakukosa taarifa.
Leo kupitia taarifa ya habari ya clouds TV ameoneshwa kijana dereva wa bodaboda ambaye kwa ushujaa mkubwa alifanikisha kukamatwa kwa jambazi Dar es Salaam.
Shujaa huyu ambaye aliwachomekea majambazi akiwa kwenye pikipiki na kupelekea yeye pamoja na pikipiki ya majambazi kuanguka jambo ambalo lilifanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa urahisi na askari.
Shujaa huyu licha ya kupata majeraha kwakuanguka na pikipiki lakini pia alipigwa risasi na jambazi iliopelekea kukimbizwa Muhimbili.
Amepata tiba lakini tatizo ni gharama za matibabu inahitajika 500,000 ili aruhusiwe pesa ambayo yeye hana.
Naamini kama polisi hua mnatangaza mpaka dau la 1,000,000 ili kufanikisha kukamatwa kwa majambazi naamini hamshindwi kulipa 500,000 ya matibabu na hata pesa ya ziada kama motisha kwa ujasiri aliounesha.