idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,282
- 38,359
Sidhani kama bila tamaa na ufisadi wa viongozi wetu ACACIA wangefanya utapeli wowote ule, kila walichokitaka ACACIA walipewa baraka na mwongozo wa kutosha kutoka kwa viongozi wetu.
Hizi sheria tunazosema mbovu ACACIA hawakutokanazo kwao, zilitungwa na viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kulinda rasilimali za nchi yetu chini ya serikali ya CCM.
Ni utani..lile lile bunge lililopitisha sheria mbovu ndio hilo hilo likarekebishe...utani huu....yule yule anaelipa bunge mwongozo wa kupitisha sheria ndio huyo huyo analipa bunge mwongozo wa kurekebisha sheria.?
Kuna haja ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kikatiba kuhusu umuhimu wa bunge letu kwa mustakabali wa Taifa letu.....
ikiwezekana hili livunjwe liundwe lingine lenye weledi.....ama tuanzishe lingine lisilo na itikadi ya vyama ili kusahihisha makosa ya bunge lililopo sasa.... maana hili linaburuzwa tu na serikali.
Bila katiba mpya mihimili yote inayojiita iko huru itaendelea kuwa kwapani mwa mhimili uliojikita chini.... rejea agizo la Rais leo kwa spika kuhusu wabunge wanaoitwa wakorofi.
Mungu ibariki Tanzania.!