Ni ugonjwa gani huu?

Feb 12, 2017
12
6
Huu ni ugonjwa gani,unasababishwa na nini,na unatibiwa kwa dawa gani?
IMG_20170214_182337.jpg
IMG_20170214_182332.jpg
 
hivi vitu uwavinatokea kwa mifugo uyo kang'atwa na vidudu vya kutambaa kama tandu nnge nk apo mtoboe na sindano utatoka upepo na damu damu then chukua mwalovela mpake alaf nyingine mnywishe
 
Kuku wana mifuko ya hewa tumboni inayojulikana kwa jina la air sacs. Mifuko hii ni sehemu ya mfumo wa hewa wa kuku. Inapotokea mifuko hii ya hewa kushambuliwa na vimelea vya magonjwa hasa bacteria ain ya E.coli, hupoteza uwezo wake wa kutunza hewa na hivyo hewa huishia kwenye ngozi. Cha kufanya: Kwa kutumia kifaa safi (sterile) chenye ncha kali mtoboe kwenye ngozi ili kutoa hewa hiyo. Hata hivyo hii sio tiba ya kudumu kwani hali hiyo itajirudia kadiri kuku anavyoendelea kupumua kwa hiyo utalazimika kutoboa mara kwa mara. Ili kuzuia tatizo kwa kuku wengine wape dawa ya kuua vimelea vya bacteria kulingana na maelekezo ya dawa husika
 
Asante kwa ushauri mzuri.Mungu na akubarikie na kukulinda.
 
Omiath hapo juu ameelezea vizuri na hii hali kitaalam inajulikana kama Subcutaneous Emphysema (yaani kujaa kwa hewa kwenye nafasi ya ngozi na nyama). Hii hutokea pale hewa kutoka kwenye air sacs au pamoja na mapafu inapovuja pia inaweza kusababishwa na taratibu za kimatibabu au dawa zenyewe ambazo husababisha mgandamizo wa hewa (pressure) kwenye mapafu kuwa mkubwa kuliko wa kwenye nyama nje na mapafu. Hali hii hupelekea zile alveoli kuchanika na kuruhusu hewa kuingia kwenye subcutenous. Matibabu ni kama alivyosema Omiath, ni kutoa tu hiyo hewa kwa sindano safi au surgical blade au kiwembe safi unachana kidogo tu ili hewa itoke. Haihitaji matibabu makubwa sana maana siyo hatarishi kwa kuku wako ila chanzo lazima kichunguzwe vizuri pengine inaweza kuwa pneumonia, hivyo hiyo itahitaji matibabu!!
 
Back
Top Bottom