Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)


Hata Bibi Bomba wa kule Bungeni anamkubali TL hata Mnyika pia. TL akiingia kwenye lango la CCM hawatoki. Anacheka na nyavu zao kama alivyocheka nazo kwenye jimbo lake katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
 
lisu ni wakili makini hakuna AG tanzania wa kufanana nae anae juwa sheria kama yy. kimsingi anahitaji muda zaidi wa kujijenga kisiasa. mheshimiwa yuko makini sana kisheria na huo ndo ukweli hata kama mimi ni ccm
 
lisu ni wakili makini hakuna AG tanzania wa kufanana nae anae juwa sheria kama yy. kimsingi anahitaji muda zaidi wa kujijenga kisiasa. mheshimiwa yuko makini sana kisheria na huo ndo ukweli hata kama mimi ni ccm

kwa mfano Lissu akifa leo, nani atachukua nafasi yake?
 
Hivi nyerere alikuwa malaika hata asifanye makosa? je asikosolewe? mkapa kafanya mangapi lakini anakosolewe? mzee mwinyi mbona anakolewa? amefanya mengi tu mema mbona hamuongei? lisu kama anataka kugombea afanye hivyo mwisho wa siku watz wataamua anae washwa nani? tanzania ya leo si kama ya zamani watu ndo watakao amua
 
Alafu lissu atashindwa kuulinda Muungano, ni bora ya Kikwete. Mtazamo wa Lissu juu ya Muungano wetu ni hasi sana.
 

Eeeeeeehhheeeee mkuu huyo tundu lissu ni noma sana yaani wakiweka hapa cv yake jamaa yuko vizuri huyo acha.
 
..mleta uzi umefanya kazi nzuri kumchambua mh.Lissu...ili watanzania wengi wazidi kumjua...maana hakika watu kama hawa wanahitajika kwa ukombozi wa mkwamo unaoikabili TZ ya leo....Taifa hili linahitaji sana rais mithili ya Lissu ili kuwakoma nyani kilagi...maana hakika taifa hili linaangamizwa na mafisi na manyang'au walafi...

...Nitaunga mkono uteuzi wa mtu huyu kugombea urais kwa nguvu zangu zote...na namwombea uzima kwa mola...ili siku moja aliongoze taifa hili...Siwaoni watu/wanasiasa wengi kama Lissu katika taifa hili...
 

Sio swala la kumeza wembe.
Lissu yuko very volatile kwenye swala la muungano.

Ni mtu anayekubaliana na aina nyingi sana za Muungano,kumbuka Muungano sio haki ya Binaadamu, Lengo kuu la Muungano ni kutengeneza dola yenye nguvu kwa namna zote, sio swala la haki.

Tunataka Rais atayejikita kutufanya sisi ni Taifa kubwa lenye nguvu,hata kama hati za muungano ni fake.
 

Yes kwa mahakama zenye mahakimu na majaji wanaopokea hongo lazima confidence iharibiwe na huu ndio umuhimu wa Lissu kwa sasa.

watu wanajichukulia sheria mikononi kwa kuwa hawaamini mfumo wa mahakama au wa kipolisi.Ni ujinga kuendelea kuwa na mahakama ambayo ni kichaka cha mafisadi na wawekezaji mithili ya singasinga,hii weakness ya mahakama imetumiwa na mafisadi,wanasiasa walaghai,wawekezaji feki,wauza unga na hata serikali yenyewe kwa manufaa binafsi na sio ya umma.watu wanaiba wakijua tutawafikisha mahakamani na watahonga watatembea mbele.
 
lisu hakuwahi kurudia mtihani kama lameki kidevu...,hapo ndipo nitapiga kura yangu kwa mara ya kwanza.
 
Alafu lissu atashindwa kuulinda Muungano, ni bora ya Kikwete. Mtazamo wa Lissu juu ya Muungano wetu ni hasi sana.
mtizamo wa Lissu kuhusu muungano ni reflection ya mtizamo na maoni ya jamii yetu kufuatia utafiti wa tume ya jaji warioba.Jiulize kwa nini amekubalika Zanzibar na Bara pia?By the way unafahamu misimamo juu ya muungano ya hao wagombea urais wanaotajwatajwa?Nimesema hapo juu kuwa sifa moja wapo ya Lissu ni kuishi na kuusema ukweli hakuna unafiki wala mawaa ndani yake.watanzania wa leo si wale wa miaka hiyo....watanzania wa leo wanahoji na wanataka majibu yenye tija na sio uongo uongo.
 
Tundu Lissu ni mropokaji na mpiga makelele anayetumia uwezo wake wa kuropoka na kuongea kwa sauti ya ukali kuweza kuwashawishi na kuwaaminisha watu kuwa anachokisema ni kweli. Hawezi kuwa mwanasheria bora huku hata hajui kama kinga ya Mbunge kwa kile anachokisema bungeni ni kwenye suala la madai tu na si kosa la jinai.
 

Muungano huanzia mioyoni mwa wanaoungana. Huwezi kuunganisha watu bila kuwapa faida zao za kuungana. Unapaswa kuwaambia hao watu watafaidikaje na muungano na uwasikilize wao wakupe aina ya muungano wanaoutaka na sio ule watawala wanaoutaka wao kwa maslahi yao. Muungano wowote ni lazima pande zote mbili zinufaike na kuungana kwao. Huwez sema muungano sio suala la kupata haki sawa sasa huo utakuwa muungano wa viongoz wachache kwa maslahi yao na sio wa watawaliwa yani wana nchi. Unahitaji uelewa kwenye swala la muungano wew. Hoja za kuwa taifa kubwa bila wananchi wake kuridhia ni ulaghai wa watawala. Upo hapo?
 
Unayosema nikweli ila cdhani km upole umelisaidia Taifa hili...kwa jazba ni kweli TL yuko hivyo lkn sasa ikiwa tumetawaliwa na wapole kwa miaka mingi nahakuna tulichofanikiwa cmbaya tukaongozwa na wenye jazba huenda wakatuvusha km Taifa

Inayohitajika ni jazba iliyochanganyika na busara. Jazba ya Tundu Lissu, waulize wananchi wa kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi. Jazba yake inatokana na dozi ya dawa alizopewa pale hospitali moja ya Dodoma. lakini kama hatuamini, agombee urais mwaka huu, tutampigia kura lkn tuwe tayari kwa matokeo ya urais wake.
 

Mueleweshe huyo hajui. Wazanzibari wanamuita ronaldoooo.....akawaulize wazanzibari kuwa lisu ni nani.
 

Hakuna asiekuwa na jazba duniani hatamaandiko matakatifu yanasema kuweni na hasira ila msitende dhambi. Je, ni wapi lisu alikuwa na hasira akatenda dhambi yakuuwa? Hata Mungu mwenyewe ana hasira sembuse Binadamu!? Naona hamna baya la lisu badala yake mnataka kufanya personal attack kwa chukibinafsi tu hapa. Hamnaga kitu kibaya kama uvivu wa kufikiri kwani hilo ndo tulichokosea tukamchagua kikwete eti kisa ana sura nzuri na ni mshikaji wa night club matokeo yake amekuwa mdhaifu kuliko hata mm.
 
Unaua kabisa ndugu yangu,kumbe nchemba ndo walewale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…