Ni tendo gani jema?

Ni tendo gani jema?

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
128
Reaction score
196
Tunatakiwa kutenda mema, siyo ili matendo mema yatupeleke mbinguni, hapana!, tunatenda mema ili kuthibitisha uwepo wa neema na kumtukuza Baba yetu wa mbinguni.
Waefeso 2:8-9, Mathayo 5:16

Hakuna tendo lolote jema unaloweza kulitenda, litakaloweza kumshawishi Mungu akukubali na akuokoe.
Ni tendo jema moja tu ambalo linamfanya Mungu akuhesabu kuwa huna hatia, tendo la Yesu Kristo kufa pale msalabani.
Hakika kama Isaya asemavyo, hata yale matendo yetu mema tunayojisifia, mbele za Mungu ni kama uchafu tu.
Isaya 64:6

Ukiamini kuwa Yesu alikufa ili Mungu akukubali wewe na kukusamehe basi utaokoka leo!
Tendo la kupigwa kwake.....
Isaya 53
 
Matendo 27 : 20 Jua wala nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, basi tukakata tamaa ya kuokoka.

... mengine ni magumu ya kimwili na ya kiroho karma hayo ya Mtume Paulo aliyosema hapo juu....
 
Yakobo 2:17 "Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake."
Kijana, tunaokolewa kwa neema (Imani), lakini neema (Imani) bila matendo imekufa. Kwa maana nyingine ni kwamba Matendo pekee hayatoshi kumuokoa mtu, na Imani pekee haitoshi kumuokoa mtu. Neema (Imani) ambayo Mungu anaiweka ndani yetu, inabidi ijidhiirishe kwa matendo mema ya nje. Waambie na wenzio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom