Ni serikali iliyofeli au wanafunzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni serikali iliyofeli au wanafunzi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by tindikalikali, Apr 12, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Ebu pitia hki kinachoitwa “vision”, mission” na sehemu ya katiba yetu.

  MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATINAL TRAINING

  VISION
  To have a Tanzanian who is well educated, knowledgeable, skilled, and culturally mature to handle national and international challenges in various political, and social-economic fields by 2025.

  MISSION
  To ensure that there is an appropriate legal and practical working environment to enable all stakeholders who are eager and able to provide quality education participate in its expansion at all levels and provide equal opportunities to all; as well as enhancing cultural administration, supervision and infrastructure.

  KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977
  11(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

  11(3) serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule ma vyuo vinginevyo vya mafunzo,

  Matokeo yalitoka huku wanafunzi zaidi ya nusu wakiwa wamefeli (wameshindwa kupata alama mbili za D). mimi sikushtushwa na haya matokeo sababu niliyategemea kutokana na mchakato wa zinazoitwa shule hasa za kata zinavyoendeshwa.

  Ifahamike kwamba shule ni mchakato unaoendelea kati ya mwalimu na mwanafunzi hivyo uwepo wa majengo pamoja na wanafunzi pekee hakukamilishi maana ya shule. Je hapa asiyekuwepo shuleni anafeli vipi? Watoto wanafeli vipi wasichofundishwa? Hivi somo lenye mada 40, alafu mwanafunzi akafundishwa mada 3, alafu mtihani ukatungwa kwa kufuata mada zote 40. huyu mwanafunzi anapiwa vipi? Hizi ndizo fursa sawa zinazohubiriwa na katiba yetu?
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ..kuwa na mission and vision is one thing towards attainment of any goals

  ..but the most important is whether you have (at hand or stashed somewhere), the TOOLS, MEANS, WAYS, and of course the WILL etc. of getting to that goal and thus fulfilling your mission and vision as well. Ndio kusema fursa sawa ni sawa ila si sawa! Hazijawekwa nyenzo wala nia ya dhati kufikia malengo haya tuliojiwekea.

  ..sitaki kukubali kuwa shule za kata ni 'tatizo' -- 1) hazina uendeshaji tofauti na shule nyingine za serikali, 2) zinafuata mtaala ule ule, 3) zinasimamiwa na wizara ileile na wataalamu walipitishwa na mfumo uleule kama shule nyingine. Siasa ni tatizo hapa, pia World Bank ambao walitoa msamaha wa deni na zikapatikana fedha za kujenga shule hizo.

  and that's where 'we' (i don't know 'who' exactly) have failed
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ..pia kumbuka Katiba ya JMT (1977) ibara ya 11 (2) inahimiza kujielimisha na sio kuelimishwa .... kulingana na stahili na uwezo

  kwa kifupi pamoja na falsafa ya Ujamaa ya JKN bado nasisitiza (na haya ni maneno yake actually) kuwa 'Sawa isiyokuwa sawa ndio sawa'
   
Loading...