Ni sehemu gani sahihi ya kumshitaki mwenza anayekunyima haki ya ndoa?

Didododi

JF-Expert Member
Jul 21, 2023
321
426
Wadau mko aje.

Leo nalisasambua jukwaa nikiileta mada hii ambayo inahusu kunyimana haki ya ndoa nikimaanisha tendo lenyewe.Wanandoa walio wengine wamekuwa wakilalamika kunyimwa haki yao ya ndoa.Kulingana na mahojiano ambayo nimefanikiwa kuwafanyia baadhi ya wanandoa wanadai muda mwingine hunyimwa haki hii kutokana na na kutofautiana baina ya wanandoa hivyo mmojawapo kuamua kumnyima mwenza wake haki hii kama kutaka kumkomoa.Tuchukulie kwa mfano mwanaume katofautiana na mwanamke katika ndoa mwanamke anaamua kumnyima mwenza wake kwa muda usiojulikana mfano mwezi mzima,mwaka au hata miaka.(inaonekana hili limekuwa likizidisha mgogoro badala ya kuutatua)

=======================================
Pia mambo mengine ambayo yameonekana kupelekea tatizo hili ni pamoja na kushinikiza jambo flani(Mfano mke anataka atimiziwe kitu flani na mumewe anaitumia njia hii kumshinikiza mumewe,akishindwa kutimiza anaendelea na msoto wake)

Lipo pia suala la kutojisikia.Hii hutokea pale ambapo mmoja wa wanandoa anapokuwa hajisikii.Hii inaweza kuwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo upendo kupungua,matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango na msongo wa mawazo.

Pamojana hayo pia Kuna swala la dharau.Hili hutokea pale ambapo mmoja wa wanandoa anaposhindwa kumtimizia mwenzake hivyo kushindwa kumkata kiu.(kwenda chini ya kiwango)Inapotokea swala hili linajirudia mara wa mara mmoja wa wahusika huweza kumbeza mwenzake na kukata huduma(huku akisearch for competent one kitani)

===============================
Jamani sababu ni nyingi nitaendelea kuwashirikisha kulingana na interview mbalimbali ambazo nimefanya.Ninachoweza kusema ni kwamba tatizo hili ni kubwa katika jamii tunazoishi japo halizungumzwi bayana kwa kuhofia aibu ,imefika hatua watu kufanyiana ukatili kutokana na sababu hii,(wengine wamekuwa kill...d na wengine hata kupeana ulemavu)Ndoa zishavunjika kwa sababu hii,Leo hii kuona Mume na mke wanalala vyumba tofauti imekuwa kawaida.

SASA ILI KUWEKA MAMBO SAWA NA KUNUSURU HALI NI SEHEMU IPI SAHIHI YA KUPELEKA SHAURI KAMA HILI.JE KWA WAZAZI? KWA MSHENGA ,KWA KIONGOZI WA DINI AMA WAPI?
 
Anza kwa mshenga ikigoma nenda kwa wazee na wazazi ikigoma ita mwenyekiti wa kitongoji ikigoma peleka kwa mtendaji ikigoma nenda kata ikigoma nenda mahakamani hapo mnasikilizwa siku moja siku ya pili mashahidi siku ya tatu talaka
 
Tatizo hawa wake wa sikuizi hawafundwi, mwanaume ni haki yake kupata tendo hatakama mmegombana,

Hawa wake wa sikuizi ni visirani tuu halafu wanaamini kumnyima mwanaume ni kumkomoa,

Ndio maana tunapata sana amani kwa michepuko kuliko wake zetu
 
Wadau mko aje.

Leo nalisasambua jukwaa nikiileta mada hii ambayo inahusu kunyimana haki ya ndoa nikimaanisha tendo lenyewe.Wanandoa walio wengine wamekuwa wakilalamika kunyimwa haki yao ya ndoa.Kulingana na mahojiano ambayo nimefanikiwa kuwafanyia baadhi ya wanandoa wanadai muda mwingine hunyimwa haki hii kutokana na na kutofautiana baina ya wanandoa hivyo mmojawapo kuamua kumnyima mwenza wake haki hii kama kutaka kumkomoa.Tuchukulie kwa mfano mwanaume katofautiana na mwanamke katika ndoa mwanamke anaamua kumnyima mwenza wake kwa muda usiojulikana mfano mwezi mzima,mwaka au hata miaka.(inaonekana hili limekuwa likizidisha mgogoro badala ya kuutatua)

=======================================
Pia mambo mengine ambayo yameonekana kupelekea tatizo hili ni pamoja na kushinikiza jambo flani(Mfano mke anataka atimiziwe kitu flani na mumewe anaitumia njia hii kumshinikiza mumewe,akishindwa kutimiza anaendelea na msoto wake)

Lipo pia suala la kutojisikia.Hii hutokea pale ambapo mmoja wa wanandoa anapokuwa hajisikii.Hii inaweza kuwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo upendo kupungua,matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango na msongo wa mawazo.

Pamojana hayo pia Kuna swala la dharau.Hili hutokea pale ambapo mmoja wa wanandoa anaposhindwa kumtimizia mwenzake hivyo kushindwa kumkata kiu.(kwenda chini ya kiwango)Inapotokea swala hili linajirudia mara wa mara mmoja wa wahusika huweza kumbeza mwenzake na kukata huduma(huku akisearch for competent one kitani)

===============================
Jamani sababu ni nyingi nitaendelea kuwashirikisha kulingana na interview mbalimbali ambazo nimefanya.Ninachoweza kusema ni kwamba tatizo hili ni kubwa katika jamii tunazoishi japo halizungumzwi bayana kwa kuhofia aibu ,imefika hatua watu kufanyiana ukatili kutokana na sababu hii,(wengine wamekuwa kill...d na wengine hata kupeana ulemavu)Ndoa zishavunjika kwa sababu hii,Leo hii kuona Mume na mke wanalala vyumba tofauti imekuwa kawaida.

SASA ILI KUWEKA MAMBO SAWA NA KUNUSURU HALI NI SEHEMU IPI SAHIHI YA KUPELEKA SHAURI KAMA HILI.JE KWA WAZAZI? KWA MSHENGA ,KWA KIONGOZI WA DINI AMA WAPI?
Kwa IGP wambura atakusaidia mpka kumpindua mkeo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom