Ni sayansi lakini wanaume wenzangu tuache hii

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,998
Nitajaribu kuiweka iwe interesting lakini nivumilie kidogo. Lets go into a classroom (Hata kama sio vitu zako soma!)

Ufunguo: Kuna metali (Metal, kama vile chuma, shaba n.k) na Si-metali(Non-Metal kama vile oxygen tunayovuta n.k) ila zote ni elements.

Substitution or Single Replacement Reactions
A single free element replaces or is substituted for one of the elements in a compound. The free element is more reactive than the one its replaces.
Cu + 2 AgNO3 -----------> 2 Ag + Cu(NO3)2
copper silver nitrate silver copper (II) nitrate

Sasa wazia kwamba metali ni ME na simetali ni KE.
Compound ni muunganiko wa element mbili ama zaidi, wazia hizo kama ni Couple (Wife/Husband au Girl/Boyfriend, you name it)

Okay, So I was having lunch with my wife. Tulienda sehemu moja wana samaki wazuri sana (Mwanza). Sasa nikanotice kwamba mke wangu hakua focused. Ila nikanyamaza. Tukala tukarudi Hotelini tulipoweka makazi ya muda. Baadae kwenye stori akaniambia kuna jamaa pale Bar alikuwa akimkonyeza sana. Kiasi kwamba akahama kiti lakini jamaa yuko naye tu. Hakuniambia pale kwa sababu hakutaka kuharibu "the moment" (Or whatever that means).

Kuna kipindi fulani (Back in the youthful days), nilimpata demu mmoja mkali balaa. Hapo nilishamhonga sanaaa, kashanizungusha sanaa! Kiukweli hata kama nilimpata hii ilikuwa Project hasara tu! Sasa Nikawa naye Hotelini maeneo ya Ilala. Ilikuwa Hoteli kali mpya room was 70,000/- (Yes, to me ndo version of expensive room For a Project). Hapo tushakunywa na kula akati namwambia nikacheck room anapata emergency mama yake kalazwa we had to go. Grrrr!!
Nikatangulia kuchukua usafiri ye kabaki nyuma kidogo. Kumbe ghorofani kuna jamaa flani la kiarabuarabu (Probably a drug dealer. Wanasema hiyo hotel matajiri wa unga wako wa kutosha). Hilo jamaa lilikuwa linatuangalia mda mrefu toka tumefika. Bana likashuka linamtongoza huyo demu. Nilimind lakini siwezi kuanzisha chochote. Nikamchukua tukaondoka zetu.

Now consider our example, wakati tupo kipindi cha Chemistry. Yani pale silver (Ag short for Agragarium the latin word for Silver) yuko na wake/michepuko/girlfriends Nitrate (Nitrogen na Oxygen) zake . Akaja kidume kijinga Copper (Cu au kilatini Cuprum) kikachukua wote kimamuacha Silver anang'aa sharubu.

Sababu ni kwamba Copper ni reactive kuliko Silver. Yani kamzidi uwezo wa kuchukua non- metals. Ndivyo Asili(Nature) ilivyo. Mimi sijaja hapa kupingana na Nature, lakini kiukweli, mwanaume unaona kabisa mwanamke yuko na mume/bwana yake ni kwanini uattempt kumchukua. Na sio kwamba kakuambia nina mtu wangu wala nimeolwewa, ni kwamba mhusika unamuona pale. Yani utadhani ni kiazi umeona na si Mwanaume mwenzio!!!
 
Mtoto wa kiume anaenda shule asubuhi njiani anaokota mawe anarusha rusha na huku anatembea watoto wadogo wanacheza gololi anavamia na kunyanganya ama kucheza nao, anaonga mbele kuelekea shule. Jioni anaporudi anapanda panda miti na kuruka huku na kule. Wa kike anatoka nyumbani kuelekea shule anajikunyata na madaftari yake moja kwa moja hadi shule, karudi jioni anatulia tu na wenzake kupiga umbeya wa shule ama kuongelea series ya jana yake. Nature wanaume tumeumbwa kujaribu jaribu hivi na kuwaza vitu vizuri utapataje haijalishi hata kama utauwa mtu.
 
Back
Top Bottom