Ni sawa kukemea uzee kwa njia hii??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sawa kukemea uzee kwa njia hii???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Jan 10, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuna tabia kwa baadhi ya wazee wetu hasa waishio mijini kufanya mambo ya ajabu yasiyoendana na umri wao kama vile kuwa na mahusiano na vijana wadogo kwa kisingizio cha kukemea uzee! Nina mifano kadhaa, kuna mzee mmoja pale mikocheni huwa hakosekani bills anadai muziki wa sasa ni mtamu sana na anausikia mpaka kwenye damu! Pia ana kazi ya kuvimaliza vibinti vya sekondari anasema vinampa joto sana na anajisikia bado anadai - anakemea uzee!

  Si ajabu tena siku hizi kukuta mama mtu mzima amejichuna ngozi, kichwani kajitwisha kichaka cha nguvu, kapiga kimini au top inayoacha sehemu kubwa ya mwili nje huku pembeni akiwa na kaserengeti boy katika harakati za kukemea uzee! Kuna mama mmoja alipoulizwa juu ya tabia yake hii alisema uzee unaanzia chalinze Dar hakuna mzee!

  Sasa najiuliza, hakuna njia nyingine ya kukemea uzee (kama uzee ni lazima ukemewe) zaidi ya hii inayoenda kinyume na maadili yetu?


  Annina
   
 2. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Annina
  Zeeka kwanza na wewe utajua kwanini tunakemea uzee (just a joke)
  Kama wanakurupua chini ya umri, wanabaka au wanatumia ofisi za serikali, madaraka waliyonayo na hela za walipakodi kukemea uzee, ni suala la kuhoji. Kuna maadili ya uongozi ambayo hayatakiwi kusiginwa.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  haya ni matabia tu ya hao wazee
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  madingi wa siku ni mafaki..
  kina mama sijui tuwaiteje, labda mabomu.
   
 5. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kuna watu wana majibu ya mkato kiasi kwamba hutakaa umuulize tena! The bottom line is Tanzania is a dying nation! Kuanzia kwenye uongozi wa nchi mpaka kwenye mmomonyoko wa maadili kwenye jamii tunazoishi! Yaani imefika mahali ambapo kuna vitu vinaonekana vya kawaida wakati viko kinyume na maadili.

  Mashoga siku hizi eti wameanza kuonekana ni watu wa kawaida katika jamii, hawajifichi tena. Vibinti vya sekondari siku hizi wala havina ''boyfriends'' wanaosoma nao, wana wakaka na wababa wanaofanya kazi na wenye kipato. Wanafunzi wenzao wanawaita ''daddy I am goin''.....!!!

  Niishie hapo kwa sasa!
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  We annina wewe

  umenichekesha sana,
  eti uzee unaanzia chalinze.....ha ha ha ha.....
   
 7. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Usiwalaumu sana wazee, vibinti vya siku hizi vina tabia za ajabu sana! Na hizi simu za mkononi ndio kabisaaa!

  Kuna siku simu yangu iliishiwa chaji na umeme ulikuwa umekatika, nikaomba ''handset'' ya mtoto wa kike wa anko wangu aliyekuwa kaja kunitembelea pale kwangu. Akanipa, nikaweka laini yangu lakini meseji na namba nyingi za simu zilibaki kwenye ile ''handset''. Niliyoyaona humo nilitetemeka !! Mtoto ana umri mdogo lakini mambo yake ni makubwa kuliko hata mimi mwenyewe!!!
   
 8. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  kama vile kuwa na mahusiano na vijana wadogo.

  Si ajabu tena siku hizi kukuta mama mtu mzima amejichuna ngozi, kichwani kajitwisha kichaka cha nguvu, kapiga kimini au top inayoacha sehemu kubwa ya mwili nje huku pembeni akiwa na kaserengeti boy katika harakati za kukemea uzee!

  1.hayo mahusiano kama ni ya hiyari basi mi' sioni tatizo waache waendelee kumegana.

  2. binadamu kujipamba hiyo ni hiyari yake.mavazi na mapambo ni mambo ya kibinfsi zaidi na kiutamaduni. unayoyaona wewe kuwa si mazuri, basi utamaduni na utashi wa mtu mwingine kwake ni jambo jema...!!
  acha watu wajipambe.................!!!!!
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280

  Ukiangalia kwa makini, hao wanaojitapa hivyo si wengine bali ni wale waliokata pande kubwa la keki ya taifa. watu wenye kwenda bills na kuhangaika na watoto wa shule pamoja ba viserengeti boys ni kwamba wana finacial capability ya kufanya hivyo na mara nyingi wala sio pesa za kustaafu manake mishahara inafahamika-ni zile zile zetu walizojipatia kwa njia ambazo si halali hata kama hatuwezi kuprove hilo!

  uzuri hawakawii kufia viuoni kama Mc Lema (RIP)
   
 10. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Masaki umesema sawa kabisa, yaani jibu la huyu mama lilijitosheleza kiasi hapakuwa na maswali ya nyongeza!


  Annina
   
 11. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35


  The Boss, mi pia nilicheka sana kwa majibu ya huyo mama, kwahiyo usihofu juu ya uzee as long as unaishi Dar!


  Annina
   
 12. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Wazee nao watu wanahitaji mapenzi, Katika mapenzi hakuna umri jamani.
   
 13. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mama mmoja alipoulizwa juu ya tabia yake hii alisema uzee unaanzia chalinze Dar hakuna mzee!

  You make my day!!,Yaani nimecheka mpaka mbavu zinauma,that is why naipenda JF
   
 14. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Asante sugar wa ukweli, nafurahi kama umecheka maana kuna faida kubwa kiafya!


  Asante sana,

  Annina
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unaposema tunahitaji busara za wazee katika kila jambo ni kama hivyo!. Hata vijana sasa wanaona wakiwa na wazee hakuna kero kuliko kijana mwenzie. Uzee dawa, na kwa ujumla tafsiri ya uzee ni "subjective".

  Mugabe ana miaka zaidi ya 80, mkewe ni 3os,
  Hon. Wasira 60s, mamsapu 30's

  nk.
   
 16. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  hahahahaha hehehehehe huyo mama keshajichokea....
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa wamama watu wazima; lets say 40+ hawasumbui kabisaa...
  wasichana -30 wanakera, kwanza wana penda kuringa na kupiga mizinga ya ajabu ajabu sana! Wacha niendelee kuitwa serengeti boy...Raha si napata mimi...
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mmmmh.
  Na wewe ni mwanaume???????
   
 19. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  wee Pape una lako jambo> Wakati mwingine kumtosheleza mtu mzima yahitaji msuli, unakuta jimama tayari 9 kids na mwanae wa mwisho ana umri sawa n wewe . Hapo yanaweza kukufika yale yule Mc wa kichaga Bw. Lema (R.I.P).

  Young woman vs old man

   
 20. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  mhhh..........
   
Loading...