Ni Samatta au nimsubiri mwingine?

Iyegu

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
6,276
12,397
Kuna raha yake kumuona mchezaji wa nchini akacheza mpira huko LaLiga,Bundesliga au pale kwa Malkia.
Unamuona mtu wa Kondoa,Kyela au Mbagala akicheza timu moja na Messi au yupo pale kwa Mourinho na Pogba,ana furaha gani mkenya anayemuona Olunga anafunga hat-trick LaLiga?...
Wakati Mbwana Samatta akianza kuwika nilijua huenda akawa Mtanzania wa kwanza kumuona kwenye ligi kubwa duniani.Lakini hali ninayoiona sasa inanifanya nijiulize "ni Samatta au nimsubiri mwingine?"
 
labda tumngoje mwingine huwenda vipofu wakaona, viwete wakatembena na viziwi kusikia
 
  • Thanks
Reactions: Osu
Fuatilia historia ya Shaaban Nonda( hasa ktk suala zima la mazoezi, nidhamu kujituma, malengo + mipango na subra) kisha linganisha na wachezaji wetu walio wengi utatambua kuna tofauti kubwa sana. Tunaridhika mapema mno wabongo
 
kama mtanzania napenda kumuona mtanzania mwenzangu akiipeperusha vyema bendera yetu, nani ambaye hapendi kumuona samatta akichezea epl, bundesliga, la liga, league 1 ama serie A ? Hakika tunapenda sana kumuona lakini kwa mwelekeo wa samatta hatafika huko, hapo alipo ndio kafika na asipokuwa makini Genk inaweza kumuacha akajikuta anaporomokea timu ya chini zaidi, akaishia kwenda sweeden, south africa, agypt, morroco na kwingineko.... kwa nini nasema haya ?

1. umri unamtupa, namkadiria ana 27-30, japo passport yake inasoma 24. kwa huu umri alio nao sasa anatakiwa ndio afikie peak kwenye kiwango chake lakini ni wa kawaida sana, bahati nzuri tangia msimu uliopita anapata namba pale Genk lakini kiwango chake (ufungaji magoli) sio mzuri. sina takwimu sahihi lakini sidhani kama amefunga goli 50 tangia atue kule, japo msimu wa kwanza hakuwa anapata muda mwingi wa kucheza, lakini tangia msimu uliopita anapata namba, hana cha kusingizia tena.

2. nafasi anayocheza(striker) inamgharimu sana, angekuwa midfilder, winger au beki kwa jinsi anavyojituma na spirit aliyonayo pengine kwa sasa tungekuwa tunaongea mengine, hata acheze vizuri vipi, hata atoe assist nyingi bado ataonekana kawaida, anatakiwa azifumanie nyavu kwa kiwango cha juu sana.

ukweli mchungu
 
Nilitegemea atakuwa na msimu mmoja Tu pale Genk lakini kwa sasa sijui kitakachotokea.
 
Back
Top Bottom