ni sahihi kwa mwanaume.....

kiasilia m/mke anatakiwa kutunzwa na kujaliwa na mumewe hata kama ana hela kiasi gani itabidi tu uwe unampatia vizawadi ili aone unamjali hata kama ana kipato zaidi unaweza kumwomba hela kisha unamnunulia zawadi kwa hela yake hiyo hiyo ili mradi ajue kuwa unamjali
 
Hapo inategemea wewe na mwenzio na set up ya maisha yenu, kama ulimzoesha hivyo go for it na kama ulimzoesha the other way round ujue kuwa ishi hivyo. wanawake ni wa ajabu hawapendi kubadirishiwa utaratibu all of the sudden. lakini wapo wengi sana ambao pengine wana play role kubwa kuliko sisi wanaume hata pesa wanatupa pale mambo yetu yanapokuwa mabaya au hata kama bado mazuri lakini wanajitoa. wenye kupenda hivyo naweka doubt !!! ni vicheche pesa zao wanapeleka wapi sasa? na nini maana ya ndoa? is all about sharing kwa christian.
 
kiasilia m/mke anatakiwa kutunzwa na kujaliwa na mumewe hata kama ana hela kiasi gani itabidi tu uwe unampatia vizawadi ili aone unamjali hata kama ana kipato zaidi unaweza kumwomba hela kisha unamnunulia zawadi kwa hela yake hiyo hiyo ili mradi ajue kuwa unamjali
Hao ni wanawake wa kiswahili.
 
hivi katika maisha ya sasa ambapo unakuta mwanaume ameoa mke mwenye kipato eg. mhasibu, mhandisi, au ambaye ana shughuli zake binafsi za kumwingizia pesa ya kutosha kwa wao kama mke na mume kushare majukumu ya kuendesha familia mfano watu siku hizi wanashare ujenzi,rent,bill za nyumbani,ada za watoto et.., je ni sahihi kwa manaumwe kumpa mkewe pesa za matumizi yake binafsi? pesa kwa ajili ya mke kununua mavazi,kwenda saluni nk nk! au hii kwa sasa dhana iliyopitwa na wakati na ya kiutamaduni zaidi?? au kwa kuwa mke anauwezo wa kupata kipato haina sababu kwa mwanaume kumpa mkewe fedha za matumizi?

kwenu wadadavuzi naomba kuwasilisha!

Sidhani kuoa mke mwenye kipato kizuri inampa mwanaume tiketi ya kutotimia wajukumu ya kiume(yanayoimarisha upendo) kwa mkewe...!! wajibu huo unaenda nafsini kwa mwanamke na si mfukoni.kama ulizoea kumletea ubuyu na ukwaju wakati wa mapenzi yenu..moto ubaki palepale au uongezeke..USILEMAE KIJANA!!
 
Nailyne, labda nikuulize swali, unaposema ni sahihi kupewa hela za matumizi unamaanisha nini;
(i)kwamba mwanamke anadai apewe hizo hela sababu ni mke wa jamaa, au
(ii) jamaa anampa tu mkewe sababu anajisikia kufanya hivyo?

Kama ni sababu ya kwanza, nadhani huyo mke hamtendei haki mume kumdai hela wakati naye ana kipato kikubwa, akumbuke kuwa maisha ni kusaidiana, mnajenga familia yenu kama kitu kimoja.
kwa namba mbili mimi naona ni sahihi, maana siyo sababu nina kipato kikubwa basi hutaki kabisa kujigusa kuhusu matumizi yangu. kumbuka kuona unajali navaa nini au naendaje saluni kunaongeza mapenzi katika ndoa. na hii ni kwa pande zote, hata mke ni sahihi kumpa mumeo hela ya matumizi yake hata kama mshahara wake ni mara 4 ya wako
 
kwa kweli.....vitu vingine ndo maana wanaume wakienda nje...ukimuuliza anasema we shida yako nini??kwenda kwangu nje kuna ulichokosa,hela si unapata,kodi unalipa wewe.gari umenunua wewe......kama huwezi waweza enda......heeeeeee.....uomba omba mwingine siyo......:decision::decision:

Hapo ndo baadae tunaanza kulalamika ooohhh mume wangu kumbe umejisababishia mwenyewe kama huna uwezo sawa kama unauwezo jihudumie bana
 
Mwanamke aliyeolewa anahitaji security toka kwa mumewe. Upendo wa mume kwa mke ni moja ya vitu ambavyoonyesha mwnamke yuko salama kwa mumewe. Kumpa pesa za vitu kama saloon ni muhimu sana kwani huonyesha upendo wa mume kwa mke. Mwanamke ni mwanamke tu! haijarishi anapesa kiasi gani.

Mapenzi sio pesa bana wewe malunde nini.
 
Ndoa ni muungano unaomfanya mwana-mke na mwana-ume wawe kitu kimoja, kipato kinachopatikana ndani ya ndoa ni chenu wote na siyo cha mmoja wenu, endapo unadhani ndani ya ndoa kuna cha mke na mume unajidanganya wewe mwenyewe kwani mahitaji ya famialia mnaya gharamia nyie wenyewe kila mtu kwa mafasi yake au uwezo wa kipato chake. Ni dhana potofu kudhani unafaidi kwa kuchua fedha kwa mumeo, unachokifanya unadidimiza maisha ya familia yako mwenyewe. Ni wajibu wa kila mwandandoa kuchangia mahitaji ya familia kutokana na kipato chake bila kujali jinsia. Familia ambazo zimeweza kufanya mambo kwa pamoja zina mafanikio kuliko familia ambayo mwanamke ana mtazamo wa kusubiri cha mume na kudhani cha kwake ni cha ziada.
 
Nailyine unakuwa kama huwajui wanawake bana? dem wa kiswahili chake ni chake hata kama ana mamilioni na cha mme/bwana/hawara ni chenu wote hata kama ni ndururu!

Inabibi ufanye hivyo na uhusiano wenu utakuwa strong! Ukileta za kuchungulia salary slip ya mwenzio, mtagombana.. As a man unatakiwa ku-take full responsibility....
 
yani NI SAHIHI KABISA KABISA....hata kama nna kipato ...NKIOMBA NAULI NIPE,HELEA YA NGUO NIPE...WANAUME WAMEUMBWA MATESO.....nafikiri ni sahihi wtaoe na mi napewaga..japo mtu analalamika lakini ndo hivyo si wanawake tunamabo mengi wao hilo tuu aaaha.....YANI ATOE KWA MOYO 1....HATA KAMA NIMEMZIDI MSHAHARA....and i love this part.......anavyolalamika pale....lol...:wink2:

Uko sahihi vkeisy, I am a Man, I will take care of you.... there i will be proud..
 
Kuna mwanaume nafanya nae kazi alishaniambiaga anapenda sana kumuhudumia mkewe hata kama anafanya kazi ,ile inampa furaha sana kuona anampa pesa mkewe kufanya mambo yake lakini mkewe hapendi. hali ile imemfanya kujiona kama sio mwanaume vile basi matumizi yote kama salon, shopping na mengine mengi anampa mistress wake. sasa na huyu utamweka kwenye kundi gani?
Mie pia naona ni vizuri mume kumtunza mkewe kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini hata kama mke ana kipato gani. inaleta heshima fulani hivi. mwanzangu asubuhi pesa ya wese na lunch naikuta kwa dressing table kama yupo siku hiyo hata kama kwenye wallet nina kilo mbili.Ila siku nikipata mshahara najitutumua sana kufanya vitu vinavyoonekana baada ya hapo mwendo ni uleule
 
Mimi sikubaliani sana kwamba lazima mwanamke ahudumiwe na mwanamume. Kwa sababu kama wote mnafanya kazi inabidi mgawane majukumu ya nymbani kwenu ili kujenga familia iliyo imara. Mwanamke ambaye hata kama ana pesa lakini haitumii kuhudumia familia mie nadhani huyo si mjenzi wa nyumba.

Hivi kweli wewe unajua kipato cha mume wako na hali halisi ya maisha mliyo nayo utadai kweli unataka kupewa pesa? kama akilipa ada ya shule kwa watoto si atakuwa amefanya jambo jema, na wewe ukipitia sokoni ukanunua mahitaji au ukapitia salun ukatengeneza nywele kwani kuna shida gani? Hayo mawazo kwamba mwanamke lazima ahudumiwe yalikuwa ni ya zamani na kwa wale kina mama wa nyumbani.

Familia inajengwa kwa kushirikiana mume na mke na kuwa na malengo na pia kuwa na mgawanyo wa majukumu kwa wote wawili kulingana na kipato chenu.
 
yani NI SAHIHI KABISA KABISA....hata kama nna kipato ...NKIOMBA NAULI NIPE,HELEA YA NGUO NIPE...WANAUME WAMEUMBWA MATESO.....nafikiri ni sahihi wtaoe na mi napewaga..japo mtu analalamika lakini ndo hivyo si wanawake tunamabo mengi wao hilo tuu aaaha.....YANI ATOE KWA MOYO 1....HATA KAMA NIMEMZIDI MSHAHARA....and i love this part.......anavyolalamika pale....lol...:wink2:

kwa mtizamo wangu mwanamke anatakiwa ajirembe mwenyewe,kama nguo anunue mwenyewe ntamsaidia pale ntakapojisikia lakini isiwe ni lazima.Au ndio nyie mnaingia bar unamwachia mumeo afungue pochi yake hata kumpa ofa hutoi au kumnunulia nguo mumeo apendeze huwezi.Kipimo cha mwanaume cha kumpata mke mwema ni yule anaeijtoa kwa wajili yako sasa siku sina kazi atanistahi kweli?CHa kushangaza unakuta ana mshahara mzuri lakni hata kuchangia ujenzi au ununuzi wa kiwanja hataki,anataka kuvaa nguo za gharama na magold wkt huo huo mnakaa nyumba ya kupanga ni ajabu sana.Wanawake badilikeni sasa wanaume watunzeni kama watoto wenu, hata mke ambae hana kazi lakini kwa mwerevu atajitahidi kusave hela anayopewa ya matumizi na kumsuprise mumewe kwa zawadi..
 
Mi kwa kweli sitii hata senti labda ndio nibadilike ila hata nikiamua kuchangia nitajikua nafanya kitu kidogo labda shopping za sokoni sababu hata nisipoomba nawekewa tu, bwana ee mi nafikiri kuna wanaume na wanaume wengine sidhani kama anahitaji hata senti yako moja. Ila hii thread imenifungua macho aisee inabidi niangalie hili jambo kwa upande wa pili, ila sasa nikianza kuchangia yeye pesa zake atapeleka wapi? maana...........
 
kwa mtizamo wangu mwanamke anatakiwa ajirembe mwenyewe,kama nguo anunue mwenyewe ntamsaidia pale ntakapojisikia lakini isiwe ni lazima.Au ndio nyie mnaingia bar unamwachia mumeo afungue pochi yake hata kumpa ofa hutoi au kumnunulia nguo mumeo apendeze huwezi.Kipimo cha mwanaume cha kumpata mke mwema ni yule anaeijtoa kwa wajili yako sasa siku sina kazi atanistahi kweli?CHa kushangaza unakuta ana mshahara mzuri lakni hata kuchangia ujenzi au ununuzi wa kiwanja hataki,anataka kuvaa nguo za gharama na magold wkt huo huo mnakaa nyumba ya kupanga ni ajabu sana.Wanawake badilikeni sasa wanaume watunzeni kama watoto wenu, hata mke ambae hana kazi lakini kwa mwerevu atajitahidi kusave hela anayopewa ya matumizi na kumsuprise mumewe kwa zawadi..

Sawa tumekusikia tutabadilika, sasa na ambao washajenga majumba na kila kitu na bado mume anapesa sana na wewe una kikazi cha mshahara tu bado utachangia tu? kununua zawadi na vitu vingine unafanya ,ila kwa mfano linapokuja swala mwenzio anakwambia ananunua kiwanja mikocheni kwa pesa nyingi ,utapeleka kimshahara chako ili na wewe uonekane umechangia? Mimi bwana nitabadilika ila kwa vitu vidogovidogo vingine namwachia tu bwana. Nafikiri wengine wanapenda kufanya kwa ajili ya family zao tu
 
Ni vizuri ndio ila sio ndio niwe nakutegemea saaana.
Hata kama nafanya kazi, inawezekana unanizidi kipato. Pia ukinipa huduma ndogo ndogo hizo nafarijika kuwa bado unanijali.
 
ndiyo ni haki yake kabisa kumuhudumia vitu kama mavazi salon na mengine pia kazi yake isyo sababu ya ww kutokumuhudumia huyo ni mkeo ni jukumu lako kumtunza,umeuliza swali zuri sana hope litachangiwa vilivyo mana mnajisahau sana mnapokutana na mwanamke mwenye kazi sometime hata hayo ya msingi hamyafanyi unamuachia kila kitu.

sasa na zile anazopata zinaenda wapi kama kila kitu uhudumie mwanaume?

 
sasa na zile anazopata zinaenda wapi kama kila kitu uhudumie mwanaume?

Umegusia kitu cha muhimu sana. Kama huyu mwanamke ana kazi yake inayompatia mshahara mzuri tu na bado tena hata hela ya saluni anategemea kwa mumewe na pengine mumewe ana kipato cha kawaida, mimi naona huo kama ni ubinafsi. Na mara nyingi hili jambo limeleta kutoelewana zaidi hasa kwa upande wa ndugu wa mwanaume. Mfano, unakuta mshahara wa mwanamke kazi yake ni kusaidia upande wa kwake (ndugu zake na kuendeleza kwako), kwa hali kama hiyo upande wa mwanaume mara nyingi inakuwa ni issue kuendeleza/kusaidia upande wa ndugu zake, sababu kubwa ni kuwa hela inayopatikana inakuwa haitoshi (inatumika mpaka kufanya vitu vingine ambavyo hata mkewe anaweza kuvimudu mfano wa hili la salun). Ikiwa tu mwanamke mpaka kiasi kidogo cha hela ya saloon anakomaa umpe (na ukizingatia ana mshahara wake) basi sidhani kwa mwanamke kama huyo atakuelewa incase umwambie mchangie suala la kodi, ada, etc. Lakini mwisho wa siku kinachohitajika ni maelewano jinsi ya kujipanga kwa suala zima la huduma kwa ujumla, lakini pia sio vibaya kwa siku moja moja kwa mwanaume kumpatia hela ya saluni mkewe bila kujali kama ana mshahara wake kwani hii inaongeza upendo na hali ya kujali zaidi.
Maada kama hii nakumbuka ilikuwa inaibuka sana wakati tupo vyuoni, mfano. mnapewa bumu sawa na mdada, ila cha ajabu hela yote ya msosi, nauli na saluni anakupiga mzinga kwa kwenda mbele na hapo huna kazi nyingine zaidi ya hilo bumu.
Nawasilisha.
 
Mshahara ukija nyumban mwenye wake hayupo, mishahara yote inawekwa mezan afu mnapanga matumizi, ila cönsider mwanamke ni delicate anahitaji pesa zaidi ya mwanamume. Ndo maisha ya kisasa vinginevyo matatizo na ubinafsi vitatawala. Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom