Ni sahihi kuoa au kuolewa na aliyekuwa mpenzi wa rafikiyo?

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,764
895
Wana JF.
Maisha ni kitendawili usemi huu una maana kubwa sana, kwa nini?

Hakuna binadamu ambaye anajua litakalotokea kesho. Lakini katika maisha yetu ya kila siku hata katika uhusiano ya kindugu, kirafiki na kimapenzi.

Mengi hutokea yanayohusisha marafiki au ndugu, kumekuwa na kitendawili kikubwa kuhusiana na urafiki na uhusiano, swali hivi ni sahihi kutaka kuoa au kuolewa na aliyekuwa mpenzi wa rafiki yako?
wadau tujadili
 
Mi naona km hao 2 wamependana hakuna shaka, ila kuna uwezekano ule urafik ukafa, uwe tayar kumpoteza rafik upate mpenzi.
 
Hakuna ubaya endapo uhusiano wao uliisha kitambo,na uwepo wa uhakika wa kutokuwepo kwa mahusiano baina yao.
 
Siyo sahihi, hata kidogo! rafikiyo ataamini vipi kama hamkuwa na uhusiano kabla ambao umesababisha yeye na mpenziwe waachane mpaka wewe ukapata hiyo nafasi? Mi naona ni kama unafiki fulani vile ...
Tafuta mwingine Bwana, acha kulala alipolala rafikiyo, ni sawa na kumvua nguo kwa makusudi!
 
Hii mie naona noma hasa kama hao marafiki bado wana urafiki na huyo anayetaka kuoa/kuolewa ndiye aliyehusika na kuvunja uhusiano wa kimapenzi wa rafikiye.

Last edited by a moderator:
nadhani inategemea walikua pamoja kivipi na walikaa muda gani, tangu viishe ni muda gani, uhusiano wao leo ni upi etc.
Kumuoa sio kosa (sababu refiki yako alishindwa anyway) ila unataka uishi na mpenzi wako kwa amani. Rafiki pia muhimu ila sio kama mke wako. urfiki unakuja na unaisha.
Sasa fikiria kama mke wako bado anahisia kwa rafiki, au rafiki anampenda mke wako, itakuwaje? haya, fikiria kama hawasikilizani, inakuwaje? au wanasikilizana ila hawapo kabisa comfortable kama wakiwa pamoja, inakuwaje? situation ingine ni kama mke wako aliwahi kutoa mimba ya rafiki yako, rafiki yako atawaonaje watoto wako atakapo kua anakuja kukutembelea?
Kuna maswali mengi hapo utakosa jibu, kwa hiyo kama unaweza jitafutie wakwako, ila kama penzi lenu lina nguvu sana basi mtashinda hayo yote na kuishi kwa furaha na amani.
 
Friendship is overrated. Rafiki ni mtu baki tu, watu wawili wakipendana na wakaamua kuoana,poa tu.
"kama mapenzi yaua, kufa sioni muhani"
 
nadhani inategemea walikua pamoja kivipi na walikaa muda gani, tangu viishe ni muda gani, uhusiano wao leo ni upi etc.
Kumuoa sio kosa (sababu refiki yako alishindwa anyway) ila unataka uishi na mpenzi wako kwa amani. Rafiki pia muhimu ila sio kama mke wako. urfiki unakuja na unaisha.
Sasa fikiria kama mke wako bado anahisia kwa rafiki, au rafiki anampenda mke wako, itakuwaje? haya, fikiria kama hawasikilizani, inakuwaje? au wanasikilizana ila hawapo kabisa comfortable kama wakiwa pamoja, inakuwaje? situation ingine ni kama mke wako aliwahi kutoa mimba ya rafiki yako, rafiki yako atawaonaje watoto wako atakapo kua anakuja kukutembelea?
Kuna maswali mengi hapo utakosa jibu, kwa hiyo kama unaweza jitafutie wakwako, ila kama penzi lenu lina nguvu sana basi mtashinda hayo yote na kuishi kwa furaha na amani.

Hapo kwenye red hapo ndo mtihani kwangu. nahisi kama rafiki kakutembelea hasikukute then wife anakueleza jamaa amekusubiri sana tumekula, ameondoka kasema atakuja baadae. siwezi kuwa na amani ingawa ni ngumu kulalamika ikwa ulioa ukielewa uhusiano waliokuwa nao zamani.
 
Ndio hivo. na nimesema kabisa, kama mtu anaona atakosa amani kwa vitu vidogo vidogo kama hivo bora aache. Kumbuka rafiki ni ndugu, kuna wakati upo safarini na rafiki anakusaidia vitu vidogo vidogo kama kupeleka gari garage,a u kusaidia kuna mtu kaumwa ghafla nyumbani, tena usiku etc. sasa kama humuamini rafiki yako ni bora uachane nae kama rafiki au usmuoe huyo mwanamke. itakua vigumu sana kuendelea nao wote.
 
Mkuu RR, lazima amani ikosekane na roho kuwa juu......kuna wanaume/wanawake wengi tu ambao wanaweza kuchukua nafasi hiyo bila matatizo yoyote, hivyo ni bora tu kuipotezea hali kama hii.
 
I don't see nothing wrong
Well, the "wrong" is not a moral wrong, it is the risk of their personnal history interfering with your marriage. I propose he ends of one of the two relations (preferably the friendship) and saves the other...
 
Wanawake/wanaume wote hawa mpaka umuoe shemejio kisa? Nadhani sio busara kufanya hivyo.
 
Ni sahihi ingawa kuna changamoto za ziada zinaweza kujitokeza ukilinganisha na kuoa/olewa na mtu mwingine baki.
 
mmmmmmmmmmmmhh, hadi akuoe ina maana kipindi yupo na rafiki yako ulikuwa unammezea mate au?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom