Ni sahihi kublokiana kwenye mitandao ya kijamii kwa mume na mke?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kwa wale ambao wameingia kwenye mahusiano hasa ya mke na mume au ya mapenzi inapendekezwa mkiishaingia rasimi inakupasa kublokiana ili msiwe mnachunguliana leo umepost nini,status,na umekoment nini kwa followers wako au kuacha mitandao ya kijamii

Kuna mgogoro umeibuka hapa kwa jirani baada ya mwanaume kuona comments za mke wake wakiitana na mwanaume mmoja Facebook kuwa "My,mke,dear" na mwanamke amekuwa akireply" My,mume love "

Mwanaume alivyohitaji kujua kulikoni mwanamke akasema huyo kaka wa Fb alimuomba wawe wanaitana kama watu walio kwenye mahusiano ili mpenzi wake walioachana hivi karibuni aumie

Mwanaume bado anadai hajaridhikana majibu ya mke wake

Je ni sahihi kuendelea kutumia mitandao ya kijamii mnapokuwa kwenye ndoa kama jibu ni ndiyo,je ni sahihi kuendelea kuwa friends au follower kwa mwenzako au kumblock ili kuzuia kuchunguzana umekuwa online, umekoment nini au walikoment nini kwenye post zako ?
 
ndoa inafungwa kwa sala na toba za mizimu, lakini inakuja kuvunjika kwa meseji moja tu ya simu

ndoanoo
 
Ukosefu wa kazi huo! Mwanaume aliye busy hawezi kuwa na mda wa kupekua account za mitandao ya kijamii ya mkewe and vice versa.
Matatizo mengine yanaepukika kwa kuchagua kutofuatiliana tu.
...Mimi Kuna mtu alihack kabisa....Yaaani
.sijawai shangazwa alafu anakuja kukutuhumu kwa Mambo ya 2018...eti kwanini ulifanya hili na lile.

Watu wanakosaga kazi Wallahi ...
 
Ukosefu wa kazi huo! Mwanaume aliye busy hawezi kuwa na mda wa kupekua account za mitandao ya kijamii ya mkewe and vice versa.
Matatizo mengine yanaepukika kwa kuchagua kutofuatiliana tu.
Sio lazima kupekua mfano mnapokuwa friends fb automatically comments huwa zinaonekana zenyewe,ili usione comments za mwenzako ni sahihi kublokiana ?
 
Anyway hii mitandao ilikuja wakati tuko ndoani. Sina urafiki naye kwenye mitandani. Si mflow wala hani folow popote pale.


Kwa nini tuwasiliane kupitia mtandao wakati tuko pamoja zaidi ya masaa 15 kwa siku?
 
Ukosefu wa kazi huo! Mwanaume aliye busy hawezi kuwa na mda wa kupekua account za mitandao ya kijamii ya mkewe and vice versa.
Matatizo mengine yanaepukika kwa kuchagua kutofuatiliana tu.

True na pia kuwepo na mipaka baina ya mwanaume na mwanamke hasa pale mtu unapojua wewe ni mke/mume wa mtu usipende kujiweka ktk matatizo ambayo yatapelekea uvunjifu wa uaminifu kama hvo kuneng’eneka na watu ambao wanaweza kuharibu mahusiano hata ndoa yako
 
Ila inabid ifike mahali kama mitandao ya kijamii ipunguzwe hasa pale mtu anapofikia level/stage flan ya maisha as long as haikupunguzii chochote ni bora kuachana nayo ili kuepusha migogoro ya kipuuzi
 
Imebid nicheke tu. Ila mimi naamini siku zote, nyie wanawake mnaangaliaga na watu wa kuwajibu ujinga.
 
Back
Top Bottom