Ni roho mbaya au nini??

Esperance

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
364
84
Hamjambo wanajamvi wote pole na mgao. Mwenzen kuna tatizo lanikwaza na kunikondesha kwa kweli. Niko kwenye mahusiano huu mwezi wa nne. Katika maongez na huyo mwenzangu akaniambia mambo yake mbalimbali ya maendeleo na mimi nikamwambia nna kakibanda kangu japo cjakamalizia basi imekuwa nongwa anaiponda mbaya, mara wadogo zangu wanafanya Masters, mara nataka kununua coaster, mara nyumba yangu ni m70. In short ka amani kamepotea kimtindo, nna vijimiradi anaviponda pia .sasa nashindwa kuelewa tatizo ni nini?hanijali tena kama zamani. Msaada wa mawazo ndgu zanguni. Asanteni
 
Hapo wivu zaidi unahusu!Inasikitisha kwasababu huyo mtu wako alitakiwa kufurahia jitihada zako!Nwyz umwambie anavyofanya sio vizuri!
 
Acha na huyo mkaka mapema kabla mambo hayajawa makubwa. Mmmhh duniani kuna mambo! Pole mwaya!!
 
Hamjambo wanajamvi wote pole na mgao. Mwenzen kuna tatizo lanikwaza na kunikondesha kwa kweli. Niko kwenye mahusiano huu mwezi wa nne. Katika maongez na huyo mwenzangu akaniambia mambo yake mbalimbali ya maendeleo na mimi nikamwambia nna kakibanda kangu japo cjakamalizia basi imekuwa nongwa anaiponda mbaya, mara wadogo zangu wanafanya Masters, mara nataka kununua coaster, mara nyumba yangu ni m70. In short ka amani kamepotea kimtindo, nna vijimiradi anaviponda pia .sasa nashindwa kuelewa tatizo ni nini?hanijali tena kama zamani. Msaada wa mawazo ndgu zanguni. Asanteni

hakujali tena kama zamani!!!?
Duh sijui zamani inaanzaga lini na wewe umesema mna miezi minne tu.
Ni muda mfupi sana kuanza kumchoka mwenzio ila ni muda mrefu na unaotosha kujua tabia za mwenzio.
Mambo madogo madogo kama hayo rekebisha mapema kabla hayajaota mizizi.
Kama una malengo nae jioneshe wazi wewe ni mtu wa aina gani ikiwa ni pamoja na unayoyapenda na usiyoyapenda.
Usipende kuonesha tabasamu la usoni wakati moyo unasononeka.
 
nahisi mmekutana washindani wawili....
...nadhani hata wewe una ushindani wa kichini chini sioni sababu mtu ajitambie mali alizonazo halafu wewe usononeke??!..mnh:A S 13::A S 13:
...atakuwa muhaya tu huyo mzoee hivyo hivyo..
 
Mueleze kwamba hupendi hiyo tabia, Hujatwambia jinsia yako, ila wanaume wengi huwa wanastukia msichana akiwa na maendeleo hufikiri labda kahongwa au ana tabia mbaya hata kama umejitutumua mwenyewe mpaka umejenga, ila kama ww ni mwanaume labda ulitamka kwa kujigamba si unajua zile wale mabishoo wanavyojifagilia? mambo mengiii ooo nina account uswizi, when i was kibaaaaaao, huwa inakera sasa labda tuambie uli ipresent vipi hii issue yako kwa mwenzako, wewe me ao ke
 
Binafsi naogopa sana mapenzi yanaypjengwa kwenye msingi wa vitu vinavyoonekana zaidi kwa macho!! Siku vikiisha ina maana na mapenzi yamekwisha?? Halafu hapo tayari naona kuna roho ya CHANGU!!! Hiki changu, gari langu, nyumba yangu.......changu. Hii lugha naona ni mbaya sana kwenye mahusiano yawe ya muda mfupi na mbaya kabisa yale ya muda mrefu.

Kwa hiyo mi nashauri mpime mioyoni yenu, mapenzi yenu yamejengwa katika msingi gani?? Upendo wa kwli....!!! Fedha na mali......, uzuri na umaarufu......au na nini???? Baada ya kulijua hilo fanya uamuzi sahihi.
 
Roselyn dia me nilimwambia kwa nia njema ili baadae acje sema nilimficha, nasononeka anavyoniponda. Mmh kweli ni mixture ya kihaya.
 
Mueleze kwamba hupendi hiyo tabia, Hujatwambia jinsia yako, ila wanaume wengi huwa wanastukia msichana akiwa na maendeleo hufikiri labda kahongwa au ana tabia mbaya hata kama umejitutumua mwenyewe mpaka umejenga, ila kama ww ni mwanaume labda ulitamka kwa kujigamba si unajua zile wale mabishoo wanavyojifagilia? mambo mengiii ooo nina account uswizi, when i was kibaaaaaao, huwa inakera sasa labda tuambie uli ipresent vipi hii issue yako kwa mwenzako, wewe me ao ke

Mimi ni ke, nilipresent kwa nia njema tu katika kuwekana wazi kama yeye alivyoanza kuniambia, sasa tatizo mwenzangu kila mara nyumba yako imekosewa ,umetumia cheap labour na sio kwa kukosoa kikawaida hapana yani anadharau kabisa, me ni nna kabachelor kamoja basi utasikia aah me mdogo wangu anafanya masters, ili mradi ni kukicritise tu.
 
Binafsi naogopa sana mapenzi yanaypjengwa kwenye msingi wa vitu vinavyoonekana zaidi kwa macho!! Siku vikiisha ina maana na mapenzi yamekwisha?? Halafu hapo tayari naona kuna roho ya CHANGU!!! Hiki changu, gari langu, nyumba yangu.......changu. Hii lugha naona ni mbaya sana kwenye mahusiano yawe ya muda mfupi na mbaya kabisa yale ya muda mrefu.

Kwa hiyo mi nashauri mpime mioyoni yenu, mapenzi yenu yamejengwa katika msingi gani?? Upendo wa kwli....!!! Fedha na mali......, uzuri na umaarufu......au na nini???? Baada ya kulijua hilo fanya uamuzi sahihi.

Nakushukuru sana LD.
 
Ahsante sana LD kwa mchango wako mzuri sana.
 
nahisi mmekutana washindani wawili....
...nadhani hata wewe una ushindani wa kichini chini sioni sababu mtu ajitambie mali alizonazo halafu wewe usononeke??!..mnh:A S 13::A S 13:
...atakuwa muhaya tu huyo mzoee hivyo hivyo..
Wewe roselyne weweee!
Utagombana na Rutashubanyuma sasa hivi!...Atakupandishia thread, huogopi?
 
Hamjambo wanajamvi wote pole na mgao. Mwenzen kuna tatizo lanikwaza na kunikondesha kwa kweli. Niko kwenye mahusiano huu mwezi wa nne. Katika maongez na huyo mwenzangu akaniambia mambo yake mbalimbali ya maendeleo na mimi nikamwambia nna kakibanda kangu japo cjakamalizia basi imekuwa nongwa anaiponda mbaya, mara wadogo zangu wanafanya Masters, mara nataka kununua coaster, mara nyumba yangu ni m70. In short ka amani kamepotea kimtindo, nna vijimiradi anaviponda pia .sasa nashindwa kuelewa tatizo ni nini?hanijali tena kama zamani. Msaada wa mawazo ndgu zanguni. Asanteni

Ya nini kuendelea kupoteza muda wako kwa mtu asiyekujali!? Dalili za mvua ni mawingu.
 
naona huyo jamaa hajiamini hata ndio maana
anajaribu kukufanya ujisikie mnyonge katika jitihada zako
za maendeleo. hakufai huyoo oohooo!!
 
jamani miezi 4 huyo kijana anakufanyia hivyo?kama unampenda jaribu kumuelewesha,maybe ni tabia yake hiyo,wala hajui kama anakuumiza.ila ukiona habadiliki tafuta ustaarabu wako mapeeeema.kwani huko mbeleni yanaweza yakawa mengine machungu zaidi.badala ya kuku support yeye anakukandamiza,mbona hajui kumpenda mtu?
 
jamani umenikumbusha rafiki yangu mmoja nshomile alikuwa hapendi kuona nina kitu kizuri,kila kitu changu lazima akikosoe,ila anchofanya yeye ndio kizuri na cha quality, mbaya zaidi alikuwa hadi idea zangu za maendeleo anazipinga, utasikia hicho kitu huwezi kufanya,hautafanikiwa yaani alikuwa ni wa kunikatisha tamaa kwa kila saa! kwa kifupi nakushauri usipoteze muda na mtu ambaye hapendi kukubali jitahada zako,anachokifanya ni kukufanya wewe uwe inferior kwake,uwe ni mtu wa kuamini hakuna kitu unachoweza kufanya hapa duniani, kwani nyumba zote zilizojengwa huko mitaani zinafanana? kila mtu si anajenga nyumba inayolingana na uwezo wake? sasa kama yeye anaweza kujenga ya m80 na wewe huna so wat? kwa hiyo nyumba yako itakuwa choo watu hawawezi kuishi ndani ila yake ndio yenye hadhi ya watu kkuishi? ni wasichana wangapi leo wamefikiria kuanza kujenga kwa kile kidogo wanachopata? usimpe nafasi mtu wa hivyo sepa bila kugeuka nyuma, atakufanya ushinde kuachieve ndoto zako za maendeleo bure!
 
Back
Top Bottom