Ni rahisi kuwapata wengi kama Magufuli lakini haitatokea kumpata kama Nyerere ndani ya CCM.

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,504
2,000
kusema ukweli ni jambo rahisi kuwapata watu kama Magufuli ndani ya chama cha mapinduzi kwa sasa na hata miaka ijayo, lakini tokea Uhuru imekuwa ngumu kumpata aliye kama Nyerere kutoka chama cha mapinduzi na tutaendelea kuwapata watu km magu lakini haitotokea kumpata kiongozi kama Nyerere ndani ya ccm

nawasilisha
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,037
2,000
IMG-20170416-WA0006.jpg

Kama ni huyu ndio Nyerere unae mzungimzia.....
Basi naomba niishie tu hapa
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,889
2,000
kusema ukweli ni jambo rahisi kuwapata watu kama Magufuli ndani ya chama cha mapinduzi kwa sasa na hata miaka ijayo, lakini tokea Uhuru imekuwa ngumu kumpata aliye kama Nyerere kutoka chama cha mapinduzi na tutaendelea kuwapata watu km magu lakini haitotokea kumpata kiongozi kama Nyerere ndani ya ccm

nawasilisha
Kila mtu aliumbwa unique kabisa/ Yaani TOFAUTI na mwingine kabisa.
Hata siku moja Magufuli hawezi kuwa
kama Nyerere. HILO kwanza TUSAHAU.
Na Nyerere angekuwa bado yu HAI asingeweza kuwa kama Magufuli hata CHEMBE.

NYAKATI na MAJIRA yamebadilika na yanahitaji KWENDA na NYAKATI.
Mfano mzuri ni wa nchi ya CHINA.
Rais wa SASA na mkuu wa chama cha KIKOMINISTI cha CHINA HAWEZI kuwa kama MAO Tsetung.
HAIWEZEKANI.
China kama NCHI na CHAMA chake tawala cha nchi hiyo kumekuwa na MABADILIKO MAKUBWA kabisa TOFAUTI na ilivyokuwa wakati wa MAO na MITAZAMO ya MAO ilivyokuwaga.

Hii ni kusema kama Mao mwanzilishi wa taifa hilo angefufuka na akute CHAMA CHAKE na NCHI yake ILIVYOBADILIKA na mfano CHAMA KILIPOYAACHA mavazi ya kaunda za MAO na watu WAKARUHUSIWA kuvaa SUTI hata viongozi wa chama, hili tu LINGEMSHTUA sana Mao na kumfanya ARUDI KABURINI!!!!!!!

Nisemavyo ni kuwa TUSIMLINGANISHE Magufuli na Nyerere wala kule TULIKOTOKA bali TUANGALIE kule TUENDAKO.

Hii pia yakiwemo MABADILIKO yanayoambatana na Present TIME, Current GEOPOLITICS nchi za dunia nazo zimebadilika nk.

Nyerere nae alifanya mahali alipoweza CHAMANI kulingana na MTAZAMO wake na NYAKATI zake. Hilo kwanza lazima tulikubali.

Na hivyo approach HAZITAFANANA hata CHAMANI CCM. Mfumo wa zamani might not be applicable kwa nyakati za SASA.
Hivyo mabadiliko HAYAEPUKIKI.
Hivyo pia si RAHISI kumpata mtu kama Magufuli
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,507
2,000
Acha kumchafua mwalimu na huyu mwizi, muongo na fisadi! Mwalimu hakuibia Watanzania hata senti moja, mwalimu hakutumia hata senti moja bila idhini ya Bunge

Huyu kahusika na kukwapua nyumba za Serikali na nyingine kuhonga, huyu kanunua kivuko uozo kwa bilioni 8 kikafanya kazi kwa wiki moja tu, huyu katumia $485 millions bila idhini ya Bunge na huyu kalidanganya Bunge kuhusu upotevu wa zaidi ya shilingi 200 bilioni za walipa kodi. Acha kabisa kumchafua Mwalimu.

Afadhali wapo Kama Magufuli!Maana wana tabia kama za Nyerere! Hata Nyerere Mwenyewe alikiri Rais bora anapatikana ndani ya CCM
 
Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,650
2,000
View attachment 522159
Kama ni huyu ndio Nyerere unae mzungimzia.....
Basi naomba niishie tu hapa
Acha ungese wewe, kawadanganye wanawake wenzako huko! Unaweza kutuambia kwa uhakika hao wa kwenye hiyo picha ni akina nani? Ebu nitumie picha yako moja tu ambayo sura yako inaonekana vzr afu uone nitakachokufanyia! Nyerere hakuwahi kuwa, na hawekuwa mtu wa kumchezea hivyo! Mbaf zako!
 
Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,650
2,000
Acha kumchafua mwalimu na huyu mwizi, muongo na fisadi! Mwalimu hakuibia Watanzania hata senti moja, mwalimu hakutumia hata senti moja bila idhini ya Bunge

Huyu kahusika na kukwapua nyumba za Serikali na nyingine kuhonga, huyu kanunua kivuko uozo kwa bilioni 8 kikafanya kazi kwa wiki moja tu, huyu katumia $485 millions bila idhini ya Bunge na huyu kalidanganya Bunge kuhusu upotevu wa zaidi ya shilingi 200 bilioni za walipa kodi. Acha kabisa kumchafua Mwalimu.
Mkuu BAK mi na wewe tunaheshimiana sana ingawa hatufahamiani. Nina "reservations" ktk baadhi ya tuhuma juu ya bwana Pombe ambazo NAFAHAMU zilipikwa na baadhi ya maadui wake wa kisiasa wakati uleee!

Lakini nakubaliana na wewe kwa asilimia zote unapopinga kumfananisha Magufuli na Baba wa Taifa. Ingawa baabadhi ya sera alizozisimamia Baba wa Taifa hazikufanikiwa lakini "credibility" yake inasimama ktk ukweli kwamba:
- Alikuwa na dira
- Aliishi kwa kiasi mno (alikufa maskini na hadi sasa familia yake ni maskini)
- Alikuwa mwadilifu kabisa
- Alikuwa Mcha Mungu

Washabiki wa Magufuli wanaweza kuniambia dira yake ni nini? Wanaweza kuthibitisha ukweli wa maisha yake binafsi ukoje? Na uadilifu wake? Na ucha Mungu wake? Kwangu mimi maswali haya yanaweza kupata majibu sahihi BAADA ya kipindi cha utawala wa Pombe kuisha.

Kwa sasa kumlinganisha Magufuli na Mwalimu ni ubadhilifu wa hoja.
 
Kwani kuna ubaya gani kupigwa busu na wajukuu zake....
Ama wapi nimetukana hata unitukane Mkuu.....
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,507
2,000
Shukrani sana Mkuu. Mkuu kama tuhuma dhidi yake ambazo baadhi zilikuwemo mpaka kwenye ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali zilipikwa na maadui wake kipi kinachomshinda kujitetea na kuja na ushahidi uliojitosheleza kuonyesha kwamba tuhuma hizo ni uongo Mkuu!?

Hasa tuhuma hizi tatu nyumba za Serikali, upotevu wa mabilioni ya ujenzi na ununuzi wa kivuko kibovu. Sasa hivi kaibuka na hili sakata lingine la kutumia $485 millions ambazo hazikuidhinishwa na Bunge na pia hakufuata utaratibu wa manunuzi ya Serikali. Pia kuna kuchota pesa kupeleka chato bila idhini ya Bunge na hili la kuhamisha pesa kutoka Wizara A kwenda Wizara B bila idhini ya Bunge.

Mkuu BAK mi na wewe tunaheshimiana sana ingawa hatufahamiani. Nina "reservations" ktk baadhi ya tuhuma juu ya bwana Pombe ambazo NAFAHAMU zilipikwa na baadhi ya maadui wake wa kisiasa wakati uleee!

Lakini nakubaliana na wewe kwa asilimia zote unapopinga kumfananisha Magufuli na Baba wa Taifa. Ingawa baabadhi ya sera alizozisimamia Baba wa Taifa hazikufanikiwa lakini "credibility" yake inasimama ktk ukweli kwamba:
- Alikuwa na dira
- Aliishi kwa kiasi mno (alikufa maskini na hadi sasa familia yake ni maskini)
- Alikuwa mwadilifu kabisa
- Alikuwa Mcha Mungu

Washabiki wa Magufuli wanaweza kuniambia dira yake ni nini? Wanaweza kuthibitisha ukweli wa maisha yake binafsi ukoje? Na uadilifu wake? Na ucha Mungu wake? Kwangu mimi maswali haya yanaweza kupata majibu sahihi BAADA ya kipindi cha utawala wa Pombe kuisha.

Kwa sasa kumlinganisha Magufuli na Mwalimu ni ubadhilifu wa hoja.
 
Nyetk

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
1,650
2,000
Kwani kuna ubaya gani kupigwa busu na wajukuu zake....
Ama wapi nimetukana hata unitukane Mkuu.....
Maneno uliyoweka kwenye picha uliyobandika vilikuwa na mantiki ya kumdhalilisha mtu ninayemheshimu sana, ndiyo maana nilipata moto. Mshukuru kichaa man amekusaidia maelezo mazuri ya picha hiyo. Lengo lako halikuwa zuri kabisa.
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
7,897
2,000
Acha kumchafua mwalimu na huyu mwizi, muongo na fisadi! Mwalimu hakuibia Watanzania hata senti moja, mwalimu hakutumia hata senti moja bila idhini ya Bunge

Huyu kahusika na kukwapua nyumba za Serikali na nyingine kuhonga, huyu kanunua kivuko uozo kwa bilioni 8 kikafanya kazi kwa wiki moja tu, huyu katumia $485 millions bila idhini ya Bunge na huyu kalidanganya Bunge kuhusu upotevu wa zaidi ya shilingi 200 bilioni za walipa kodi. Acha kabisa kumchafua Mwalimu.
Swali rahisi sana kwako BAK. Lowasa ni mwizi, au siyo mwizi?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom