Ni pepo au nyota?

Mimi ninatabia ya kuwaambia client wangu hasa vijana wa kiume, nimekutibu na nikakupa masharti ya kupunguza au kuacha zinaa ukanigomea nakuandikia matibabu ya ghali ili ujutie kosa lako kwa gharama kubwa.....

Wazee matibabu ya zinaa ni gharama wakuu tupunguze zinaa wakuu
 
Mimi ninatabia ya kuwaambia client wangu hasa vijana wa kiume, nimekutibu na nikakupa masharti ya kupunguza au kuacha zinaa ukanigomea nakuandikia matibabu ya ghali ili ujutie kosa lako kwa gharama kubwa.....

Wazee matibabu ya zinaa ni gharama wakuu tupunguze zinaa wakuu
 
Hilo ni pepo! Mungu hapendi zinaa! Hiyo roho ya zinaa haijatoka kwa Mungu na kama haijatoka kwa Mungu bila shaka imetoka kwa shetani ndiyo maana katika swali ulilouliza (ni pepo au nyota?) binafsi naona jibu ni pepo!

Shetani atatumia njia nyingi kukuingiza mitegoni na majaribuni na ukishaingia na kupata matatizo atakuacha na kamwe hatakupa msaada wa kukutoa katika matatizo hayo.

Nakushauri kimbia kama maandiko yanavyosema "IKIMBIENI ZINAA". Kuna stori katika Biblia inayomhusu kijana YUSUFU mtoto wa YAKOBO aliyeuzwa Misri. Alikumbana na hicho unachokiita nyota! Alipendwa na mke wa bosi wake. Hata hivyo Yusufu alipewa akili na Mungu ya kujua na kukimbia ujanja wa shetani. Yusufu alikimbia.

Kama Yusufu angechekelea kula tunda la mke wa bosi wake angepoteza urafiki na Mungu na ndoto zake zingezimika! Kwakuwa alitii amri ya Mungu ndoto ya kuwa waziri mkuu ilitimia!

Kuna vitu shetani ameona kwako ambavyo Mungu amekuandalia na anataka akukwamishe usivipate kwa kukugombanisha na Mungu kupitia dhambi ya uzinzi! Kimbia.
Ushauri murua huu mtumishi wa Mungu Elisha
 
IMG_20200920_174343.jpg

Sio wote ni wawazi kama huyu. Ila hongera kwa kula Minofu mingi ya nyama
 
Mimi ninatabia ya kuwaambia client wangu hasa vijana wa kiume, nimekutibu na nikakupa masharti ya kupunguza au kuacha zinaa ukanigomea nakuandikia matibabu ya ghali ili ujutie kosa lako kwa gharama kubwa.....

Wazee matibabu ya zinaa ni gharama wakuu tupunguze zinaa wakuu
Sawa daktari. Watu wengine tuwasidie hata kwa njia zinazoonekana za kibabe kwa ajili ya kuokoa maisha yao.
 
Wakuu naomba maoni au ushauri au Kama na wewe una hii Hali unaweza kujazia, sijajua Hadi Sasa Ni kwa nini kila mwanamke naemtongoza anakubali!!!

Hii Hali imekua ikinistaajabisha Sana sio mimi tu Hadi watu wangu wa karibu huniambia we una urimbo au ulifanyiwa dawa ya wananwake.

Ni Mara chache Sana mwanamke nkimtokea atakataa sijui huwa Ni nn kinasababisha wanavutika kwangu!! Mfano nkienda sehemu nkakuta wanawake na wanaume mfano wako mezani na mimi nkakaa kwenye hiyo meza utaona wanawake wananikazia macho Sana na hata nkiongea wananipa usikiivu mkubwa kosa niombe namba ya simu!!

Hamna nguvu ya kukataa hata Kama amekaa na mume wake atafanya awezalo Hadi ahakikishe inanifikia!!majuzi hapa Kuna sehem nilienda (kwa shuguli zangu) kukawa na watu wa TRA (2) wamekuja kufanya ukaguzi maeneo hayo !! Walikua wawili mwanamke na mwanaume jioni mwenyeji wng akanikaribisha chakula mezani tulikua wanaume 4 na huyo mwanamke mmoja

Wakati tukila huyo mwanamke akawa ananisogezea nyama (kuku) upande wangu yaani anachagua minofu mizuri ananiwekea upande wangu ,kumbuka hatujawahi kuonana Wala hatujuani na kufika hapo zaidi ya Salam nlikua sijaongea kitu chochote!!! Visa Ni vingi vya namna hiyo siwezi kuviandika vyote Ila hii Hali inanistajaabisha na naona Kuna kitu si Cha kawaida ndani yangu
Naomba kwasilisha na kukaribisha maoni kwa anayeweza kujua hii Hali ikoje na inasababishwa na nini
Hilo ni PEPO!👹👹👹
 
Nimesoma comments zote ,imekosekana comment ya kuulizwa umri wako.

Una miaka mingapi dogo??
 
Back
Top Bottom