Kama wa kike tafuta kazi ya u bar maid. Unaingia saa 12 mpaka saa 6 usiku.
Kama ni pisikali utapata hela za tipu za walevi ila kama una sura ya baba jitahidi uwe na kauli nzuri ili walevi wakuamini uwabambikie bili.
Kama dume nunua kapu na rangi za kucha ikifika jioni unazunguka uswahili upake rangi na kusugua miguu mademu.
Kama muongeaji mzuri basi unaweza kuwa dalali wa vyumba pia ule pesa za kodi za mwezi mmoja pale utakapowapatia vyumba wateja.
Na kama una kipaji cha kusifia na kujitoa ufahamu then kuwa chawa wa tajiri mmoja. Ukitoka kazini wewe una kazi ya kumganda tajiri na kumjaza misifa.
Options za kutosha hizo, shindwa wewe sasa.