Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Ngoja tupekue na upande wetu wavaa vipedo na yeboyebo kama kweli wanasema hatupendi Elimu bali tunapenda Ilimu Akhera.
 
Anajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.

Siyo lazima wawe walikuwa wanafahamu! Hata hivi sasa siyo wote waliofahamu kuwa kuna huyo mtu, hata baada ya taarifa zake kuwekwa kwenye mitandao!
 
Ngoja akitoka hapo tumuulize mwenyewe

Huyo hata kanisani hujitambulisha kwa hivyo vyeo vyake sometime! Huwa wakati mwingine kwenye mahubiri yake anapenda kuelezea historia yake na huko kote alikopitia hadi kufika alipo hivi sasa...huna haja ya kumvizia uchochoroni umuulize!
 
Padre yeyote wa Katoliki ni waelewa sana. Miaka mingi wanayosoma, maadili yao imewafanya waelewe mambo mengi sana.
 
View attachment 2033297
Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!

Credit @malisa_gj
Vatcan ni serikai kamaili yenye majajusi wake na idara ya usalama, wenye utii mkubwa na uwezo wa kuibadilikia hata inchi aliyo zaliwa,ni taasisi tajili yenye kumiliki ardhi na miradi Duniani kote,watu wao wa usalama ni pamoja na hao,kuhakikisha hakuna mali wala fedha na heshima yao inanyakuliwa na mtu yoyote au taifa lolote.

Wasimuamini sana
 
Back
Top Bottom