Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,612
- 12,880
Wakuu wa baraza amani kwenu!
Nimejaribu kujiuliza ni zipi sababu zinazo wafanya viongozi na watumishi wa serikali kusaini mikataba yenye hasara kwa taifa lakini sipati jibu sahihi.Mikataba inayo nyonya taifa na kutuletea umasikini ilihali wawekezaji wakibeba utajiri usiopimika.
Kwenye kutafakari kwangu nimepata hypothesis zifuatazo ambazo pengine mojawapo ama zote zaweza kuwa ni sababu za kusainiwa kwa hii mikataba mibovu.
1.UELEWA MDOGO WA VIONGOZI KIAKILI?:
Kwamba hawa viongozi wanaosaini hii mikataba ni watu mambumbu sana wasiokuwa na uwezo wa kufanya analysis juu ya hii mikataba ili kujua faida na hasara zake.Kwamba hawa viongozi kutokana na kuwa na akili ndogo wanapofushwa kirahisi na wawekezaji na kuingiza nchi kwenye hasara.
2.VIONGOZI WA SERIKALI WANAHONGWA NA WAWEKEZAJI:
Je ni watu ambao wanaulewa mpana wa kujua ubaya na uzuri wa mkataba lakini wanachagua upande wa ubaya baada ya kuhongwa? Yaani ni watu wasio na uzalendo ambao wapo tayari kuuza nchi kwa maslahi binafsi?
3:WANATISHWA NA NCHI WANAKOTOKA WAWEKEZAJI:
Kwamba mataifa ya wawekezaji wanawatisha viongozi wa serikali kuwa wasiposaini hiyo mikataba nchi yetu itaingia kwenye matatizo? kwamba wasiposaini uongozi wao utakuwa mashakani? labda watakata kutupatia misaada, kutuuzia vitu muhimu kama silaha na mahitaji mengine ya tekinolojia? labda ndio sababu inayowafanya viongozi waelewa na wasiohongeka[waadilifu] kusaini mikataba yenye hasara kwetu ili wasi-disturb ukawaida uliopo na uliozoeleka nchini?
Ni vema tukajua sababu ya viongozi kusaini mikata mibovu kwa taifa ili kwa kuwa hili ni tatizo tuweze kulipatia uvumbuzi.Je waku kuna anayejua sababu au mwenye hypothesis nyingine?