Ni nini mtazamo wako wewe mwanandoa katika scenario hii

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
573
140
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni
 
Acha mawazo mgando kama ambavyo umekuja uliza huku ndio unatakiwa kuondoa misianderstarnd zilizopo huo ndio ungwana utamfanya akuone kweli umeziba pengo
 
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni

Hmm...interesting.

Unadhani kaiweka hiyo picha ya marehemu mkewe baada ya mkwazano wenu?

Na je, umekwazika nayo?

Kwenye hiyo akaunti yake picha yako au picha zako wewe na yeye kwa pamoja zipo? Au hata ya wewe peke yako ipo?

Kama hakuna picha yako, je, ishawahi kuwekwa hata mara moja?

Na kama picha yako ishawahi kuwekwa, je, ishawahi kutolewa baada ya kutofautiana kauli?

Wewe kwenye akaunti yako huko fesbuk umeiweka picha yake?

Vyovyote vile, sidhani kama ni jambo maanani la kukupa kiroho dunda.

Nasema hivyo kwa sababu huyo dada hayupo tena hapa duniani kuweza kurudiana au hata kukumbushiana na huyo mumeo.

Naliona kama ni suala dogo.

Ila wewe ndiye unayeijua hali yenu halisi hivyo, kama hiyo picha inakusumbua, njia pekee ya kupata ufumbuzi ni kuongea naye.
 
Asante nyaningabu, ndio kaiweka baada ya mkwaruzano. Hajawi kuweka hapo awali tangu amenioa.

Kinachonikwaza ni kuwa tumetofautiana amekimbilia public, kuna watu watahoji au kutaka kufahamu nini chanzo cha kuweka hiyo picha na ndipo anaweza kuweka mambo ya ndani kwenye public.

Ndio kuna picha zangu za awali wakati wa mwanzoni kabisa za current hazipo, make sio mtu wa social network. Kwangu zake zipo.
 
Kama kwa miaka miwili umeshindwa kumhandle mr vizur hadi amsahau hyo aliyetangulia mbele za haki sasa sisi tukusaidiaje?any way jamaa alikuwa anampenda sana huyo mkwewe wa kwanza ila ndo hvyo tena,so jaribu kuwa karibu naye sana na kumfanya apunguze kumwaza hyo wa kwanza.
 
Suluisha huo ugomvi wenu mamy, inaonekana ameumia mpaka akamkumbuka marehemu.
Usiruhusu hali ya namna hiyo itokee maana next time badala ya kumuwaza marehemu ataanza kuwaza namna ya kupata faraja nyingine, hapo ndo atatafuta wa kuchepukaa nae.

Kaeni chini muongee myamalize, tofauti kwenye ndoa hutokea sana na hutatuliwa na wanandoa wenyewe.....
 
Mara nyingi watu hukumbuka yaliyopita kama ya sasa hayaendi.......ni kumbukumbu tu kama kumbukumbu zingine. Nadhani ujumbe umekufikia hivyo rekebisha sehemu yako kama bado upo.
 
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni
Nenda taratibu! Hiyo haina maana yoyote zaidi ya kuwa amemkumbuka mareheme mke wake! Ujue huyo bwana bado anasimanzi kubwa sana ya kufiwa na mwenza ambaye ameishi na kujaliwa watoto. Halafu ukiongezana hiyo migogoro kama ulivyosema, kwa kweli ni hali ngumu sana anayopitia huyo jamaa. Kwa mtazamo wangu hili si jambo haya. Unawasiwasi na marehemu? Ningemuelewa vibaya kama angeposti picha yamchepuko! Nadhani unayonafasi mkubwa sana kumsaidia huyo bwana na kufanya ndoa yenu kuwa ya furaha.
 
Habari wana jamii, Ni takribani miaka miwili imepita tangu nimeolewa na tuna mtoto mmoja. Mume wangu huyu alifiwa na mke wake wa kwanza miaka mitano iliyopita na akamwachia watoto wawili ambao tunaishi nao pia.

Basi mimi sio mzuri sana na mtembeleaji wa social network sababu ya ubusy wa kazi, lakini leo nikaona ngoja nipite pite walau niperuzi account yangu ya facebook. Mh nikapita pia kwenye account ya hubby nikakuta ameupload picha ya marehemu mke wake waliyopiga wakiwa pamoja katika hug bila kuwa na maelezo yoyote katika hiyo picha. Nimepita kama vile sijaiona na sijamuuliza chochote.

In fact hatuko kwenye condition nzuri make kuna some misunderstanding baina yetu. Ni nini mtazamo wako wewe mwanajamvi? Naomba maoni na mchango wenu. Karibuni

Moja ya matatizo makubwa ya wanandoa kwa sasa ni fesi buku na simu za mkononi.

Picha ilipigwa na ipo kabla hujaolewa kwa hiyo ilikuwepo na isikutie wahka.
 
Asante nyaningabu, ndio kaiweka baada ya mkwaruzano. Hajawi kuweka hapo awali tangu amenioa.

Kinachonikwaza ni kuwa tumetofautiana amekimbilia public, kuna watu watahoji au kutaka kufahamu nini chanzo cha kuweka hiyo picha na ndipo anaweza kuweka mambo ya ndani kwenye public.

Ndio kuna picha zangu za awali wakati wa mwanzoni kabisa za current hazipo, make sio mtu wa social network. Kwangu zake zipo.
Usijali sana. Wanaume hawalii kwa sauti na machozi wanapoona wenzi wao hawawaelewi. Bali hulia kwa hisia kali kama hivi. Jitahidi sana mmalize migogoro yenu. Katika hali ambsyo mume wako anapitia, wewe ndiye mwenyewe nafasi nzuri na mkubwa katika kuanzisha mazungumzo hayo.
 
Pole sana kwa kuumia kihisia japo huna sababu ya kuumia maana huyo ni mumeo, jaribu kuwa tayari kumaliza tofauti zetu haraka iwezekanavyo ili kila mtu abaki na amani, kukosa amani kwa muda flani kwa sababu ya mtu flani inaweza kusababisha mawazo ya mwenzako yaende bali sana kiasi kwamba hata mkijapatana kuna kitu kitakuwa kimepungua katika mahusiano.

Kitu cha msingi kuliko vyote ni kujitahidi kutomuudhi mwenzi wako na ikitokea kuwa tayari kumaliza mapema iwezekanavyo, kamwe usiweke msimamo usio na tija, utaharibu mwishowe utajutia.

Mungu akusaidie ujishushe ili mmalize tofauti zenu ili kurejesha amani ya familia yenu.
 
Ugomvi wa kwenye ndoa au mahusiano hautakiwi kukaa muda mrefu hata kidogo ni vema mkayaongea myamalize msifukie mambo na huwa inasaidia kumpa amani kila mtu hivyo nakushauri Sana mmalize tofauti mumeo Ndio rafiki yako Sababu inaonekana Hana amani wala raha na wewe mpaka kumkumbuka huyo.

Kingine lazima ujue baadhi ya Wanaume au sijui ni wote sio wasemaji ila huwa wanaumia kwa extent kubwa isiyoelezeka na kujua kuwa kaumia yakupasa umfahamu mwenzio.

Mzungumze tofauti zenu hiyo picha facebook haina shida wala ila tu ameonyesha kaumia mpaka kumkumbuka muweke karibu mumeo.
 
Katika vitu nisivyohangaika navyo kwenye ndoa/mahusiano ni:-

1. Mwenza kaweka DP gani Whatsapp
2. Mwenza kapost nini facebook/insta
3. Mwenza kaomba ushauri gani kwenye magroup, JF, FB nk
4. Mwenza kaomba ushauri gani kwa rafiki zake
5. Mwenza kaota ndoto gani juu ya uhusiano/ndoa yetu

Nadhani labda ni kwa sababu mimi ni old school, nina prefer kuzungumza ana kwa ana kuliko kupitia kwenye public, misuguano kwenye mahusiano haiepikiki, ila mkianza kuipeleka kwenye public kabla ya kuzungumza ni tatizo.

Usijibu chochote kupitia huko, kama ukiweza mpe muda then discuss naye hiko kitu.
 
Pamoja na kwamba wengi watakuambia 'ni marehemu' lakini inaonesha kuwa mmeo amefanya hivyo kwa kusudi fulani. Kuna ujumbe anataka kukufikishia arguably kwa njia isiyo sahihi. Yeye kama mwanaume na kichwa cha familia hakutakiwa kutumia njia hiyo kukufikishia ujumbe alioudhamiria ambao kwa thread yako inaonesha hata hujaupata ila umekwazika - rightly so!

Basi cha kufanya bi Nyakwaratony ni kumkalisha chini na muyazungumze yote yaliyowakwaza kisha umuombe siku nyingine akikwazwa akuambie directly badala ya kutumia mizunguko mingi ambayo badala ya kusuluhisha huenda ikaongeza mikwaruzo zaidi.

Wewe ambaye kwa sasa ndiyo upo calm basi uchukue hatua kuzungumza naye.
 
Back
Top Bottom