Ni nani Mkali wa DANCING duniani kwako? Binafsi, C. Brown hashikiki ila M. Jackson ni TIMELESS!

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari zenu wale wapenzi wa dancing na wapenzi wa burudani kwa ujumla.

Mimi binafsi sio dancer mkali, ila NAJITAJIDI sana kudance. Napenda kucheza muziki. Kila naposikia muziki unaochezeka na mazingira yananiruhusu, huwa nacheza! Siongelei taarab au kukata viuno, naongelea type za kina Usher, Genuine, C. Brown etc.

Binafsi mimi HANIELEZI mtu kuhusu ujuzi wa Michael Jackson na kucheza, NAMKUBALI balaa huyu King of POP, May his soul rest in peace! Jamaa ka-inspire dancers wengi sana, kanifanya nami nipende kudance.

Na kwa kizazi cha hivi karibuni, kulikuwa na Usher, Genuine na baadhi ya makundi kama kina N-Sync etc waliokaribu kuwa dancers wakali, ila kwa sasa jamaa Chris Brown kwangu hana mpinzani. Jamaa ni mbunifu, na pia ana originality ya hali ya juu. Anashuka mziki wowote. Nikiangalia video kama ms. China, zero, she aint you, loyal etc nakosheka vibaya, kwa wale madansa watakubaliana nami.

Usher alikuwa mzuri ila yuko poa zaidi ktk choreographed dancing na group dancing, akienda solo sio mbunifu sana.
Jamaa Jason Delure nae anajitahidi sana.

Upande wa makundi kuna kundi moja la USA nililiona Youtube, linaitwa JABBAWOCKEEZ, jamaa fulani wanavaa masks, ni shida!
Pia kwa UK kuna DIVERSITY, jamaa wazuri pia upande wa makundi.

Hapa bongo kwa kweli bado sijaona dancer, upande wa wasanii. Diamond na Alikiba ni zile dance za kuelekezwa na mwalimu alafu unakariri steps!

Nimewahi muona Wyre wa kenya akicheza, anajitahidi sana!
Mnyama TID hamna kitu, huwa ananyonga nyonga tu mikono na huwa hana sync na mziki.
Huu ni mtazamo wangu!

Je kwako, kwa kutumia vigezo vya:
-Originality
-Flair
-Creativity
-Deliverance
-Na dancing kwa ujumla, unamkubali nani duniani na hapa bongo??
 
Dah hao Jabawockeez nakumbuka final yao na Status Quo na wenzao Fysh n Chicks ,

Michael Jackson hana mpinzani aisee ,B2K walijaribu ,Criss brown hana pia Mpinzani kwa sasa
 
Hao jamaa wa mamasks ni shida! Yeah, kina omario walijaribu, alafu pia omario anaweza flani! Ila Cris Brown hana mpinzani kwa sasa!
 
hahahaaaaaaa,eti mnyama ananyonganyonga mikono tu,ngoja akusikie,ila kwa diamond asingepewa tuzo ya best dancer ya afrika kama hajui kucheza,sasa cjui wewe unatumia vigeao gani kwani naamin hata huyo breezy ana steps nyingi za kufundishwa darasani na anazipractice
 
Nami napenda sana kucheza muziki,kila style mpya inapotoka huwa najipinda hadi niiweze!
Kwenye suala la nani ni mkali wa dancing huwa nakosa hasa wa kumpa hicho kikombe baada ya the late MJ.
Chris yuko poa,na Usher yuko poa pia.
Hata huyo Jason DeRulo anaweza kwa kiasi chake.
Ila kibongo bongo umemsahau Msami mkuu,haka kajamaa kanaweza bwana.

BTW,umenivunja mbavu ati TID hajui kucheza,ngoja Muuza Sura akusikie...lol
 
kwa Bongo Msami ndio anatisha na kundi ni T Africa walishinda Dance Mia ilioendeshwa na EATv na walishiriki Sakata Mashariki iliojumuisha makundi mbalimbali kutoka East Africa na uko walishinda.
 
Habari zenu wale wapenzi wa dancing na wapenzi wa burudani kwa ujumla.

Mimi binafsi sio dancer mkali, ila NAJITAJIDI sana kudance. Napenda kucheza muziki. Kila naposikia muziki unaochezeka na mazingira yananiruhusu, huwa nacheza! Siongelei taarab au kukata viuno, naongelea type za kina Usher, Genuine, C. Brown etc.

Binafsi mimi HANIELEZI mtu kuhusu ujuzi wa Michael Jackson na kucheza, NAMKUBALI balaa huyu King of POP, May his soul rest in peace! Jamaa ka-inspire dancers wengi sana, kanifanya nami nipende kudance.

Na kwa kizazi cha hivi karibuni, kulikuwa na Usher, Genuine na baadhi ya makundi kama kina N-Sync etc waliokaribu kuwa dancers wakali, ila kwa sasa jamaa Chris Brown kwangu hana mpinzani. Jamaa ni mbunifu, na pia ana originality ya hali ya juu. Anashuka mziki wowote. Nikiangalia video kama ms. China, zero, she aint you, loyal etc nakosheka vibaya, kwa wale madansa watakubaliana nami.

Usher alikuwa mzuri ila yuko poa zaidi ktk choreographed dancing na group dancing, akienda solo sio mbunifu sana.
Jamaa Jason Delure nae anajitahidi sana.

Upande wa makundi kuna kundi moja la USA nililiona Youtube, linaitwa JABBAWOCKEEZ, jamaa fulani wanavaa masks, ni shida!
Pia kwa UK kuna DIVERSITY, jamaa wazuri pia upande wa makundi.

Hapa bongo kwa kweli bado sijaona dancer, upande wa wasanii. Diamond na Alikiba ni zile dance za kuelekezwa na mwalimu alafu unakariri steps!

Nimewahi muona Wyre wa kenya akicheza, anajitahidi sana!
Mnyama TID hamna kitu, huwa ananyonga nyonga tu mikono na huwa hana sync na mziki.
Huu ni mtazamo wangu!

Je kwako, kwa kutumia vigezo vya:
-Originality
-Flair
-Creativity
-Deliverance
-Na dancing kwa ujumla, unamkubali nani duniani na hapa bongo??

Uliowataja hao wote ni fake na siyo original.....wacheza dansi wakali ni wamakonde wacheza sindimba na wamasai tu.
 
hahahaaaaaaa,eti mnyama ananyonganyonga mikono tu,ngoja akusikie,ila kwa diamond asingepewa tuzo ya best dancer ya afrika kama hajui kucheza,sasa cjui wewe unatumia vigeao gani kwani naamin hata huyo breezy ana steps nyingi za kufundishwa darasani na anazipractice
Diamond ni kweli performance zake stejini ni emergetic na burudani, ila kama nilivyosema, kama solo dancer hajiwezi, anachochezaga ni ktk group dancing unafuata tu routine mlizopewa na choreographer wenu, nadhani yule mpenzi wa Aunt Ezekiel ndo dancer ila sio Diamond.
Mnyama kama nikimuona live labda ana kitu cha ziada ila kama dancing zake ni kama nionavyo ktk tv, hata mimi naweza mknock out one on one!
 
Uliowataja hao wote ni fake na siyo original.....wacheza dansi wakali ni wamakonde wacheza sindimba na wamasai tu.
C. Brown hata ukimuwekea mziki wa sindimba ni anausikiliza na kucheki rhythm zinaendaje kisha anashuka!
Ila ni kweli ulilosema kiaina.
 
Nami napenda sana kucheza muziki,kila style mpya inapotoka huwa najipinda hadi niiweze!
Kwenye suala la nani ni mkali wa dancing huwa nakosa hasa wa kumpa hicho kikombe baada ya the late MJ.
Chris yuko poa,na Usher yuko poa pia.
Hata huyo Jason DeRulo anaweza kwa kiasi chake.
Ila kibongo bongo umemsahau Msami mkuu,haka kajamaa kanaweza bwana.

BTW,umenivunja mbavu ati TID hajui kucheza,ngoja Muuza Sura akusikie...lol
Yap! Kibongo bongo Msami yuko poa, kwa mnyama, kimtazamo wangu kwa jinsi ninavyomupnaga ktk tv akijinyonga nyonga, labda niseme anajua ila wa kawaida sana. Huwa akicheza naona haendi na mziki alafu anayonga nyonga tu mikono na kusogeza sogeza miguu ktk hali ya kawaida kabisa!
 
Alafu naangaliaga malegend wa dancers, footwork, James Brown na Prince ni shida. M. J alipata footwork toka kwa James Brown.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom