NI NANI HAWA CULES?

NI NANI HAWA CULES?

mollel_afrika

Member
Joined
Sep 5, 2026
Posts
8
Reaction score
11
JIKUSANYENI WOOOOOTE!

Niwaandikie mshororo wa vina isiyo na mizani, niwaeleze kuhusu furaha ya soka na uchungu mkubwa wa mapenzi ya mpira wa miguu.

Ndio ule uchungu wa kuumizwa pale unapokuwa na kikosi kinachoaminika kuwa ni bora, halafu unakutana na mdhaifu anakufundisha jinsi ya kucheza.

Licha ya ubora wa hawa jamaa, Espanyol waliwafundisha jinsi ya kukusanya alama tatu.

Majina yao hayakutosha kuwafanya Levante wawasujudie, ama Getafe kuwasalimu kwa kuwapa vichwa.

Usiniambie ukubwa wa kikosi, niambie kilichotokea dakika tisini.

Maana hata Barça ya Ronaldinho iliwahi kufika kwa watakatifu wa Kanisa la San Mamés, kutoka Basque, kwa maana ya Athletic Club de Bilbao, ikarudi huku hesabu zikiwa zimewapiga chenga.

Kati ya mara 89 walizokutana kabla ya 2014, Blaugrana walifanikiwa kujichekesha mara 22 pekee, huku wakilia mara 49 na kuondoka bila heri wala shari katika michezo 18.

Ndio ni ile Bilbao, klabu ya familia ya Williams, ambao wanaifanya Hispania kama shamba la zabibu, na ngedere kazi yake ni kujichumia tu.

Kaka akicheza winga ya kulia na timu ya taifa ya Ghana, wakati mdogo mtu akicheza winga ya kushoto na timu ya taifa ya Hispania.

Watoto wa kabila la Catalan, yaani wanaopatikana katika taifa linalodai uhuru kutoka Hispania na kutambulika kama Catalonia, wanafahamu safari ya FC Barcelona kuwa miongoni mwa stori tata na zenye hisia mseto kwa kila anayependa soka.

Na mimi kazi yangu ni moja tu:
Kuhakikisha unafurahi na kuhuzunika kwa wakati mmoja.

Njooni nyote msome hapa, mshiriki pamoja ili niwape kila nukta itakayokamilisha neno katika sentensi iliyoijenga Barcelona.
Itaendelea.....


Mwandishi: Mwanafalsafa Joshua Mollel.
 

Attachments

  • 59121.jpeg
    59121.jpeg
    58.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom