Ni nani aliyewapa vibali vya Business permit badala ya work permit Huawei-tiGO?

TCRA ,TRA NA WIZARA YA KAZI

Katika kipindi hiki ambacho kila mtu mwenye mapenzi na nchi hii anahangaika ili tutoke hii sehemu na tusonge mbele, ni jukumu la kila mwenye nafasi kuitumia vizuri kufanya majukumu yenye tija kwa Tanzania.

Neno outsorcing (uhamishaji wa majukumu ya kampuni kwenda kampuni nyingine)limejitokeza sana Tanzania katika sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka 3 au 4 iliopita likihusisha kampuni kongwe na kubwa ambazo ni Airtel , Vodacom na tasisi za kifedha (mabenki)

Kwa sasa vitengo vyote vya watalaam wanaowezesha simu zetu kupiga na kupokea simu kwa hizi kampuni kubwa za Vodacom na Airtel vilishahamishiwa India muda mlefu.

Hii imewaacha watalaam wa kitanzania kubaki wamebung’aa kazi waliobaki nayo ni kuuza na kukwangua vocha maana hata voucher printing ni kazi ya m-South Africa

Zipo aina kuu mbili za outsorcing:

1. Outsourcing within the country(uhamishaji wa majukumu ya kikazi kwenda kampuni inayofanya kazi nchini)

2. Outsourcing outside the country (uhamishaji wa majukumu kwenda kampuni inayofanya hayo majukumu nje ya nchi.

Tanzania na watanzania kwa ujumla wetu hili neno sio zuri sana ingawa linaweza kutetewa kwa nguvu zote na wafanya biashara hasa wawekezaji.

Kwa aina ya kwanza ya outsorcing sio mbaya maana kampuni inahitaji kupunguza baadhi ya majukumu yake ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kupata faida.Hii huleta ufanisi na mbinu mpya katika kampuni na kuondoa desturi ya kufanya kazi kwa mazoea.

Madhara ya outsorcing yamejitokeza katika aina ya pili :

1. Watanzania kukosa ajira na kuleta madhara kwa mtu mmoja mmoja.

i. Mfano katika miaka ya hivi karibuni vyuo vingi hapa nchini vilianzisha fani za mawasiliano na uhamasishaji ukawa mkubwa ili kuleta mafanikio katika hii sekta ya mawasiliano. Kama sikosei ndo sekta inayozalisha watembea na bahasha wengi kwa sasa.

ii. Hawa ni vijana ambao tafiti zinasema ndio wanaoongoza katika matumizi ya simu na internet, hela zao ndo ambazo zinaenda kuwalipa mishahara vijana wenzao walioko India na Uchina.

2. Nchi kupoteza mapato

i. Fanya tathimini ya wafanyakazi wa Vodacom na Airtel mchango wao kama Pay As You Earn, ilikuwa kiasi gani na kwa sasa hilo pengo limezibwaje.

ii. Bora hayo mapato yaongezwe kwenye kodi yao ili nchi isipate hasara kwa maamzi ya mwekezaji.

3. Usalama (mambo ya udukuzi wa mawasiliano ya simu)

i. Hizi nchi zetu ambazo ni changa katika sekta ya mawasiliano kuna mengi yanaweza kujitokeza unaporuhusu mifumo yote ya kimawasiliano kwenda nje.Huwapa shida wawekezaji wanapokuwa na waajiriwa wazawa katika mifumo ya kampuni maana hujui uliemwajiri ni nani au ni mzalendo kiasi gani.

ii. Kazi hii huwa rahisi sana wanapokuwa na watendaji wote wa nje, ni bora kama TTCL yetu ingekuwa imara ingetusaidia baadhi ya number za viongozi wetu kutumia mfumo wa kwetu.

Ni ushauri kwa wenye mamlaka kama TCRA, WIZARA YA KAZI NA AJIRA,TRAkuliangalia hili suara kwa mapana, naamini tuna viongozi wa juu wazuri wenye mapenzi mema na nchi hii chini ya uongozi uliotukuka wa dr. J.P.MAGUFULI
 
Haya malalamiko yametulia na nina imani yamefika mahali pake. subiri tu JPM atafanya yake kama hao wahusika hawatuchukua hatua
 
Nimetafuta point katika haya maelezo inayoweza kuweka positive input katika uzi huu hakika sijafanikiwa kuiona......Tafadhali mkuu Andrew Nyerere unaweza saidia nijue point yako ni nini hapo?
 
Huyu Norman aliulizwa unapafahamu Namanga au ulishafika Kenya akasema hapana lakini passport yake inaonyesha alitokea Kenya. Hili nalo ni jipu.

Tunatumahini utalifanyia kazi hili JIPU.

Watu wananeemeka na ofisi za Umma! Anyway Miezi imeenda basi rudisheni mrejesho tuone kama JP anatimiza ndoto yake ya Hapa Kazi tu!
 
Mkuu hapo umemaliza kila kitu, sasa ni kazi ya Serikali kufanya yanayostahiri
 
procedure za uhamiaji nazo ni jipu tu maana hili suala linaongelewa sana hata mipakani na rwanda huko, watu wanaingia kama cheap labour wanapiga kazi kimya kimya maana kupata documents milolongoaf helakubwa...tujipange turekebishe kwanza uhamiaji wakati huo tunawakaba vilivyo hawa wageni wasannii(kuingia kwa magumashi)
 


lakini kumbuka,kinacho fanyika tigo huawei project ni ujanja ujanja,unacho ongelea wewe ni by books..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…