Ni nani aliyewapa vibali vya Business permit badala ya work permit Huawei-tiGO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani aliyewapa vibali vya Business permit badala ya work permit Huawei-tiGO?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gwijimimi, Jan 19, 2016.

 1. gwijimimi

  gwijimimi JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2016
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 6,587
  Likes Received: 1,448
  Trophy Points: 280
  LHUAWEI TIGO PROJECT:

  Je, ni nani aliyewapa wachina na wahindi hawa vibali vya "BUSINESS VISA" badala ya "WORK PERMIT"?

  Tangu tarehe 04-01-2016 wageni wakiokuwa wakifanya kazi hapa Huawei Tigo project kwa vibali vya CTA tangu vipigwe marufuku na waziri wa kazi na baada ya ukaguzi wa kina wa uhamiaji walianza kukimbia ofisi nakutokuja ofisini huku wakifanyia kazi majumbani kwa kutumia njia ya VPN(virtual private network). Lakini majira ya jion na usiku huonekana ofisini wakiendelea kufanya kazi zao kama kawaida. Rais JPM, Je Serikali yako ikifika usiku nayo inaenda kulala?

  Kama ujuavyo any foreigner is a boss pia wakiendelea kutupa majukumu kama boss kama kawaida. Sasa basi haya yote tuliyaripoti uhamiaji kwa zile ermegency contact zao na baadhi akiwemo mkuu wa idara ya ufuatiliaji hapa kinondoni. Lakini bila mafanikio.

  Ikionekana kabisa kuwa kunaendekea figisu figisu ndani ya uhamiaji kinyume na utendaji wa Rais wetu mpendwa Mhe. Magufuli.

  Hii hali imeendelea mpaka jana, sasa cha ajabu leo wachina, wahindi wa hapa Huawei-Tigo project (kijitonyama -Derm house 1st floor) wameingia wengi na kufurahia kuwa wamerudi kazini kama kawaida tukiwauliza kuwa mmepata work permit wamekiri kuwa work permit ni kazi kuzipata lakini kampuni ya Huawei imetutafutia BUSINESS VISA ambayo hutolewa na immigration kwa ajili ya kufanya kazi kama business trip.

  Sasa wafanyakazi wazawa tumeshangazwa na hatua na mpango madhubuti wa serikali ya away ya tano na kasi ya HAPA KAZI TU ikifanyiwa mzaha na baadhi ya watendaji wa uhamiaji either kwa maslahi binafsi au kutokuwa na mlengo wa uzalendo wa nchi au kutaka kwenda kinyume na kasi ya raisi wetu mpendwa.

  Hii business visa zimetolewa kidanganyifu maana hawa foreigners ni boss wetu na wanafanya kazi hapa wengine wana mwaka mmoja na zaid kama Boss Zhang Dong, Fu shiyou , Fen Gui, n.k

  Pia na GNOC boss Arul Doss, Pia wengine maboss wamekuwa wakija kazini lakini tuna utata na work permit zao walizokuwa nazo haziendani na kazi wanayoifanya kama HR wetu ni mchina Chen Xuli ambaye akifuatiliwa ana work permit ya kitu kingine kabisa ambacho sicho ambacho anachokifanyia kazi maana nitashangaa serikali yetu makini impatie mgeni work permit ya HR ambayo mtanzania anaweza kufanya,

  Pia bado tukiwa na HR consultant Fan Xiliang ambaye yeye ni sawa lakini si huyu Chen Xuli aliyesomea English leo ni HR wetu katika hii project wakamleta HR assistant Andrew Ikangula (Mtanzania) ambaye hathaminiki kabisa.

  Pia kuna binti mmoja aitwaye Guan Shanmei (Mchina) ambaye ana work permit ambayo pia hatuna uhakika ni ya nini maana kiuhalisia anafanya kazi ya receipt checkup for retirement ambayo mtanzania anaweza kufanya ambaye akionyesha uwezo wake hafifu alishawahi kutuma mishahara ya staffs kwa bahati mbaya kwenye email ya staffs ambapo mishahara ni siri kubwa,

  Pia walipokuja kukaguliwa na immigration alionyesha uwezo mdogo sana mpaka akampiga picha immigration officer akachukuliwa kwenda ofisi za uhamiaji figisu figisu zikafanyika akatolewa kwa muda mfupi sana.

  Tuna mengi ya kulalamika lakini kwa ofisi stahiki za kushughulikia haya mambo tunaomba yashughulikiwe maana hatutachoka kufanya further escalation ili tuenende na kumuunga mkono Raisi wetu Dr Magufuli.

  Pale uhamiaji kuna majipu mengi tu ya kutumbuliwa pia kuna wageni wengi ambao pia passport zao zilionekana zimegongewa mhuri wa namanga boarder of Kenya na passport ya Norman (mZimbwabwe) ikachukuliwa kwa ufuafiliaji lakin kesho yake alirudishiwa na kila kitu kikabaki kimya figisu. Huyu Norman aliulizwa unapafahamu Namanga au ulishafika Kenya akasema hapana lakini passport yake inaonyesha alitokea Kenya. Hili nalo ni jipu.

  Tunatumahini utalifanyia kazi hili JIPU.
   
 2. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2016
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,974
  Likes Received: 1,856
  Trophy Points: 280
  haya majipu yalipuliwe wakatwe kwa wembe
   
 3. mshipa

  mshipa JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2016
  Joined: Jun 16, 2015
  Messages: 7,090
  Likes Received: 11,718
  Trophy Points: 280
  Uhamiaji wachunguzwe
   
 4. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2016
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  tanzania......ni zaidi yauijuavyo!
   
 5. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2016
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 5,120
  Likes Received: 2,678
  Trophy Points: 280
  Na wewe ukiandika uwe unaweka paragraph basi:mad:
   
 6. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2016
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 3,100
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Tangu tarehe 07-01-2016 wageni waliokuwa wakifanya kazi hapa huawei Tigo project kwa vibali vya CTA tangu vipigwe marufuku na waziri wa kazi na kutakiwa kuomba work permit na baada ya ukaguzi wa kina uliofanywa na uhamiaji hawa wageni walianza kukimbia ofisi nakutokuja ofisin huku wakifanyia kazi majumbani kwa kutumia njia ya VPN(virtual private network), huku majira ya jion na usiku huonekana ofisin wakiendelea kufanya kazi zao kama kawaida, kama ujuavyo any foreigner is a boss pia wakiendelea kutupa majukumu kama maboss kama kawaida.

  Sasa basi haya yote tuliyaripoti uhamiaji kwa zile ermegency namba walizozitoa lakini kilichojiri ni kusikilizwa na kutotendewa kazi na baadhi akiwemo CIO(chief investigation officer) Pima lakin bila mafanikio ikionekana kabisa kuwa kunaendelea figisu figisu ndani ya uhamiaji kinyume na utendaji wa rais wetu mpendwa Mhe. Magufuli.

  Hii hali imeendelea mpaka jana, sasa cha ajabu leo wachina na wahindi wa hapa huawei-Tigo project(kijitonyama -Derm house 1st floor) wameingia wengi na kufurahia kuwa wamerudi kazin kama kawaida tukiwauliza kuwa mmepata work permit?

  Baadhi yao wamekiri kuwa work permit ni kazi kuzipata lakini kampuni ya Huawei imewatafutia BUSINESS VISA kwa gharama ya usd 700 ambayo hutolewa na immigration pale airport ukiwa unafika Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi kama business trip, sasa wafanyakazi wazawa tumeshangazwa na hatua na mpango madhubuti wa serikali ya tano na kasi ya HAPA KAZI TU ikifanyiwa mzaha na baadhi ya watendaji wa uhamiaji either kwa maslahi binafsi au kutokuwa na mlengo wa uzalendo wa nchi au kutaka kwenda kinyume na kasi ya raisi wetu mpendwa.

  Hizi business visa zimetolewa kidanganyifu maana hawa foreigners ni boss wetu na wanafanya kazi hapa wengine wana mwaka mmoja na zaid kama Boss Zhang Dong,bFu shiyou, Liton Saker, Jun Jun n.k. Hii pia imetushangaza kuona kuwa passport zao zilikusanywa na kampuni ya Huawei ili wampelekee mtu wa immigration (ambaye hajulikani) ili awagongee mhuri kama wamefika nchini ambapo si kweli maana walikuwa wakiendelea kuishi katika apartments zao.

  Kutolewa kwa business visa kwa wageni wanaoendelea kuishi Tanzania na kufanya kazi za wazawa ni fedheha kubwa na kinyume na hotuba ya Raisi aliyohutubia bungeni tarehe 21/11/2015.

  Pia wengine maboss wamekuwa wakija kazini lakini tuna utata na work permit zao walizokuwa nazo haziendani na kazi wanayoifanya kama HR wetu ni mchina Chen Xuli ambaye akifuatiliwa ana work permit ya kitu kingine kabisa ambacho sicho ambacho anachokifanyia kazi maana nitashangaa serikali yetu makin impatie mgeni work permit ya HR ambayo mtanzania anaweza kufanya, pia bado tukiwa na HR consultant Fan Xiliang ambaye yeye yupo vizuri sana na ni sawa kwa ajili ya company mediation lakini si huyu Chen Xuli aliyesomea English leo ni HR wetu katika hii project wakamleta HR assistant Andrew Ikungula(Mtanzania) ambaye hathaminiki kabisa na hata mambo ya msingi ya ki HR akiwa mbali hivyo wamemuweka kama gelesha tu.

  Pia kuna binti mmoja aitwaye Guan Shanmei(Mchina) ambaye ana work permit ambayo pia hatuna uhakika ni ya nini maana kiuhalisia anafanya kazi ya receipt checkup for retirement ambayo mtanzania anaweza kufanya ambaye akionyesha uwezo wake hafifu alishawahi kutuma mishahara ya staffs kwa bahati mbaya kwenye email ya staffs ambapo mishahara ni siri kubwa.

  Walipokuja kukaguliwa na immigration alionyesha uwezo mdogo sana mpaka akampiga picha immigration officer mmoja aitwaye Lema akachukuliwa kwenda ofisi za uhamiaji figisu figisu zikafanyika akatolewa kwa muda mfupi sana.

  Tuna mengi ya kulalamika lakini kwa ofisi stahiki za kushughulikia haya mambo tunaomba yashughulikiwe maana hatutachoka kufanya further escalation ili tuenende na kumuunga mkono Raisi wetu mpendwa Dr Magufuli.

  Pale uhamiaji kuna majipu mengi tu ya kutumbuliwa pia kuna wageni wengi ambao pia passport zao zilionekana zimegongewa mhuri wa namanga boarder of Kenya na passport ya Norman (mZimbwabwe) ikachukuliwa kwa ufuafiliaji lakin kesho yake alirudishiwa na kila kitu kikabaki kimya figisu.

  Huyu Norman aliulizwa unapafahamu Namanga au ulishafika Kenya akasema hapana lakini passport yake inaonyesha alitokea Kenya. Hili nalo ni jipu.

  Immigration kuna majipu makubwa na yameiva yanahitaji mtumbuaji mzuri na makini.
  UPDATES:

  Uhamiaji wametinga ofsini huawei
   
 7. dafity

  dafity JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2016
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 890
  Trophy Points: 280
  Umeandika kwa UCHUNGU sana. Ushahidi wa kutosha, ila hofu yangu JF nani atayetekeleza?
  Acha niwa copy wahusika
  c.c.
  1. Jeshi la Uhamiaji
  2. Wizara ya mambo ya ndani.
  3. Huawei Tigo Project

  Labda itasaidia. Asante kwa UZALENDO
   
 8. T

  Tibet Senior Member

  #8
  Jan 19, 2016
  Joined: Dec 30, 2015
  Messages: 173
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mhmmmmm,hoooooo huuuuuuuu,
   
 9. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2016
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,503
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  Maafisa wa uhamiaji ni wala rushwa sana! Hiyo mihuri ya boda itakuwa imegongwa mtaani kwa md tgl.
   
 10. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2016
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 3,100
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Hii Nchi watu wamefanya shamba la bibi nashangaa hata amri ya raisi inachezewa hv....

  Hizi kampuni za telecom zimeoza sana
   
 11. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2016
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  Hapa ndio waafrika tunaonekana machizi. Waziri a naenda kufanya ziara ya kushtukiza anaibua maroroso ya kutosha,kumbe watendaji waliofatana nae wanamng'ong'a wanasubiri arudi wizarani warudi kukusanya rushwa.

  Mijitu ya aina hii ni ya kufunga kwa uhaini ili iaipate hata dhamana.

  Hakuna nchi duniani ya kueleweka ukafanya kazi ya kueleweka huku ukiwa bosi wa wazawa bila kuwa na proper documentation.

  Kwa mwendo huu magufuli anatwanga maji kwenye kinu.
   
 12. msafwa93

  msafwa93 JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2016
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,759
  Likes Received: 2,554
  Trophy Points: 280
  kwa nini Rais asianzishe ofisi maalumu kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya mitandaoni.???
   
 13. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2016
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,631
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Aisee basi hii nchi huenda ikamshinda Magu mapema
   
 14. taamu

  taamu JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2016
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 4,528
  Likes Received: 778
  Trophy Points: 280
  Unaandika kwa umakini ila unachokosea ni kusema ni serikali ni makini.wakati idara ya uhamiaji ni serikali pia.hakuna kitu kitafanikiwa kwenye hii nchi.
   
 15. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2016
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 3,100
  Likes Received: 2,123
  Trophy Points: 280
  Kwa kasi waliyoanza nayo tukaamini sasa kazi imeanza kumbe kuna watu wanazunguka mlango wa nyuma...
   
 16. mchumia tumbo

  mchumia tumbo JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2016
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 1,390
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Naamini wamekupata,jukwaa hili lilishawahi vuta matokeo ya interview,hope hata haya madai yatawafikia wahusika.
  Sometimes hii ni njia bora ya kufikisha kero.Kuliko kulitumia jukwaa kwa kutoa matusi na kejeli
   
 17. c

  chenga mchina Member

  #17
  Jan 19, 2016
  Joined: Jan 19, 2016
  Messages: 5
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hii hali ya hapa ofisini siyo kabisa maana yote yaliyosemwa ni kweli na Amina maana tangu tumehamishiwa kutoka tigo kwenda huawei wageni wamekuwa wengi sana kuliko tulivyokuwa tigo na wakati teknolojia ni ile ile lakini kwa sasa kuna wageni takribani 34 hapa wakiwa wana business visa tu bila vibali vya work permit.

  Sasa wameanzisha idara mpya ya GNOC ihamie india huku ajira za hapa watanzania wakiachishwa kazi ili waajiriwe wahindi huko India.
   
 18. taamu

  taamu JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2016
  Joined: Dec 11, 2012
  Messages: 4,528
  Likes Received: 778
  Trophy Points: 280
  na ndipo wanaoamini umoja husema mbuzi hawezi kufanikiwa katikati ya chui wenye njaa.mgufuli ana kazi au ahasi au ajiunge nao.jambo ambalo nahisi ndio jepesi zaidi.tuangalie kikwete asijekuwa malaika kwa magu.
   
 19. LWENYI

  LWENYI JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2016
  Joined: Jul 4, 2013
  Messages: 1,405
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Aisee haya mabaki ya msoga bado ni magumu sana kutumbuka!
  Yanaamini yana nguvu kuzidi serikali yenyewe!
  Na yanaprove hilo sasa Mh.Rais haheshimiki namna hii itakua sisi wapiga mayowe?
  Hapa ndo ninapoelewaga maana ya mfumo!
   
 20. S

  SEBM JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2016
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Poleni sana kwa yaliyotokea hapo Tigo Huawei Project. Wakati ikiwa sina ni na dhamira ya kupinga ulichoandika, naomba nikupatie elimu na ufahamu juu ya mambo ya uhamiaji na vibali vya kufanya kazi.

  1. Idara ya uhamiaji - kwenye mipaka au ofisi zao - hawatoi business visa. Hizi zilikuwa replaced na CTAs kulingana na Sheria ya Uhamiaji ya 1995 na regulations zake.

  2. Kulingana na Sheria ya Uhamiaji ya 1995, Mkurugenzi wa Uhamiaji alikuwa ana mamlaka ya kutoa vibali vya kufanya kazi kwa muda mfupi (CTAs). Hizi ni kazi za ushauri, miradi nk. Uhai wa vibali hivi ni miezi 3 au siku 90.

  3. Kutungwa kwa Sheria ya kusimamia mambo ya ajira ya mwaka 2015 na kanuni zake iliyoanza kutumika 15.09. 2015 ilibadilisha baadhi ya vipengele vya sharia ya uhamiaji ya mwaka 1995 na hivyo kumpa mamlaka Kamishna wa kazi kusimamia na kutoa vibali vyote vya ajira.

  4. Kwa kuwa kulikuwa na harakaharaka ta kutekeleza sheria na pia kukidhi matakwa ya kisiasa (mambo ya ajira za wageni yalikuwa sehemu ya agenda za Magufuli wakati wa Kampeni) na kutokana na sharia mpya kunyang'anya mamlaka yeyote ya utoaji wa vibali vya ajira kwa Uhamiaji, Kamishna wa Kazi alikuwa na changamoto kubwa ya kusimamia utoaji vibali vya muda (zamani CTA).

  5. Sasa ni sharti kila mtu anayekuja nchini kwa kazi ya pungufu kwa miezi 6, aombe - in advance - kibali cha muda mfupi (short term permit) kwa kamishna wa kazi kwa ada ya USD 500.

  6. Uhamiaji hawana mamlaka ya kutoa kibali chochote cha kazi, bali sharia hii mpya inawapa majukumu ya kumsaidia Kamishna wa Kazi kufanya Ukaguzi sehemu za kazi na kuhoji, kukagua na kukamata yeyote ambaye hana kibali cha kazi (mamlaka haya wamepewa pia Polisi na Maafisa Kazi).

  7. Uhamiaji kulingana na Sheria ya 1995 wanalo jukumu bado kusimamia "ukazi" wa watu. Kwamba ukipata kibali cha ajira cha muda mrefu kutoka Labour (Wizara ya Kazi na Ajira...) kwa ada ya dola 500, 1000 au 0, bado Uhamiaji wana mamlaka ya kutoa kibali cha ukazi (Residence Permit) kwa dola 2050 (labda kama imebadilika).

  8. Kwa sasa, ukitoka airport, visa pekee wanayokugongea Uhamiaji ni "tourist".

  9. Hata hivyo kutokana na heka heka hizi za mambo ya vibali vya wageni, kuna habari zisizo rasmi kuwa serikali inalegeza masharti na hivyo itarudisha utaratibu wa Business Visa (uliokuwa replaced na CTA) na hivyo kwenye entry points mtu unaingia nazo na kufanyia kazi zisizo na kipato (mkutano, semina, warsha etc).

  10. Hadi leo jioni, hayo hapo juu 1-10 ndiyo yaliyokuwa yanafanywa na mamlaka zetu mbili ambazo ziko wizara mbili tofauti ndani serikali moja (Mambo ya ndani na Kazi, Ajira, Sera.....)

  Kama una maswali bado tunaweza kusemezana "inbox"
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...