Ni nani aliyeacha alama ya mguu kwenye jiwe hili la Morogoro?

Secret Star

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
1,708
1,553
Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza swali hili bila kupata majibu yanayoeleweka!,

Ni kuhusu alama ya unyayo wa mguu wa kushoto na mkito wa fimbo ulioachwa kwenye jiwe pale kwenye milima ya Uluguru Morogoro.

Safari hii nilitinga tena maeneo yale kwa ajili ya kufanya utafiti hasa ni kipi ambacho kilipita hapo, ambapo unyayo unaonekana dhahiri kuwa ni wa
Binadamu!

1. Kwa jinsi hali ilivyo inaonyesha mtu huyo ambaye aliacha alama ya unyayo na fimbo eneo hilo alikuwa anaruka kutoka mahari pamoja kwenda
pengine!

2. Inaonyesha alitua kwenye lile jiwe juu ya kinara cha mlima akiwa anaruka kwenda upande wa chini, (Morogoro mjini kwa sasa)

3.Inaonyesha kuwa alikuwa akitembea na fimbo kubwa ambayo alikuwa nayo akitembea.

4.Inaonyesha alitua kwenye jiwe hili kutoka kwenye vilele vingine vikubwa vilivyo nyuma ya kilele hicho, Umbali km kama 3!

Baada ya kushuhudia hayo nilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi wazee wakongwe wa milimani huko ambao walidai hizo hatua wao walizikuta,
huku wakisema kuwa na mababu zao walidai nao walizikuta! Kifupi wazee wote kwa vizazi na vizazi walizikuta hizo hatua hivyo haijulikani ninani hasa ambaye alipita!

Baadhi ya imani za wazee na mababu wa kale wa eneo hilo walidai kuwa hiyo ilikuwa ni Hatua ya Mungu!, alipokuwa akiutengeneza ulimwengu!
Wengine walidai kuwa hiyo ilikuwa ni hatua ya Shetani!.

Kifupi kuna madai mengi ambayo yalikuwa yakitolewa na vizazi kuhusu hatua hiyo na haijulikani la kweli ni lipi!

(Jambo la kukatisha tamaa!)

Imani za watu zimezaa jambo jipya! wao huamini kuwa kwenye jiwe hilo kuna nguvu! hivyo wengi wanaenda hapo kunoa visu na mapanga yao! mpaka sasa hatua zile zinazidi kupoteza uhalisia wake! sababu ikiwa ni watu kwenda kunoa visu na mapanga yao kwa shughuri zao katika hilo jiwe!

(NACHUKUA WAKATI WA KUFIKIRIA)
Baada ya hapo nilirudi Dar es salam ambako sasa kwa akili yangu mwenyewe nilianza kuwanza mambo mengi mfululizo! Ni mwanadamu wa aina gani huyo ambaye aliweza kuruka lile eneo?! Sijawahi kuona kitabu chochote cha historia kikielezea kama walishawahi kuwepo Binadamu ambao
walikuwa na nguvu hiyo! Sijawahi kuona mahala popote kwenye vitabu vya
imani vikieleza kama kuna muda waliwahi kuishi watu ambao walikuwa na uwezo kama Mtu yule aliyeruka pale!

Baadhi ya Imani za Dini na Historia zinadai kuwa Binadamu wa zamani walikuwa ni wakubwa! ila cha kushangaza mguu ule ni wakawaida kabisa sawa ni Binadamu wa kawaida wa sasa!

Swali nilililonalo mpaka sasa ni nani ambaye aliruka pale Morogoro! sijawahi kusikia kisa kama hiki popote Duniani! Naombeni wazee wa kupasua vichwa kwa kufikiiri mnisaidie mnafikiria nini hapo?


 
Hujaandika vizuri hii mada. Mantiki inapotea kila ukisoma sentensi inayofuata. Hatimaye unafika mwisho inabaki kuwa na maswali mengi. Kama huna uwezo wa kujieleza vizuri walau ungepiga picha ukatuwekea. Tujenga stories sisi wenyewe.
 
Hujaandika vizuri hii mada. Mantiki inapotea kila ukisoma sentensi inayofuata. Hatimaye unafika mwisho inabaki kuwa na maswali mengi. Kama huna uwezo wa kujieleza vizuri walau ungepiga picha ukatuwekea. Tujenga stories sisi wenyewe.
Picha kaweka. Ila jiwe lenyewe halitambuliki kama ni la volkano ama jiwe jabali, kutokana na rangi yake lilivyo.
Maelezo ya aina ya jiwe ingetusaidia kuungaunga stori na za kule Arusha sijui Kilimanjaro zilikoonekana nyayo za watu wa kale kwenye mawe ya jamii ya volkano.
 
Unyayo uliodidimia kwenye jiwe gumu pia unapatikana Iringa, Wilaya ya Mufindi, Kijiji Cha Ifwagi eneo linaitwa Nyonga. Eneo hilo halina makazi bali ni eneo ambalo lilikuwa linatumika kuchungia mifugo. Niliushuhudia unyayo huu kwa macho yangu enzi hizo nikiwa nachunga mbuzi. Haijulikani ni nani alikanyaga pale. Nakumbuka tukiwa watoto tulikuwa tukijaribu kupima miguu yetu kwenye alama ile ya unyayo.
 
Huyo Jamaa itakua alikua anapenda kupita kwenye milima
 
 
 
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…