Ni namna gani ya kushangaza uliweza kujua kwamba rafiki yako ni tajiri

Naona wengi wanazungumzia watu wenye uwezo wa kati, maana mtu kua mkuu wa kitengo cha jeshi mama kua mbunge bado hakukufanyi kua ni tajiri..wengi nyumba zinawachanganya..
 
Primary nilisoma na Watoto wengi wa vigogo enzi hizo za Mwalimu tuli kuwa tuna wajua kwa majina ya baba zao kwani kila siku tuli kuwa tuna Wa sikia wakati Marehemu Mzee Devid Wakati ana Soma taarifa ya Habari .

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Maisha ndio yapo hivyo mwenye pesa huwa hana mambo mengi utaona tu kuwa budget na vitu anavyo miliki ndio utajua kuwa huyo sio saiz yako.
 
Nimeangalia baadhi ya maoni ya watu kuna kitu kikubwa sana watu hawaelewi kuhusu utajiri kwa nchi zilizo ulimwengu wa tatu kama Tanzania, maana nimeona kuna watu wamehoji kumiliki Toyota Land Cruiser V8 ni utajiri?

Pato la wastani la mwananchi wa Tanzania kwa mwaka ni $1,090 (Tshs. 2,512,559.05) kwa mujibu wa wizara ya fedha chini ya taasisi ya taifa ya takwimu NBS kwa mwaka wa fedha ulioisha mwezi wa sita mwaka jana. Je, mtu (mbunge na wakuu wengi wa taasisi za umma) anayepokea mshahara kwa mwaka kiwango kisicho pungua Tshs. 90,000,000 pamoja na posho ni mtu wa kipato cha kati kwa Tanzania?

Kwa mataifa ya dunia ya kwanza kama Marekani mtu tajiri huanzia $ 1,000,000 (Tshs. 2,305,100,045.38) huwezi kutumia vigezo vya dunia ya kwanza kutafsiri utajiri kiutaalamu zaidi sawa sawa na dunia ya tatu unless if you're working for magazines like forbes, wao wanatumia kigezo kimoja kumpima mwananchi aliye mahala popote ulimwenguni ili aingie ktk list zao. Ni tofauti kabisa ukilinganisha na vigezo vinavyotumika na benki ya dunia (WB) au shirika la fedha (IMF) au OECD.

Japokua mtoa mada anaonekana haku-factor in vitu kama being rich vis-à-vis living large, tafiti nyingi sana zinaonyesha watu wengi they're living large yaani endapo vipato vyao vikikata hawawezi ku-survive kwa standard ya maisha yale yale kwa zaidi ya miezi 12. Mf wa living large wengi wao huwa na flashy lifestyle magari ya gharama na mijumba mikubwa yenye kumbi za cinema na mabafu 5 in leafy suburbs kibongo bongo maeneo kama Masaki, Oyster Bay au Njiro. Kwa Tanzania mtu yeyote yule anayeweza kumiliki gari kama Toyota Land Cruiser V8 lenye thamani zaidi ya Tshs. 80,000,000 si mtu mwenye kipato cha kawaida ni tajiri kwa maoni yangu mimi.

Thamani ya Tshs. 80,000,000 ukiwa na nidhamu ya matumizi kwa nchi za ulimwengu wa tatu unaweza kuitumia zaidi ya miaka 10 ktk familia yenye watu 5. (under ceteris paribus including inflation rates)
 
Kongole mkuu
Wewe umenipata vyema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa ana x5 lakini yupo kundi moja na Paul Allen dah! Maisha haya kama Caranteen ya wagonjwa wa Corona Hospital moja tu wote Tajiri na Masikini
 
sasa hao uliowataja ni matajiri au watu wenye ahueni ya maisha?kuna tajiri aliyeajiriwa kweli?
 
Tang'ana,
kuna tajiri aliyeajiriwa kweli?

Wapo wengi sana, hawa ni baadhi ya mimi ninao wafahamu na taarifa zao rasmi zimethibitishwa na Forbes;

  • Steve Ballmer (Microsoft) - $ 59B
Huyu kwa sasa amestaafu na nafasi yake mwisho alikuwa ameajiriwa kama mtendaji mkuu. Aliajiriwa kama mfanyakazi wa 30 mwaka 1980 na Bill Gates baada ya kumaliza chuo kikuu cha Harvard. Japokuwa alifanya kazi kidogo Proctre & Gamble.
  • Eric Schmidt (Google) - $ 14.9B
Baada ya kufanyia usahili(interview) watu wengi sana, wagunduzi wa Google Larry Page na Sergey Brin walivutiwa na hiki kichwa wakaamua kukiajiri kama mtendaji mkuu (CEO) wa Google kuanzia mwaka 2001 mpaka 2011.
  • Sheryl Kara Sandberg (Facebook) - $ 1.6B
Huyu amefanya kazi wizara ya fedha ya Marekani na baadae Google. Huyu aliajiriwa Facebook na Mark Zuckerberg as chief operating officer mwaka 2008 mpaka sasa bado yupo ktk hiyo nafasi. Huyu ndiye aliyefanya mabadiliko makubwa ktk business model ya Facebook mpaka wakaanza kutengeneza faida. Before she joined, the company was primarily interested in building a really cool site; profits, they assumed, would follow.
  • Tim Cook (Apple Inc.) - $ 1.3B
Huyu ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Apple tokea mwaka 2011 mpaka sasa. Aliajiriwa na Steve Jobs kama msaidizi wake worldwide operations.
  • Roberto Goizueta
Coca-Cola CEO from 1980 to 1997. One of the first non-founder executives to have become a billionaire. No longer alive.
 
Kuna kabinti fulani hivi nilikutana nako fb,nilkua nakaa nako mji mmoja siku naonana nako nilikaona ka kawaida mno ndo kalikua kamemalza form 4..aisee siku kamenipeleka kwao nilbaki natoa macho tu mjengo niliokutana nao ni laana zmepaki ndinga 3 za maana,moja bonge la V8 jeupe..akanigusia tu baba ake anafanya kazi Canada..hyo V8 baba ake alipewa zawadi siku ya birthday yake na kaka ake anaeishi ujerumani..nikahoji kaka ako na dada ako je wako wapi,kaka ake ansoma sweden na dada ake anasoma australia sikuendelea kuhoji,ule msemo ukanijia kichwani, usi mdharau usie mjua binti mwenyewe ukimkuta mtaani unaweza sema kwao maisha magumu
Hako Kabinti itakuwa ni Mdogo wake @kidukulilo
 
Habari wakuu

Natumaini kuna watu umekuwa nao na tumesoma nao na wanatokea kwenye familia tajiri ila bila kujua wala kuwafahamu kwa kuwa watu hao wanakuwa na tabia za kawaida na wanaopenda kujichanganya.

Mimi wakati nasoma O level nilikuwa na rafiki ambae aliamia kipindi tukiwa form 2 kutokea kusini.

Basi kutokana na kupenda story za movies tukawa marafiki mi nikawa namchukulia poa tu.

Tulikuwa tukiwafata madem wanamdharau kwani alikuwa wa kawaida tu na hana swaga so mimi ndio nilikuwa namsaidia kumpigia mapande japokuwa mengi yalikuwa yanachomoa.

Bwana wee ikafikia Siku ya karibia na kumaliza kidato kukaagizwa kikao cha wazazi jamaa walikuja wazazi wote wawili na mi V8 kila mmoja.

Baba kaja na V8 jeupe mama kaja na la damu ya mzee aisee sikutegemea yani na dogo alikuwa hana shobo nao wala nini... ye yupo kujichanganya na masela hana hata habari na wazazi wake.

Baba yake alikuwa sijui na cheo gani jeshini huku mama akiwa ni mbunge wa jimbo la kusini hukoo

Kuanzia hapo ndo watu wakaanza kumuheshimu, Masista wakaanza kumuelewa kweli sasa.

Kuna watu ni huwa hawapendagi show off.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Ally Kiba tu.Hapend show off.
Ahahahahabahah
 
Yupo mmoja pia chuo tulikuja kumgundua siku ya graduation....

Jamaa alikuwa simple sana hana tabia za show off na cha kushangaza WhatsApp haweki profile picture wala hajawahi kuweka status tangu namfahamu

Nilipowahi kumuuliza alinijibu hapendi tu.

Sasa cha kushangaza siku ya graduation alikuja na BMW X5 Mpyaaa kabisa

Tulipomuuliza alisema ameuza BMW x3 yake aliyokuwa anamiliki kitambo tu ndo kanunua hilo X5...

Kuna watu huwa ni ma silent mkuu acha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmmhh sasa mkuu si unaweza enda azima tu kwa iyo siku then unarudisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom