Ni namna gani ya kushangaza uliweza kujua kwamba rafiki yako ni tajiri

Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,110
2,000
Habari wakuu

Natumaini kuna watu umekuwa nao na tumesoma nao na wanatokea kwenye familia tajiri ila bila kujua wala kuwafahamu kwa kuwa watu hao wanakuwa na tabia za kawaida na wanaopenda kujichanganya.

Mimi wakati nasoma O level nilikuwa na rafiki ambae aliamia kipindi tukiwa form 2 kutokea kusini.

Basi kutokana na kupenda story za movies tukawa marafiki mi nikawa namchukulia poa tu.

Tulikuwa tukiwafata madem wanamdharau kwani alikuwa wa kawaida tu na hana swaga so mimi ndio nilikuwa namsaidia kumpigia mapande japokuwa mengi yalikuwa yanachomoa.

Bwana wee ikafikia Siku ya karibia na kumaliza kidato kukaagizwa kikao cha wazazi jamaa walikuja wazazi wote wawili na mi V8 kila mmoja.

Baba kaja na V8 jeupe mama kaja na la damu ya mzee aisee sikutegemea yani na dogo alikuwa hana shobo nao wala nini... ye yupo kujichanganya na masela hana hata habari na wazazi wake.

Baba yake alikuwa sijui na cheo gani jeshini huku mama akiwa ni mbunge wa jimbo la kusini hukoo

Kuanzia hapo ndo watu wakaanza kumuheshimu, Masista wakaanza kumuelewa kweli sasa.

Kuna watu ni huwa hawapendagi show off.

.....Kisa kingine......

Kuna kisa moja nilikisoma Quora kilitokea nchi za uarabuni hukoo

Palikuwa na mgahawa kama ulivyo Mac Donald's mtaa fulani sasa moja ya wafanyakazi akawa anasimulia

Kwamba siku moja walikuwa wanahitaji wafanya kazi sasa wakawa wameweka kibao cha tangazo kwamba wanaajiri. Kumbuka Ajira kama hizi za kuuza restaurant kwa nchi za kiarabu ni zimezoeleka kufanywa na watu wenye vipato vya chini.

Basi mara akajitokeza kijana akamwendea mkurugenzi wakati huo na huyo mfanyakazi mwengine yupo hapo akiwasikiliza wakiongea

Dogo: nimeona kibao cha tangazo manaaajiri

Mkurugenzi: ndio, ulikuwa unahitaji ajira?

Dogo: ndio boss, kwani kuna nafasi gani?

Mkurugenzi: Kuna nafasi ya kitchen assistant na waiter/waitress

Dogo: nitachukua ya waiter au muhudumu

Mkurugenzi: upo tayari kuanza lini kazi?

Dogo: kesho mapema asubuhi

Baada ya mazungumzo dogo akaondoka.
Have you notice something strange there..?
Ni kwamba dogo hakubageni kuhusu mshahara....

Jamaa alishangaaa sanaa kwani hapana mahali paliwekwa wazi kwamba mshahara utakuwaje kwa saa kwa kipindi hicho mshahara huwa ni kati ya $5 mpaka $10 kwa saa inategemea na mwajiri.

Basi kesho kufika dogo akawahi akaanza kazi mapema sana na alikuwa hamble na mwenye furaha.

Aliifanya ile kazi kwa unyenyekevu na heshima kubwa kwa miezi mitatu mfululizo. Then one day akaja akiongozana na mtu mzima wa makamo ambae alionekana ni mtu tajiri na kijana mwenzie pamoja na mfuko uliokuwa umewekwa vitu.

Alipofika counter alivitoa vile vitu kwenye mfuko lahaulaaa..... zilikuwa ni saa 4 za gharama kubwa, alikuwa amewalete zawadi, hapo moja inachezea $20,000 akawakabidhi kila mfanya kazi pamoja na yule msaidizi na mkurugenzi jumla walikuwa wanne.

Then baada ya hapo Akaskika akimwambia yule mtu mzima aliefatana nae kwamba...

"I told you, I could make it"

Ikaja kufahamika kwamba yule mtu mzima ni Baba yake mzazi anamiliki makampuni ya mafuta na ni tajiri sana na alibeti na baba yake kwamba anaweza kufanya kazi za hali ya chini... baba hakuamini

Wafanyakazi wote walibaki na mshangao

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kizzy Wizzy

JF-Expert Member
Aug 2, 2013
3,110
2,000
Yupo mmoja pia chuo tulikuja kumgundua siku ya graduation....

Jamaa alikuwa simple sana hana tabia za show off na cha kushangaza WhatsApp haweki profile picture wala hajawahi kuweka status tangu namfahamu

Nilipowahi kumuuliza alinijibu hapendi tu.

Sasa cha kushangaza siku ya graduation alikuja na BMW X5 Mpyaaa kabisa

Tulipomuuliza alisema ameuza BMW x3 yake aliyokuwa anamiliki kitambo tu ndo kanunua hilo X5...

Kuna watu huwa ni ma silent mkuu acha kabisa
Ni rahisi kuficha kama wewe kwenu kuna uwezo kwenye level hiyo ya elimu ila kwa level ya chuo ngumu sana hata ufanyaje hata uwe sio wakuvimba na kuShow off ila watu watajua kama wewe kwenu kuna kitu.

Portfolio | 2020
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nima Imma

JF-Expert Member
May 14, 2015
2,322
2,000
Mm wala si shule ni kitaa cha kukutaniana tu jamaa lilikuwa bonge chafu chafu tu , anakibanda cha chips tulikuwa tunapenda kukaa tu nae kupiga story na nini muda uende aiseee kumbe bhana mshikaji ni anahela balaaa migorofa kkoo yani pale kwenye chips za jioni ni kupenda tu kuishi maisha ya kawaida sana, kuna watu hela kwao ni kitu cha kawaida mnoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Joh Doe

Senior Member
Sep 23, 2019
159
1,000
Umenikumbusha bilionea mmoja alikua anaitwa Paul Allen (mwanzilishi mwenza wa Microsoft pamoja na Bill Gates), mwezi wa sita mwaka 2018 nilibahatika kukutana nae Serengeti alikuwa yupo na wamasai anapiga nao soga. They had no clue who he was, and how much loaded he was.

Hakuna kitu kizuri kama kujichanganya na watu halafu hawajui kama una mfuko mpana au la (stealth wealth). Inakuepusha vitu vingi sana kuanzia marafiki bandia mpaka business proposals kila mtu anataka uweke pesa ktk mipango yake.

Always avoid being flashy (kama upo mjini endesha magari madogo madogo, mf IST au Carina), don't splash your lifestyle on social media.
 

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
683
1,000
Kuna mmoja yupo group la WhatsApp ni tajiri na wote hatukujua,
Siku tunabadilishana mawazo akatukaribisha Kwake ni Arusha bwana weee kwenda kwenda kwa Maelekezo tukajikuta tumasimama mbele ya boonge ya mgorofaaaa.....

Kilichofata ni historia, kumbe ule mjengo ni wa kwake na yeye ndo anaishi hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana we jamaa unashoboka Sana,ukifika Kwa MTU unaanza kumuuliza uliza hiki cha Nani,unashngaa magari etc,mpaka huyo jamaa kakujibu shombo nimeuza X3 sasa hvi Nina X5,hqta mm ukinikuta mahali nakunyoosha Tu ili uache kutafuta hela uwaze kupost ujinga kama huu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
51,150
2,000
Ni rahisi kuficha kama wewe kwenu kuna uwezo kwenye level hiyo ya elimu ila kwa level ya chuo ngumu sana hata ufanyaje hata uwe sio wakuvimba na kuShow off ila watu watajua kama wewe kwenu kuna kitu.

Portfolio | 2020
Watajuaje? Kama mtu ameamua kukaa hostel na wenzie, anapokea boom kama wenzie na anakula canteen kama wenzie tutajuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,557
2,000
Watajuaje? Kama mtu ameamua kukaa hostel na wenzie, anapokea boom kama wenzie na anakula canteen kama wenzie tutajuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pressure za kusubili boom utakuwa huna, vile vipindi vya pasi ndefu boom limekata utakuwa havikupati, kukopakopa kawaida kwa mwanachuo wewe hutakopa na kukopwakopwa kawaida 100K nk kioindi watu wanasota...kuna life huwezi kuliigiza au ku-fit hapo ndipo some questions mark zitakuja kwa jamaa huyu vipi mbona hayaface tunayo yaface.

Mshikaji wangu kwao maDon anaishi kawaida ila pressure kama hizo hatawai zi face.

Portfolio | 2020
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
1,916
2,000
Pressure za kusubili boom utakuwa huna, vile vipindi vya pasi ndefu boom limekata utakuwa havikupati, kukopakopa kawaida kwa mwanachuo wewe hutakopa na kukopwakopwa kawaida 100K nk kioindi watu wanasota...kuna life huwezi kuliigiza au ku-fit hapo ndipo some questions mark zitakuja kwa jamaa huyu vipi mbona hayaface tunayo yaface.

Mshikaji wangu kwao maDon anaishi kawaida ila pressure kama hizo hatawai zi face.

Portfolio | 2020
We umewasema watu wenye uchumi wa kati mtoa mada amewasema madon.
Haya mambo ya kutokopa wala kutokuwa na hekaheka za boom hata mimi nayaweza sana wakati njaa kali home.
Kuna jamaa naishi nae ghetto mzee wake ana mashine za kukamua dhahabu, vitalu, gesti, ekari kibao, bajaj, gereji na miradi kibao. Huyu jamaa binafsi ana nyumba yake ya kuishi kaijenga mwenyewe kutokana na mishe alizokuwa anamfanyia mzee wake na ana kiwanja pia.
Sasa huyu mtu kwa kukopa ndo hatari, anakopa vibaya mno wakati kwao ana hela. Ukimtazama hivi utaona ni mtu wa chini lakini siku akiamua kuonesha makali watamtambua.
 

Moo Click

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
2,721
2,000
Ni rahisi kuficha kama wewe kwenu kuna uwezo kwenye level hiyo ya elimu ila kwa level ya chuo ngumu sana hata ufanyaje hata uwe sio wakuvimba na kuShow off ila watu watajua kama wewe kwenu kuna kitu.

Portfolio | 2020
Hata chuo wapo mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom