Ni mv skagit na sio sea gull imepinduka na haijazama bado iko inaelea

Nafikiria sana hiyo mechanism mpaka mtu asie umwa hata kidogo anyongwe na maji mpaka kufa!!!!!!!!!!! R.I.P all who went away!
 
Ilikuwa na abiria wangapi? Hivi bunge letu state of emergency ni hadi nin kitokee ndio bunge liahirishwe by unanimouse decision
 
malipo ya kuchoma makanisa na bar za wakristo....mungu hutenda haki.

hapana ndugu usiseme hivo, inawezekana kuna ndugu zako wafanyabiashara kutoka bara. Si malipo ni uzembe wa serkali yetu sikivu. Wewe magamba nini!!
 
Mie nafikiria sasa ipitishwe sheria ingawa "mama hana muda huo" Wachina wanaweza kabisa kutengeneza suruali za boya (Vacuum) ili kila abiria apewe anaponunua tiketi apewe na aingie kaiva, inawezekana, maana kusafiri majini sasa inakuwa kama unaenda vitani lazima uwe equiped
 
malipo ya kuchoma makanisa na bar za wakristo....Mungu hutenda haki.
MUNGU AWAREHEMU NA AWAPE NGUVU WALE WOTE WALIOOKOKA
Leo ndio tunasikia mitusi ya ajabu, kwanini Bunge haliahirishwi, haraka, nakubaliana na wote hii ni laana ya kuchoma makanisa na kuwadharau ndugu zenu wasio waislaam, na kutaka kuuvunja Muungano, Huku Bara hatukuinunua hiyo Meli na wala hatuna Mamlaka ya kuizuia, pili mlielezwa kabisa kuwa hali ya hewa ni chafu kwa muda wa siku 3 mfululizo
 
Haya majanga mpaka lini jamani? Poleni wafiwa na marehemu walazwe pema mbinguni.
 
Ama kweli kwa hali hii ni dhahiri kbs ya kwmb serikali hii ya wachumia matumbo yao ni DHAIFU!

Wote wale waliopatwa na janga hili nasema poleni sana na MUNGU AWALAZE MAREHEMU WOTE MAHALA PEMA PEPONI, Amen!
 
Wana JF tuiulize serikali yetu ya muungano na Zanzibar kwa msingi wa kitaakamu nchi hii inatakiwa iwe na helkopta na vifaa gani na vingapi kwa tahadhari ya janga kama hili? Bilioni 9 kana walivyopanga za kuwatibu viongozi wastaafu!! Wqatwambie!!
 
Kwake tumetoka na kwake tutarejea, Mola Mlezi awape makazi mema walotangulia, awape wepesi majaruhi ndugu jamaa, na Watanzania sote kwa jumla. AMINA
 
Tukio moja hufuta kumbukumbu ya tukio lingine kwa tz mfano mabomu ya gongo la mboto na kikombe feki cha babu wa loliondo ccm ni very creative kwa poteza tukio dr.uliomboka pona haraka
 
Nashindwa ku-connect haya matukio ya kupoteza roho nyingi kwa wakati mmoja katika kipindi fulani. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi tukio la kuzama kwa MV Islanders lilitokea wakati wa heka heka za kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani. Hili la MV SeaGull limetokea wakati wa heka heka za kuanza mfungo wa Ramadhani!

Wakati tukiwapa pole wote waliopoteza ndugu, jamaa, na marafiki katika matukio haya ya "ajabu"; wenye macho ya rohoni kuna kitu cha kujifunza hapa. Huenda adui ameanza kazi zake waziwazi bila kificho sasa - TULIOMBEE TAIFA LETU. Hakika haitatanguka yodi wala nukta moja ya Torati hata yote yatimie. AMEN.
 
Jamaa hao ni kiboko, wameongea na Mzee huko juu naye akawakubalia na kuwatengenezea bonge la upepo.
Na upepo haukufanya ajizi, ukapindua boti hapohapo.
 
Nashindwa ku-connect haya matukio ya kupoteza roho nyingi kwa wakati mmoja katika kipindi fulani. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi tukio la kuzama kwa MV Islanders lilitokea wakati wa heka heka za kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani. Hili la MV SeaGull limetokea wakati wa heka heka za kuanza mfungo wa Ramadhani!

Wakati tukiwapa pole wote waliopoteza ndugu, jamaa, na marafiki katika matukio haya ya "ajabu"; wenye macho ya rohoni kuna kitu cha kujifunza hapa. Huenda adui ameanza kazi zake waziwazi bila kificho sasa - TULIOMBEE TAIFA LETU. Hakika haitatanguka yodi wala nukta moja ya Torati hata yote yatimie. AMEN.
 
Naona kuna watu wanaleta utani katika tukio la kusikitika kama hili, napenda tuelewe huu msiba utakuwa umetugusa Watanzania sote iwe Bara au Viswani kwani kuna ndugu zetu tele kule Mawimbini ,kiwengwa na etc kila kukicha wamo safarini, pia tumechanganya damu, hili halina ubishi, hayo mambo ya laana za kuchoma Makanisa na Mabaa hayana uhusiano hapa ni chuki binafsi Makanisa ya kwanza yameanza kujengwa Zanj na vibali kilitolewa na walokuwa Mfalume wa wakati huo ambao walikuwa Waarabu na Waislamu ni kusema yamekuwapo Zanzibar Miaka zaidi ya 100 ilopita na sijasikia kuchomwa moto, acheni chuki binafsi au nyie wakimbizi hamzijui offside trick za siasa za TZ, mbona wahusika hawajakamatwa?
Ama hayo Mabaa miaka nenda rudi yamekuwapo na Hotel mbali mbali zinajulikana, African House, Zanzibar Hotel, Starehe Club, Golf Club, Police Mess, na hizo nyumba za Kuuza gongo na kangara Kikwajuni, Miembeni Kwa alinatu na etc etc idadi hazina mbona hazija chomwa Moto iweje leo???? Ukiambiwa jiambie unafikiri walevi wanaojaza hizo baa ni nani? Joseph Au David? think twice! leo si siku yake I will be back for this one Day
Leo ningeli penda tukatafakari zaid juu ya haya maafa, maisha ya Watanzania yanayopotea kila kukicha inauma sana, leo wao Kesho unajua ni nani ? hivi kama juhudi za kusudi hazija chukuliwa kudhibiti matukio kama haya au kujitayarisha na hayo mambo Emergency Disaster Management, rescue squards, mobile Medical Teams, mass Causality Managements, equipment for Rescue and resuscitation ! tungeweza kuokoa watu wangapi??
Hivi ni kudura za Mwenyeenzi Mungu uzembe au ?? hiyo meli siijui lakini kweli ina uwezo wa kuchukua abiria 280? mamlaka ya hali ya hewa hawakuuona huu upepo? hizo helikopta zinafanya nini? Serikali imejitayaisha au imejifunza nini kwa majanga kama haya ambayo si ya kwanza! kutokea? Nini tufanye sasa hivi na in the future?
Hatua gani wahusika kama watajulikana wamehusika na uzembe zitachukuliwa? fidia, matibabu ya ziada, referal na etc
Nakumbuka mimi mdogo kulikuwa na meli za Maendeleo na Mapinduzi ni mapipa hasa yamekenda wapi uliwahi kusikia mambo kama haya hii ni mifano ya mambo ya kujiuliza na kuyatafakari.
Loh! Wakuu naona kama nimekuja na moto kidogo nivumilieni yanauma sana, Nawakilisha!
Mola Mwenyezi awarehemu na kuwalaza pema Walotangulia Sisi tuliwapenda Bwana amewapenda zaid, na majaruhi wapoe Haraka AMIN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom