Ni muhimu kufuta vyama pinzani nchi hii

Ni muhimu kufuta vyama pinzani nchi hii

Mtazama MAMBO

Senior Member
Joined
May 20, 2014
Posts
159
Reaction score
24
Ndugu zangu Watanzania, umefika wakati sasa wa nchi yetu kuwa na chama kimoja, kilicho asisi uhuru wa nchi hii na kujenga udugu, upendo na umoja, yaani tanu na sasa ccm.
Nayasema haya kwa sababu,
1. Kwa sasa nchi imegota, mipango na bajeti waliyopitisha waheshimiwa wabunge wetu imeshindwa kutekelezeka! Na hii ni kutokana na ufinyu wa uzalendo wa chadema baada ya kupeleka umbea kwa wazungu ambao walipaswa kutoa sehemu yao katika bajeti yetu. Sasa tunasota watz WOTE! Tukibaki na ccm tu, haya hayatakwepo.
2. Ule umoja na kuwatii viongozi wetu hakuna tena. Wakati wa ujana wangu kulikuwa na kitu ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM. Na ile ilikuwa kama dua, maana kweli mwenyekiti alikuwa anapewa mafikira mazuri mazuri. Leo hii chadema na wapinzani wengine wanadiriki kutamka hadharani eti rais ni Mdhaifu mara KACHOKA!
Kwa maneno haya ataachaje kuchoka na maneno yanaumba?

Rudini nyumbani ccm enyi wana wapotevu. Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. CCM oyee!
 
Back
Top Bottom