Ni muda wa adhabu, tuache maneno

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,495
24,212
Tangu awamu hii imeanza kazi kumekuwa na speed kubwa ya kiutendaji kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu hasa Mkuu wetu Mh JPM na watu wake wa chini.
Tukiwa kama watanzania bila shaka wote kwa wingi wetu tunahitaji maendeleo na maisha bora, ili kufikia maendeleo na maisha bora kwa karne hii lazima kuwe na speed ya kiutendaji,kimaamuzi na kimatokeo maana muda sio rafiki tena kwetu.
Utendaji, Maamuzi na matokeo lazima yawe sahihi na yenye maslahi kitaifa.

Matatizo makubwa ya nchi hii watanzania wote wanayajua, penye makosa makubwa ya kiutendaji na kuleta hasara kubwa kwa taifa mpaka likabaki nyuma kimaendeleo watanzania walio wengi wanaelewa, Uozo wa kila taasisi katika taifa hili tayari kila mtanzania anaujua na kuwajua wahusika mpaka kwa majina.

Huu sio muda tena wakutuambia watanzania kila uozo mnaouna kama matokeo ya ziara zenu, hatuhitaji kuambiwa maana mtakuwa mnarudia tayari huku mtaani tunafahamu kila aina ya uozo kwenye taasisi tofauti tofauti KINACHOTAKIWA SASA NI ADHABU KWA WAHUSIKA. TISS, TAKUKURU,POLISI,MAGEREZA,JWTZ ni mali ya watanzania na viko kulinda dola na kupokea amri. tuwaadhibu sasa wahusika kama makosa yao na nyie mmeyaona au tunawaogopa?
Jela tunazo, vitanzi vipo kwanini amri za adhabu zisitoke maana kila kitu tulikijua na nyie mnakijua sasa. MANENO SIO MUDA WAKE NI WAKATI WA KUADHIBU WAHALIFU MAANA WAKATI UMESHATUTUPA MKONO.

Ramadhan kareem.
 
downloadfile-28.jpeg

bado naisoma number.

swissme
 
hivi unajua hii nchi inaitwaje, hasa ya upande wa bara ukitoa T na uweke D? usinijibu! ila ulizia Masamaki na wenzake baada ya kupata dhamana kwa sh 2.6 bilioni wameenda wapi? na ndo utajua jina la nchi hii.
 
ukweli ni kwamba sijui Masamaki alienda wapi baada ya kupata dhamana labda utusaidie maana wale wengi tunaowafahamu wanaotutia hasara kila kukicha wako mtaani tunawaona na wengine bado ni waajiriwa serikalini wanaendelea kula mshahara kila mwezi... pale HESLB Mama kaenda baada ya kuchukua hatua naye anatuambia tatizo lililopo, hao wezi wametuibia miaka nenda rudi lakini bado wapo wanadunda tu..
 
Back
Top Bottom